Askofu Bagonza: CAG vs TAKUKURU

Acha kunipakazia matope! Inanihusu nini
Bia yetu inakuhusu hii
"Tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu" Dkt. Benson Bagonza, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?

Tupe mrejesho wa uchunguzi wa Kange Lugola na hatua iliyochukuliwa. Wananchi wajinga washaisha mjomba.
 
Kama Takukuru wanachunguza matumizi mabaya kwanini 2.7 trillions ambazo hazijulikani zilipo hawajachunguza kwa miaka miwili sasa kwa 1.5 trillion!?

Vipi kuhusu ripoti wizi wa “Mali za ccm” lini wataanza uchunguzi?

Takukuru ni genge la wahuni tu na halistahili kuwepo na sasa linatumika kuwachafua watu kwa kuokoteza uzushi tu na tuhuma za kweli wanazifumbia macho.

Katibu mkuu wa CCM Dr. Bashuri: CCM kuna majizi nikiyataja hapa mtashangaa. Sasa wezi wako CCM na ndio wenye serikali - JamiiForums
Huu Ubabe wa Mkulu... Mahara yake yatachukua generation kuyarejebisha.
 
VIJIWENI hakuna mtu anabishana juu ya DED na DC na CAG na DG-PCCB

Vijiweni hatujui wala hatujali kujua DED ni nini wala DG-PCCB ni nani

Wewe Askofu unakaa kijiweni, kijiwe gani?

Kwanza hutakiwi kukaa kijiweni tangia hapo.
Daa ! CCM wana uelewa mdogo sana wa mambo. Vipi kwenye kampeni zenu kutakuwa ubwabwa maharage?
 
CAG huwa anakagua vitu vichache

Mfano Chadema walidanganya kwa CAG fedha za ruzuku zinalipia deni la chama
Kumbe deni la chama alitengeneza Mbowe, fedha zinaingia kwenye mfuko wa Mbowe

Ila Takukuru wanakagua hatua kwa hatua

Lazima Mbowe aulizwe madeni feki yametoka wapi?

Wewe ndugu, likely una tatizo huko upstairs....

Ama wewe inawezekana ni li-robot fulani ambalo liko programmed na kuwekewa kiitikio cha "Mbowe na CHADEMA" kwa kila utakachooandika humu...!!

Askofu hajataja CHADEMA wala CCM ama chama chochote popote katika andiko lake, wewe huyooo unaingiza ishu za CHADEMA...

Ni wazi hata hujaelewa kilichomo kwenye andiko la Askofu Bagonza...

Pole sana...
 
Yaani takukuru wanaacha kumchunguza rais anayefanya manunuzi mbalimbali yakiwemo ya ndege kwa siri tena bila kufuata sheria ya manunuzi wanahangaika na chadema?
Yaani badala kufanya uchunguzi zilipo trilioni 1.5 zilizoibuliwa ma cag wanahangaika na beat za kisiasa? WHY? KWA NN?
Kweli
 
Kwanini inatumika nguvu kubwa ya kupinga takukuru wasifanye kazi Yao? Kuna nini chadema mpaka wanaogopa?
 
CAG na TAKUKURU

Watanzania wanapenda sana kushindanisha. Vijiwe vingi utakuja mijadala nani zaidi kati ya DC na DED, Waziri na RC, CAG na DG-PCCB, nk. Wanaweza hata kushindanisha hata visivyo na uhusiano kama nani zaidi kati ya Askofu na Mtendaji Kata, Nabii na Sangoma fulani, rubani wa ndege na dereva wa Bajaji au ungo.

Sasa kuna mjadala kuhusu nani zaidi kati ya CAG na TAKUKURU? Inahusu uchunguzi wa fedha za CHADEMA. Mmoja kasema vizuri alipobainisha kuwa kuna mambo ya Takukuru yasiyokuwa ya CAG. Ningeongeza, kuna mambo ya CAG yasiyokuwa ya Takukuru. Mmoja anatafuta wizi zaidi na mwingine anatafuta matumizi mabaya yenye harufu ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka. Nina matatizo mawili na suala zima:

1. Natamani uhuru (independence) aliyo nayo CAG wangelikuwa nayo TAKUKURU. Nawaomba wasinipige mawe. Kama wanao uhuru, basi mimi nawaombea zaidi. Kwamba, kwa utendaji wa sasa, tunaona Takukuru ni sehemu ya mfumo ule ule unaolalamikiwa na umma. Yaani ni halali mtu kujiuliza Takukuru wakiwa sehemu ya kamati za ulinzi na usalama wilayani, mikoani na taifa, wana uhuru gani wa kuwatuhumu, kuwachunguza, na kuwashtaki wajumbe wenzao wa kamati. Kadhalika, Takukuru wenyewe hawana chanjo ya kuzuia rushwa miongoni mwao. Rushwa ya ndani yao yaweza kuwanyima uhuru wa kushughulikia rushwa nje yao. Naonekana mnadharia zaidi? Hata mimi napenda kuishi eti! Lakini ni hatari kuwa na kundi la watu wanaofikiriwa kuwa wao hawawezi kujihusisha na rushwa.

