Askofu Bagonza: Elimu yetu inafuta ujinga, Haiongezi maarifa. Kwani kikombe cha Babu si walienda hadi maprof, na maaskofu. Shida iko kwa Watanzania

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Ameandika Askofu Benson Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe

ELIMU YETU
Inafuta Ujinga, Haiongezi Maarifa

Duh!! Tanzania yetu inaumwa. Pole sana. Habari mbaya kila wakati. Taifa linaumwa sana.

Tuliona Samunge. Walikwenda madaktari, Maaskofu, Mitume, Wanajimu, Maprofesa, na wengine wasiotajwa kirahisi. Mzee wa kikombe ni mzalendo kweli. Kama mabeberu wangemtumia, tungekosa majeneza ya kuzikia. Tatizo hapo si ugonjwa. Ni kukosa maarifa. Kikombe kutibu magonjwa yote!!??

Tumeona Morogoro, Mbeya na kwingineko. Lori la mafuta linaanguka. Wenyeji wanaona Mungu kawakumbuka! Wanaiba mpaka betri ya gari. Mafuta yale na betri vina wateja mitaani. Eti serikali ipige marufuku!? Itapiga marufuku malori kuanguka? Elimu haijaongeza maarifa. Tunataka miujiza, tuibe katikati ya moto wa petroli bila kuungua.

Sasa umekuja upako. Mafuta, chumvi, maji, juice, vitambaa, na hata mikate. Si bure, kuna mtu anapata fedha. Sasa badala ya kukanyaga mafuta, tumekanyagana kwenye mishipa ya fahamu. Upako umetutoa roho. Eti serikali ihakiki vyeti vya Mitume na manabii? Subutu!! Wahakiki vyeti ndio wateja wa upako. Polisi anaenda kuwasaka mitume akiacha kidumu cha upako uvunguni mwa kitanda!! Ujinga umeondoka, maarifa hayajaripoti.
Kupenda vya bure, kupenda mafanikio bila kazi, ni donda ndugu.

Tuwe wapole, tujadili kwa nini:

- Watu wapewe chandarua halafu wanavulia dagaa,

- Watu wanakufa kwa mafuriko mabondeni, wengine wanajenga msingi siku hiyo hiyo bondeni,

- Serikali inafukuza watu mabondeni, huku inapokea kodi ya ardhi ya walio mabondeni,

- Manabii wa upako wapate vibali vya mikutano bila ulinzi wa polisi lakini Asasi zikose vibali hata kwa mikutano ya ndani!

- Serikali haijawapa maji safi wananchi, lakini wanaojichimbia kwa gharama, inawatoza kodi au kufungia visima vyao,

-Serikali inatangaza elimu bure. Inafuta karo ya elfu 70 lakini inakalia kimya michango inayofikia laki 6!

Duh! Kuna mtu kakanyaga mrija wa Oksijeni. Mgonjwa wetu atakata roho.

Leteni kodi ya ujinga, upako utakosa wateja. Tunavyopenda kukwepa kodi, tutajielimisha ili tusilipe kodi ya ujinga.

Poleni wafiwa, poleni watanzania.
Mnaopenda kutukana, msijisumbue. Ni heri kutukanwa kuliko kutukana. Unayo Ole ukitukana, ninayo Heri nikitukanwa.
 
Wekeni picha tuone walioenda kunywa kikombe Cha babu
images (2).jpeg
download.jpeg
images (1).jpeg
 
*Ameandika Askofu Benson Bagonza wa Dayosisi ya Karagwe*

Another stupid contribution. Yeye kama kiongozi wa dini au aliyesoma theology anatuambia nini juu ya Lady of Fatima and miracle of the sun. Kuna nini cha kuwashawishi watu hadi leo hii. Kuna mambo anatakiwa asiyahusianishe na elimu. Kuna mambo ambayo ni ya kijamii na hayana uhusiano na elimu. Ni sawa na kusema ukisoma usilie kwenye msiba kwa kuwa unafahamu kilichotokea.

Nchi gani imeendelea ambayo waliosoma hawafanyi mambo ya aina hiyo? Leo hii US bado watu hawataki vaccine!
 
Back
Top Bottom