Askofu Bagonza(KKKT): Hivi viongozi wa dini wana mipaka kusema juu ya mienendo ya nchi? Hiyo mipaka imeanza lini?

26166514_10155962664961726_3483064440778089644_n.jpg

Yamkini na hapa ni kanisani na alikuwa anahubiri :D:D:D
 
Tunaendesha nchi kwa Divinity na theology? Nonsense!
Utakuwa lofa na mjinga mpaka lini?
Hapo sijajibu uzi nimejibu post ambayo mchangiaji alileta maandiko ili kuhalalisha udhalimu, ndipo nikamweka sawa.
Au wewe umgeni jf, maana inaonyesha hujui jinsi inavyooperate.
 
Sisi waislamu jamani tuna bahati mbaya,,
hii miviongozi yetu imebakia unafiki tu,, lkn yote sababu haina elimu ya dunia,,, walichokijua wao kufuga midevu ,,,aisee inakera,,aswa Hawa bakwata,,, bora sheikh ponda ndo angekuwa mkuu wa waislamu
Mkuu waislamu tunaugulia chini chini tukiongea sisi maneno yanakua mengi hatusikilizwi wala kuungwa mkono tunaonekana tunlalamika sana..alafu sisi kuwekwa ndani fasta tu lakini askofu hawezi wekwa ndani
 
Hizi akaunti zetu za JF tunazitumia na nani? BAK nimekuamini kwa miaka kutokana na jinsi ulivyotumia uwezo wa kufikiri kuchambua mambo. Lakini kwa mchango kama huu nashindwa kuelewa kama ni yule wa siku zote au BAK inatumika na watu au kundi fulani.

Swali la huyu Bangonza ni swali la kijinga. Nani ktk Dunia hii hana mipaka? Hata Rais ana mipaka. Yeye mchungaji au askofu ana mipaka, ndo maana wakilawiti watoto wetu wanatiwa hatiani. Mfano wako wa Rwanda, ni hao hao Mapadri waliochochea upuuzi na kushiriki mauaji.

Tatizo la wachungaji, maaskofu, mapadri wamezoea kushangiliwa ktk kazi zao. Hawaulizwi maswali na kupewa heshima hadi kuitwa 'Baba....' Ukiwa nao kwenye pombe, wanataka kulipiwa, njiani wanapewa lift bure, wakikosea na kupingwa wanadhani wamekosewa. sasa eti anauliza swali la kipuuzi kabisa eti kuna mipaka! Nani hana mipaka?
Kwa nini unamuunga mkono? Au ni huu utabili kwamba kila aliyekabwa dili mitaani anahisi kaingiliwa haki yake?
Inabidi ukapimwe akili na mkojo kuona coordination na ubongo wako maana unaumia nyuma kufikilia
 
Hawa Viongozi wa dini mie mwenzenu wananipa raha sana kwa jinsi wanavyomkabili Magufuli. Namuomba Mwenyezi Mungu awape ujasiri na sauti yenye nguvu ili waweze kumkabili huyu uchwara bila woga.

Hana hati miliki ya Nchi yetu. Tanzania ni yetu sote anapovurunda na kuipeleka nchi siko ni lazima tumwambie kweli tena hadharani na bila woga.

Kama hataki tumkosoe abwage manyanga arudi kwao Chato akafuge ng’ombe lakini hatuwezi kukaa kimya huku tukiona anaivuruga nchi yetu na kuipeleka kule ambako hatutaki ielekee.

Tumeyaona ya Rwanda, Burundi na nchi nyingine za kiafrika. Hatutaki hayo tuliyoyaona katika nchi hizo yatokee nchini mwetu.

Unahisi tukikupa nafasi yake unaweza kutupeleka tunapopataka???

Justify kwa sentensi tatu tu kuwa unauwezo wa kutupeleka nchi ya ahadi.
 
Yesu alishawahi kusema ya kaisari muachie kaisari naona viongozi wa dini wanasahau hapa.
Na pale wanapowaombea viongozi wa kisiasa mbona huwa hamsemi habari za kaisari?Acheni akili za kushikiliwa.
 
Utakuwa lofa na mjinga mpaka lini?
Hapo sijajibu uzi nimejibu post ambayo mchangiaji alileta maandiko ili kuhalalisha udhalimu, ndipo nikamweka sawa.
Au wewe umgeni jf, maana inaonyesha hujui jinsi inavyooperate.
Suppose mi mgeni. Ndo ulete mambo ya makanisani bila kumbukumbu ya subject yetu?
 
Yesu alishawahi kusema ya kaisari muachie kaisari naona viongozi wa dini wanasahau hapa.
Wakijenga hospitali hamsemi kaingilia ya Kaisari, wakijenga mashule, hatusikii mipaka ya siasa na dini, wakisema kiongozi yule ni chaguo la Mungu mnakenua mimeno, wakisema katiba imevunjwa: ooohhhhh toka madhabahuni, nenda kwenye jukwaa ka siasa, kooooommmaaaaa
 
Lakini kama mamlaka za kiserikali zinaongoza kwa kufuata katiba, kutenda Haki kwa wote na kuheshimu Haki za raia, mamlaka za kidini hazitaingilia.. Kumbuka, viongozi wa dini ni raia kama wewe(mwenye mamlaka) na wao kwao hakuna vyama, watu wote ni sawa mbele za Mungu. Wapo kwa ajili ya kuwafanya waumini wao(ukiwemo wewe) kujirekebisha pale wanapokosea ili wapate thawabu kwa Mungu.
Viongozi wetu wamekuwa wakijinadi kwetu tuwaombee, tutawaombeaji wakati wànatutendea ndivyo sivyo? Nani anaongoza maombezi hayo?
Hapa hatupimani kuelewa au kutoelewa mambo ya siasa na dini, lengo kuu ni kuwekana sawa ili kama jamii tubaki na thamani halisi kwa Mungu wetu. Mwongoza maombezi anapomwambia mtawala anayetaka kuombewa kuwa amekosea na anapaswa kutubu, ni suala la mtawala mwenyewe kujitathimini na kuona kama amekosea ama la, siyo matarumbeta ya wapambe kulalamika as if watahukumiwa pamoja naye.
Migongano ya mawazo na mijadala ya pande zinazokinzana huzaa mwafaka bora na hatimaye tunapata mambo mazuri ya kusimamia kama Taifa.
Kuna tatizo usiloona hapo kwa viongozi wa kidini. Ukiwasikiliza wote huzungumza kwa mamlaka kwamba huwa hawakosei. Mazoea yao huwaaminisha kwamba wote tunaoingia makanisani, sisi ni mali yao.

Kukosoa serikali siyo suala la viongozi wa dini kama kikundi maalumu. Kuna viongozi wa vyama vya wafanyakazi, kuna viongozi wa vyama vya wakulima, kuna viongozi vya wana-taaluma, kuna viongozi wa vyama vya wauza sokoni. Kwa nini Bagonza anaamini viongozi wa dini wana nafasi maalumu? Mbona ubora wao siyo mzuri kiasi hicho cha kuomba kukosoa na kuongoza serikali?
 
Inabidi ukapimwe akili na mkojo kuona coordination na ubongo wako maana unaumia nyuma kufikilia
Mmh! Nakusoma na hisia za kuwa uko mbele ya viongozi wa kidini wakikufanyia watakalo. Siyo kwangu! Kasma unaamini wanakusaidia kwenda Mbinguni wafuate, mkifika gizani najua kitakachokupata.
 
nachokiona kuna jiwe limerushwa kwenye kundi la mbwa....hizi kelele ni za usawa wa kichwa....mpaka miaka 10 iishe tutasikia mengi
 
Hawa Viongozi wa dini mie mwenzenu wananipa raha sana kwa jinsi wanavyomkabili Magufuli. Namuomba Mwenyezi Mungu awape ujasiri na sauti yenye nguvu ili waweze kumkabili huyu uchwara bila woga.

Hana hati miliki ya Nchi yetu. Tanzania ni yetu sote anapovurunda na kuipeleka nchi siko ni lazima tumwambie kweli tena hadharani na bila woga.

Kama hataki tumkosoe abwage manyanga arudi kwao Chato akafuge ng’ombe lakini hatuwezi kukaa kimya huku tukiona anaivuruga nchi yetu na kuipeleka kule ambako hatutaki ielekee.

Tumeyaona ya Rwanda, Burundi na nchi nyingine za kiafrika. Hatutaki hayo tuliyoyaona katika nchi hizo yatokee nchini mwetu.
Viongozi au watumishi wa Mungu wametumia hekima sana
Hawajakurupuka walisubiri wakati muafaka
Nadhani ni wakati wa viongozi wa serikali na chama tawala kutafakari mahubiri haya badala ya kutumia vyombo vya dola kuziba midomo ya watafutao Amani na Haki ya Kweli
Wajitafakari saaana kabla ya kufanya ambalo tutaliita 'Zoezi la Kipumbavu'
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kabisa Pakawa wahuni hawa wanadhani wana hati miliki ya Tanzania hivyo genge lao la wahuni wachache wanaweza kutuburuza Watanzania vile watakavyo.

Viongozi au watumishi wa Mungu wametumia hekima sana
Hawajakurupuka walisubiri wakati muafaka
Nadhani ni wakati wa viongozi wa serikali na chama tawala kutafakari mahubiri haya badala ya kutumia vyombo vya dola kuziba midomo ya watafutao Amani na Haki ya Kweli
Wajitafakari saaana kabla ya kufanya ambalo tutaliita 'Zoezi la Kipumbavu'
 
Huoni wapinzani wanavyokimbia vyama vyao na kukikimbilia chama pendwa?? Unasema wanachukiwa kumbe kaw mara ya kwanza rais inasemekana utafiti umeonesha anapendwa 100%?? Umemwona rais gani mwingine aliyependwa ka huyu??
Huu ni uchizi! Hii nchi ina watu vilaza sana
 
Back
Top Bottom