Askofu Bagonza, barua ya kumkaribisha Rais Magufuli Mkoani Kagera na tahakiki ya mjadala tunduizi

Siku moja tumekaa kijiweni watu watano. Tunaongea hili na lile. Mmoja wetu akasema: Mnajua mimi sikusoma lakini mambo yangu supa. Nilishangaa sana. Supa anaongelea chumba kimoja na bodaboda boxer. Aliuza shokora alilopewa na marehemu babu yake.
Mexicana ana elimu ya mavyuma. Hakusoma. Elimu haijamponza. Yupo yupo kama hayupo. Mji wake supa. Mipango miji ni watoto wa chekechea!
Siwezi endelea. Naishia hapa. Kichefuchefu. Huyu naye great thinker!

Kuna tofauti kubwa kati ya Yesu aliyezaliwa kijiweni na askofu mwenye kanisa lililoezekwa kwa mabati yanayoshilikiwa kwa kuta za mabati huku akikusanya sadaka na kujenga orofa nyumbani kwake kwa ajili ya mke, watoto na ukoo wake.

Yesu wa kijiweni ni bora kuliko askofu tapeli anayeishi orofani.

1610698631019.png

Homeless Jesus was born in KICHEFUCHEFU LABOR WARD at Bethlehem
 
Alichofanya mleta bandiko ndivyo CRITICAL DISCOURSE ANALYSIS inafanyika.
Unashauriwa kuanza kuizoea.
Kama hutaki kuona CRITICAL DISCOURSE ANALYSIS usisome bandiko hili.
Mhadhiri mkuda! Mara useme bandiko linasomeka hata kwa darasa la saba mara nione critical discourse analysis. Lipi ni lipi? Superiority complex at play!
 
Hivi kila mkoa kuwa na chuo ni sera ya taifa ama?! Naomba kueleweshwa.
Sio sera ya Taifa.

Lakini, pointi ya mwandika waraka ni kuwa mchujo wa p/schoool unajaza s/school, mchuzo wa s/school unajaza college/vyuo.

Kwa kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka kila shule ya Kata, it is logical kufikiria juu ya vyuo vya mikoa na Taifa.

However, that needs to be argued carefully, kwani sio lazima wanafunzi wa mkoa X wasomee chuo kilichoko mkoa X.
 
Mhadhiri mkuda! Mara useme bandiko linasomeka hata kwa darasa la saba mara nione critical discourse analysis. Lipi ni lipi? Superiority complex at play!
Critical discourse analysis ndivyo ilivyo. Izoee. Huwa tunafanya matatu makubwa:

- kwanza ni kubainisha hoja kwa kuangalia sehemu zake nane: claim, ground, warrant, backing, objection, rebuttals, qualifiers and concessions.

- pili ni kuhakiki hoja kwa kuangalia muundo na maudhui yake kama yanakidhi vigezo vya ukweli uliomo katika jamii.

- tatu, ni kuchunguza kama ukweli uliomo katika jamii ni ukweli wa kudumu au ukweli wa mpito wenye kutengenezwa na kikundi cha watu kwa ajili ya maslahi binafsi.
 
Mhadhiri mkuda! Mara useme bandiko linasomeka hata kwa darasa la saba mara nione critical discourse analysis. Lipi ni lipi? Superiority complex at play!

Kipi bora:

Superiority complex?

Inferiority complex?

Au unyenyekevu complex?
 
Mhadhiri mkuda! Mara useme bandiko linasomeka hata kwa darasa la saba mara nione critical discourse analysis. Lipi ni lipi? Superiority complex at play!

Kipi bora: mhadhiri mkuda au askofu waruwaru?
 
Kipi bora:

Superiority complex?

Inferiority complex?

Au unyenyekevu complex?
Ms Critical Discourse Analysis, hapo hakuna kilicho bora. Nimekuelewa kuwa unadhani superiority complex ni bora! The complex you're practicing. Hata nayo haifai hata kidogo. Kwa kuwa humaanisha arrogance iliyopitiliza.

Wakati inferiority complex ni unyenyekevu wa kuelekea kwenye ujinga! Hakuna complex nzuri. Kila kitu kiwe kwa kiasi. Hata upendo na uzuri wake wote nao pia uwe kwa kiasi. TOO much of ANYthing(complex) is HARMful!
 
Kipi bora: mhadhiri mkuda au askofu waruwaru?
Najua chaguo lako hapo. Na hivyo ndivyo ulivyo,unfortunately! Kama kuna jambo lolote baya kwako academically, chanzo chake ni ujivuni pachae ukuda! Muhongo complex. Na hili ndilo sababu ya bandiko lako. Askofu waruwaru? Hivyo ulterior motive ya bandiko lako ni yote mawili disinformation na malinformation.

Wataka nini au walenga nini ni usiku wa giza kwangu. Bado nasoma mabandiko yako with reservations kwa sababu sikufahamu. Kukufahamu ni muhimu kuongeza uelewa maridhawa wa mabandiko yako! Moral Rearmament wanasema: you can't live crooked and think straight nor think crooked and live straight. Nakubaliana!
 
View attachment 1681268

A. UTANGULIZI

Rais wa Tanzania, John Magufuli alikuwa Mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi wilayani Karagwe na baadaye Wilayani Bukoba tangu tarehe 18 Januari 2020. Inaonekana kuwa, siku hiyo, Askofu Dr. Benson Kalikawe Lwakalinda Bagonza, aliandika barua tepe kwa ajili ya kumkaribisha Rais Magufuli Mkoani Kagera na kuisambaza katika mitandao ya kijamii.

Nimeisoma barua husika na kuiweka mwishoni mwa andiko hili, li wasomaji wanaotaka kujisomea wenyewe waweze kufanya hivyo. Kwa maoni yangu, hoja ya sasa ya Dr. Bagonza, ambayo nakusudia kuiunga mkono kwa kuongezea ushahidi ninaoufahamu, inakusudia kutetea pendekezo lifuatalo:

Kwamba, kuna haja ya kuwawezesha watu wa Kagera kuendelea kuvaa kofia yao yenye nembo ya “Nshomile” kwa kufanya jambo mojawapo kati ya mawili: (1) Ama, kwa serikali kurejea maamuzi yake ili kuwaruhusu watu wa Kagera kufufua vyuo vyao haraka na kuviendeleza; (2) Au, kwa serikali yenyewe kubeba jukumu la kuanzisha chuo kikuu cha umma mkoani Kagera, ambacho chaweza kuwa tawi la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini kwa sasa au chuo kikuu kipya.

Ametaja sababu tatu kulitetea. Pia amebashiri pingamizi dhidi ya hoja yake na kulijibu.

Hii ni hoja nzuri na nzito, endapo itaboreshwa kama nitakavyopendekeza baada ya kuchambua kwa kina na kuhakiki hoja nzima.

Uhakiki rasmi unafuata hapa chini kwa kutumia mbinu za kuchambua na kuhakiki mijadala iliyosheheni hoja chokonozi (critical discourse analysis), yaani uchambuzi wa mijadala iliyobeba hoja chokonozi, kwa maneno mengine.


View attachment 1681294
Jengo la Utawala, Chuo cha KARUCO, Karagwe

B. UCHAMBUZI WA HOJA YA BAGONZA

Dhamira kuu ya mwandishi, Dk. Bagonza, ilikuwa ni kusanifu na kutetea hoja ambayo, kianatomia, inazo sehemu kuu sita zifuatazo:

Kwenye pendekezo kuu (claim) inadaiwa kwamba, kuna haja ya kuwawezesha watu wa Kagera kuendelea kuvaa kofia yao yenye nembo ya “Nshomile” kwa kufanya jambo mojawapo kati ya mawili: (1) Ama, kwa serikali kurejea maamuzi yake ili kuwaruhusu watu wa Kagera kufufua vyuo vyao haraka na kuviendeleza; (2) Au, kwa serikali yenyewe kubeba jukumu la kuanzisha chuo kikuu cha umma mkoani Kagera, ambacho chaweza kuwa tawi la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini kwa sasa au chuo kikuu kipya.

Kwenye sababu ya kwanza (ground) inadaiwa kwamba, kwa sasa watu wa Kagera wanajiona wanyonge kwa kuwa hawana chuo kikuu hata kimoja, baada ya vyuo vikuu kadhaa vilivyoanzishwa mkoani humo “kufwariki” kwa sababu ya “tetemeko la ardhi” lililotokana na mawimbi ya maamuzi ya serikali ya awamu ya tano, chini ya Rais Magufuli;

Kwenye sababu ya pili (warrant) inadaiwa kwamba, kwa mujibu wa historia, umaarufu wa watu wa Kagera unatokana na uwepo wa taasisi za kielimu zilizowafanya wavae kofia ya “Nshomile,” yaani kofia ya usomi;

Kwenye sababu ya tatu (backing) inadaiwa kwamba ukosefu wa elimu ya chuo kikuu inayopatikana kwa urahisi na katika maeneo ya karibu na nyumbani kunasababisha watu kujiona “wanyonge” kielimu mbele ya majirani zao wanaozidi kupaa kwa sababu ya kupata unafuu kama huo.

Kwenye pingamizi tarajiwa (anticipated objection), mwandishi alibashiri uwezekano wa mtu kupinga pendekezo lake la serikali kuvifungua vyuo vikuu vya Kagera, kwa kutumia sababu kwamba, vyuo hivi vilifungwa kwa sababu ya “mdomo” mrefu wa wamiliki wa vyuo hivi dhidi ya serikali. Mwandishi amemtolea mfano “mdomo” wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe” ambaye amekuwa mkosoaji endelevu wa maamuzi kadhaa ya serikali.

Kwenye ubutuaji wa pingamizi tarajiwa (rebuttal), mwandishi alitumia maelezo kwamba, pingamizi hili nidhaifu kwani, mbali na “mdomo” wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe” anayemiliki chuo kikuu cha KARUCO kuna vyuo vingine vitatu vimefungwa wakati wamiliki wake hawana “mdomo” kama wa “Askofu [Bagonza] wa Karagwe.”


View attachment 1681299
Jengo la utawala, CARUMCO, Muleba

C. UHAKIKI YA HOJA YA BAGONZA
Utetezi wa sababu ya kwanza umefanywa na mwandishi kwa kuorodhesha vyuo vikuu vinne vilivyoanzishwa mkoani humo na baadaye “kufwariki,” yaani: (1) University of Bukoba iliyoanzishwa na Profesa Teddy Maliyamkono na wenzake; (2) Josiah Kibira University College (JOKUCO) KKKT iliyoanzishwa na KKKT; (3) Cardinal Rugambwa University (CARUMCO) iliyoanzishwa na TEC; na (4) Karagwe University College (KARUCO) iliyoanzishwa na Dayosisi ya Karagwe (KKKT).

Nimeridhika na utetezi huu. Hata hivyo, sababu hii ingeweza kuimarishwa zaidi kwa kusisitiza kwamba, kitendo cha kufunga chuo kikuu chochote ni hatua ya kulizuia Taifa kufikia idadi mwafaka ya watu wenye kiwango cha elimu ya chuo kikuu (university education attainment level) inayoliwezesha Taifa kushindana kwa ufanisi katika ulimwengu wa soko la pamoja linaloambatana na siasa za utandawazi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu za UNESCO, watu wenye elimu ambayo ni angalau kidato cha nne hapa Tanzania ni chini ya 10%; Kenya ni juu ya 25%; na Uganda ni juu ya 15%. Kwa hiyo, kuna haja ya kupanua udahili katika ngazi ya vyuo vikuu ili tuweze kushindana na majirani zetu.

Utetezi wa sababu ya pili umefanywa na mwandishi kwa kuzitaja shule kongwe za mkoa wa Kagera kwa kutumia neno la “BUIKANO” linalomaanisha shule ya Bukoba Seco, Ihungo, Kahororo, Nyakato na Omumwani. Nimeridhika na utetezi huu.

Utetezi wa sababu ya tatu haukufanwa na mwandishi. Lakini, hii ni sababu ambayo iko wazo, kiasi kwamba, ni watu wachache wanaweza kuipinga. Kuna tofauti za kiuchumi na kisaikolojia kati ya anayepata elimu mkoani mwake na mtu anayepata elimu katika maeneo ya mbali na mkoa wa nyumbani.