2. Kinadharia CAG anawakagua au anaweza kuwakagua Takukuru. Kinadharia pia, Takukuru wanaweza kumchunguza CAG endapo atatuhumiwa au wao wenyewe wakitengeneza tuhuma na kuzichunguza. Uhalisia unaonyesha vyombo vyote viwili, siku za karibuni vinafanya kazi vizuri zaidi vinapoagizwa kuliko vinapoletewa tuhuma. Well, nani angeweza kufanya tofauti? Hata mimi nisingeweza. Ndipo ninapojitutumua na kusema, kama tuna dhamira ya kupambana na kuzuia rushwa katika taifa letu, tufanye matatu:

1. Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa. Anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Niwe wazi zaidi; wakati mwingi tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza sana katika kuwadanganya waliotuteua. Mioyo ya watu inaficha mengi.

2. Tuwekeze katika mifumo na kuziba mianya kuliko kutegemea umahiri wa mtu na uthubutu wa watendaji. Mifumo inatibu kuliko watu. Kinachotakiwa ni viongozi kuheshimu na kuitegemea hiyo mifumo. Mfumo utaeleza namna ya kumshughulikia kiongozi asiyefuata mfumo. Nitaambiwa "hayo yote tumeyashika tangu utoto". Tunapungukiwa na nini?

3. Tamaa ya rushwa haina chama, dini wala kabila. Ni kosa la kiufundi kupambana na rushwa kwa kufuata misingi hiyo. Wala rushwa wakiligundua hilo watakimbilia mahali pa salama ambako rushwa inavumilika na kamwe rushwa haitakaa iishe katika taifa letu.

Hoja yangu ni tuache kutukuza ukosefu wa uaminifu unaotunufaisha. Mtu akikosa uaminifu katika mambo yake, tukamtukuza kwa kuwa kukosa uaminifu kwake kunalifunaisha kundi letu, tujue dhambi hiyo itatokea tena na kuliangamiza kundi letu. Wengi wanasema hiyo ni siasa, mimi nasema maisha yetu na taifa letu yanaamuliwa na siasa. Kwa hiyo tukikubali kuwa katika siasa ni mahali pachafu, padipohitaji uadilifu, tuwe tayari kula uchafu maana jiko letu ni chafu.

Wenye mawe rusheni, lakini mjue kuwa mada inahusu rushwa. Kurusha jiwe ni sawa na kukiri wewe ni mla rushwa au unashiriki kuilea.
Ilikuwaje Eva akamsaliti Adam kwenye bustani ya Eden na binadamu tukapewa adhabu ya mauti. "Mwanzo 3:13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala."

Vipi na Yuda Iskariote kumsaliti Yesu. "Luka 22:3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara."

Matukio hayo ya kwenye Biblia yanadhihirisha kuwa Rushwa imekuwepo na itakuwepo milele kwa sababu mbalimbali za udhaifu wa binadamu kama mifano michache aliyotoa Askofu.

Swali la kujiuliza "je, mifumo ya utendaji inaweza kuondoa rushwa ndani ya mioyo ya binadamu?"
 
Ilikuwaje Eva akamsaliti Adam kwenye bustani ya Eden na binadamu tukapewa adhabu ya mauti. "Mwanzo 3:13 Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya, nikala."

Vipi na Yuda Iskariote kumsaliti Yesu. "Luka 22:3 Shetani akamwingia Yuda, aitwaye Iskariote, naye ni mmoja wa wale Thenashara."

Matukio hayo ya kwenye Biblia yanadhihirisha kuwa Rushwa imekuwepo na itakuwepo milele kwa sababu mbalimbali za udhaifu wa binadamu kama mifano michache aliyotoa Askofu.

Swali la kujiuliza "je, mifumo ya utendaji inaweza kuondoa rushwa ndani ya mioyo ya binadamu?"
Itaondoa kwa mtindo wa uwajibikaji na kuwajibishwa.
 
"Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
mkuu Pascal Mayalla naomba kwa heshima naomba hii point ianzishie uzi ktk zile nyuzi zako za maslahi mapana ya taifa
Asante, nitaifanyia mchakato.
P
 
"Tupambane na rushwa ya madaraka. Kwa hili msafi hajazaliwa, anahitajika malaika kumkatalia anayemlisha. Madaraka huja kwa uteuzi na kuchaguliwa. Wakati mwingine tatizo si la anayeteua. Wateuliwa tuna kansa ya kujipendekeza na kujiongeza kuwadanganya waliotuteua"Dk Benson Bagonza
mkuu Pascal Mayalla naomba kwa heshima naomba hii point ianzishie uzi ktk zile nyuzi zako za maslahi mapana ya taifa
Asante, nitaifanyia mchakato.
P
 
Bagonza tunajua ni kaada wa Chadema


Km Kweli anakipenda chama chake asimuogope Mbowe amwambie arudishe bilion 8
Haya sasa mzee wa kuongea ushuzi katika ubora wako nafikir message sent km cyo delivery
Kawaite tena wenzako USSR,Patriot na mje na kashfa yenu ya ukabila kaongea Bagonza sa hvi mara kada wa cdm,Toa tena na sifa nyngine ya baba Askofu...
 
Haya
Haya Mambo inabidi wafadhili wetu waambiwe pia maana CCM Ni kundi la hujuma na dhuluma kwa wanyonge chadema wamepewa hati Safi leo hii hao tako huru wanatumika kisiasa kwasababu uchaguzi umekaribia ujinga kabisa.
Walipenda nzi wa kijani waone chadema wanapata hati chafu. Hawo si mabw.egeeee.
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom