Askofu Bagonza: Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa Umma!

Askofu anaacha majukumu yake ya msingi sasa anaingia mzima mzima kwenye siasa zenye mlengo fulani.

Hatumpangii,ila tunamuasa kuwa na busara,ndio sifa kubwa ya viongozi wenzake wa dini.

Anaunga mkono maneno ya dialo??
 
Hii kauli ya vichokochoko wa Ikulu wangesema wapinzani wangeambiwa ni wachochezi wanataka kuleta machafuko nchini.

Mwendawazimu kawambukiza, ndio maana wamekua Washenzi wa Taifa.
Bi, Chokochoko mfano mzuri, na mwasirika mkubwa wa KICHAA. Anasema polisi wa CCM kuua mwisho risasi tatu. Zikizidi unafutwa upolisi.
 
Mwendawazimu kawambukiza, ndio maana wamekua Washenzi wa Taifa.
Bi, Chokochoko mfano mzuri, na mwasirika mkubwa wa KICHAA. Anasema polisi wa CCM kuua mwisho risasi tatu. Zikizidi unafutwa upolisi.
 
Walishangaa kwa sababu ulisema hadharani na kweli ungeweza kukamatwa, lakini waliikubali kauli yako. Yule dhalimu alimteka na kumuua Ben Saanane kwa kutaka elimu yake ifanyiwe uhakiki.
Hahahahahahahahahahaha
 
Askofu anaacha majukumu yake ya msingi sasa anaingia mzima mzima kwenye siasa zenye mlengo fulani.

Hatumpangii,ila tunamuasa kuwa na busara,ndio sifa kubwa ya viongozi wenzake wa dini.

Anaunga mkono maneno ya dialo??
Mbona huko kwa mafisadi mna askofu Gwajima akiunga waziwazi siasa za mrengo wenu hamlalamiki?
 
Mbona huko kwa mafisadi mna askofu Gwajima akiunga waziwazi siasa za mrengo wenu hamlalamiki?
Kaka chadema na ccm tofauti yao ni rangi za tishirt zao kuna haja gani ya kujinadi watafanya tofauti na ccm wakipewa madaraka!!!

Hayo yanatokea ccm,chadema nayo imekumbwa na mdudu gani!!!!
 
Askofu anaacha majukumu yake ya msingi sasa anaingia mzima mzima kwenye siasa zenye mlengo fulani.

Hatumpangii,ila tunamuasa kuwa na busara,ndio sifa kubwa ya viongozi wenzake wa dini.

Anaunga mkono maneno ya dialo??
Ukweli una sura au upande mmoja tuu. Ukweli ni ukweli tatizo tunaangalia kasema nani na sio kilichosemwa. Pia nyumba za ibada zinawezaje kujitenga na maisha ya watu? Si hawa hawa kina mwendazake na wengine wamekuwa wakitumia mimbari za nyumba za ibada kuhubiri maisha ya Si-hasa???
 
Hatupaswi kuongozwa na hisia bali uhalisia.

Bagonza amechagua kuwa msemaukweli kipindi cha jpm???

Pasipo kuamua kuikataa kweli anayoisema,tuhoji.anatuhakikishiaje kwamba anaosema ndio ukweli wenyewe hasukumwi na mambo mengine!!!

Ana tofauti gani na dialo ambaye kaamua kutema nyongo baada ya kunyooshwa na huyo anayemsema!!!vipi asingeguswa lini angeamua kuwa mkweli kwa niaba ya wengine??
 
INAFIKIRISHA! INASUTA! TUSUTIKE

Nilipochaguliwa kuwa Askofu baada ya wanaofaa kukosekana, marafiki zangu waliandaa tafrija ya kuniaga huko Chicago, Marekani. Mmoja wa watani wangu akatoa hotuba na kusema "Benson, wewe sasa ni Askofu. Tangu sasa una uhakika wa mambo matatu:

1. Daima utakula chakula kizuri
2. Daima utavaa vizuri
3. Daima hutaambiwa ukweli.

Ni miaka 19 tangu niambiwe na yote nimeyaona. Ufafanuzi wa niliyoyaona nitaufanya siku nyingine. Kimsingi Viongozi katika jamii tunaishi kwa kujidanganya, kudanganya na kudanganya.
Leo Nina hili:

Comrade Anthony Diallo amesema maneno mazito. Ametimiza ahadi ya mwana TANU/CCM isemayo "Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko". Ukweli uliochelewa ni bora kuliko uwongo uliowahi.

Nitoe ushauri ufuatao:

1. Viongozi na watawala wetu kama hawawezi kuzuia kusifiwasifiwa basi angalau wanune wakisifiwa.

2. Waliokwishamaliza muda wa uongozi wasijengewe masanamu au kutangazwa ni watakatifu mpaka muda maalum upite.

3. Ikithibitika kuwa kiongozi wa umma ngazi yeyote amewahi kuwa na tatizo la afya akili, maamuzi yake yote yatenguliwe.

4. Walioathirika au kunufaika na maamuzi ya kiongozi mwenye tatizo la afya ya akili wajulikane na kusaidiwa.

5. Itungwe sheria maalum kujinaisha (Criminalize) vitendo vya kusifia viongozi wa umma hadharani au kupendekeza ukiukwaji wa Katiba. Kuwasifia iwe sawa na kuwakashifu. Anayetaka kumsifia au kumkashifu kiongozi amwandikie barua binafsi. Kusifia hadharani ni rushwa.

6. Iwe marufuku wananchi kuwapigia makofi viongozi au kuwachezea ngoma, badala yake Viongozi wawapigie makofi wananchi na kuwachezea ngoma. Waliomba kutumwa, makofi ni ya nini?

Haya yote yanasisitiza msimamo wangu wa TUSUBIRI KUPONGEZA WALA KULAUMU.

Tangu enzi ya Mwalimu mpaka Samia, wanajitokeza watu wa kushinikiza kuvunja katiba ili Viongozi waongezewe muda wa kutawala. Wakiishakufa ndipo tunaanza kuambiwa mambo mazito yaliyokuwa yanaendelea nyuma ya pazia.

INAFIKIRISHA, INASUTA, TUSUTIKE.

View attachment 1848441
Law no One NEVER OUTSHINE THE MASTER. Let them flatter the master so they can live comfortably
 
Back
Top Bottom