Pingamizi tarajiwa na ubutuzi wake uliofanywa na mwandishi vinakubalika kimantiki. Hata hivyo, mwandishi alipaswa kwenda mbali na kubaini mapingamizi ya ziada na kuyabutua ili kulinda zaidi hoja yake.

Kwa mfano, nayafahamu mapingamizi mengine matatu ambayo mwandishi hakuyabaini wala kuyabutua. Mapingamizi hayo ni haya:

  • Kwamba, vyuo vinashindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU);
  • Kwamba, vyuo vinashindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu;
  • Na kwamba, vyuo vinakiuka misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Pingamizi linalohusu vyuo kushindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) linakigusa chuo kikuu cha KARUCO pekee. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii.

Nilipokuwa nakwenda Rwanda kumsalimia mjomba wangu, nilipita kwenye Chuo Kikuu cha KARUCO Karagwe ili kumtafutia nafasi mdogo wangu aliyekuwa anasoma Rugambwa.

Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Katabaro, aliniambia kwamba kwa sasa wameruhusiwa kutoa mafunzo kwa kutumia mitaala ya NACTE na wamenyimwa usajili wa chuo kikuu, japo miundombinu waliyonayo inawaruhusu kufanyakazi kama Chuo Kikuu.

Katika maelezo yake aliniambia kuwa, kigezo kigumu katika kutafuta usajili wa chuo kikuu ni sharti la kuwa na walimu walioajiriwa kwa mkataba wasiopungua idadi kadhaa. Walimu hao wanapaswa wasiwe wameajiriwa chuo kingine chochote. Na TCU inazo kanzidata ya kusajili walimu wa vyuo vikuu ili kuweza kufuatilia mikataba yao.

Dk. Katabaro aliniambia kuwa, ili kupata fedha za kuwaajiri walimu wa chuo kikuu watano inabidi ama chuo kiwe na vyanzo vyake vya mapato au kisajili wanafunzi na walipe karo. Kusudi upate wanafunzi walioidhinishwa na TCU inabidi kwanza usajiliwe na TCU kama Chuo Kikuuu! Kwa hiyo, njia hii haiwezekani. Na mpaka siku ile naongea na Dk. Katabaro, chuo cha KARUCO kilikuwa kimeshindwa kupitia njia mbadala ya kupata fedha za kuajili walimu ambao ni sharti muhimu kwa ajili ya usajili.

Kuhusu pingamizi hili, nilimtarajia Dr. Gagonza aseme jambo akieleza ni kwa vipi amepambana na changamoto husika, na kuhakikisha kwamba, mkwamo wa usajili hauanzii kwenye upande wake yeye kama mmiliki wa chuo cha KARUCO. Ni kwa njia hiyo, angekuwa amefungua mlango wa kujadili ni kwa vipi mkwamo wa usajili wa KARUCO unaanzia kwenye upande wa serikali.

Ni baada ya hapo, Profesa Ndalichako angelazimika kutoa maelezo juu ya mkwamo huo na kushauriwa ipasavyo na wanazuoni. Bila Dr. Bagonza kujipambanua katika jambo hili, pendekezo lake kwamba chuo cha KARUCO kinapaswa kusajiliwa kama Chuo Kikuu linabaki likining’inia hewani.

Pingamizi linalohusu vyuo kushindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu linavigusa vyuo vikuu baki vitatu, yaani, University of Bukoba, JOKUCO, na CARUMCO. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii pia.

Hata hivyo, siku nilipoongea na Dr. Katabaro wa chuo cha KARUCO, nilifahamishwa kwamba, hata vyuo hivi jirani yake vinayo matatizo na serikali kwa sababu mbili.

Sababu ya kwanza ni kwamba, kuna sera ya serikali ya kuitaka TCU kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu katika namna ambayo inatoa kipaumbele kwa vyuo vya serikali. Kwa mujibu wa sera hii, kama wanafunzi wenye sifa wakigawiwa kwenye vyuo vya serikali na kuisha, basi vyuo binafsi vinabaki mikono mitupu.

Na sababu ya pili niliyoambiwa na Dr. Katabaro ni kwamba, kuna sera ya serikali ya kutoa mikopo ya elimu ya juu ambayo inatoa kipaumbele kwa masomo maalum, kama vile masomo ya sayansi. Kwa sababu hii, vyuo binafsi vinavyotoa elimu kwa kufundisha kozi ambazo hazifadhiliwi na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu vinakufa kwa sababu ya kukosa wanafunzi wanaoweza kujilipia ada na mahitaji mengine yan kielimu.

Na pingamizi linalohusu vyuo kukiuka misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) linavigusa vyuo vikuu vyote vilivyoko sekta binafsi, kama vile University of Bukoba, JOKUCO, CARUMCO, SAUT, TUMAINI, na kadhalika. Katika barua yake, Dr. Bagonza hakusema lolote kuhusu tuhuma hii vile vile.

Nililibaini pingamizi hili mwenyewe wakati namsomesha mdogo wangu mmoja chuo cha TUMAINI. Wakati ule wanafunzi wa TUMAINI walilalamika sana juu ya ukubwa wa karo. Askofu Dr. Malasusa alipokuja kuongea nao aliwambia kauli fupi sana: “asiyetaka kulipa karo hiyo na kusoma hapa aondoke.”

Na katika mazingira haya, serikali ilianza kuvituhumu vyuo vikuu binafsi kadhaa kutumia fursa ya uwepo wa fedha za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kufanya biashara kwa kutoza ada kubwa. Jambo hili, kwa maoni ya serikali, linapingana na msingi wa kuanzishwa kwa HESLB.

Dr. Bagonza yuko Kanisa moja na Dr. Malasusa. Hivyo, huenda anayafahamu mamalalamiko haya kupitia kwa Askofu mwenzake. Hivyo, angeweza, na alipaswa, kulinda pendekezo lake la kuitaka serikali “kufungua” vyuo vikuu vya Kagera, kwa kusema jambo dhidi ya tuhuma hizi.


View attachment 1681303
Jengo la utawala, Chuo cha JOKUCO, Bukoba

D. MATUMIZI YA LUGHA NA TASWIRA
Mdadisi wa mambo, kama vile Askofu Dk. Bagonza, anapoandika “mjadala tunduizi” (critical discourse) ulio katika muundo wa shairi, dayalogia, riwaya, makala au barua hutumia lugha ya picha aliyoichagua yeye ili kujenga taswira maalum inayofafanua na kuweka mkazo juu ya sababu, athari na utatuzi wa matatizo ya jumuiya kama vile uonevu, ubaguzi, ukabila, udini, ukanda, upotoshaji wa ukweli na unyonyaji kama yanavyojitokeza kati ya matabaka mbalimbali ya kijamii kwenye sekta za maisha kama vile afya, elimu, ofisi za utawala wa kisiasa, uchumi na media.

Kwa hiyo, wanazuoni wanapofanya “tahakiki ya mjadala tunduizi” (critical discourse analysis) wanatakiwa kubainisha, kuhakiki, kufafanua kuthibitisha au kukanusha uwepo wa sababu, athari na utatuzi wa matatizo ya jumuiya yaliyoibuliwa na mtunzi wa mjadala.

Kwa kuangalia lugha inayotumiwa na mtunzi, tunaweza kubaini aina kuu tano za taswira zinazoweza kutumikwa na mtunzi kusanifu mijadala ili kuitaka jamii kuingilia kati kumaliza tatizo.

Taswira hizo ni hizi: taswira inayoonyesha uwepo wa mgongano wa kitabaka (conflict frame); taswira inayoonyesha uwepo wa hisia kali (human interest frame); taswira inayoonyesha uwepo wa madhara hasi/chanya ya kiuchumi na kijamii (socio-economic consequences frame); taswira inayoonyesha uwepo wa ukiukwaji wa kanuni za maadili ya jamii (morality frame); na taswira inayoonyesha uwepo wa uwajibikaji au ukosefu wa uwajibikaji kwa wahusika (attribution of responsibility frame) (Semetko and Valkenburg 2002).

Kwa kuzingatia haya, “tahakiki ya mjadala tunduizi” uliomo katika “barua ya wazi kwa Rais,” kama ilivyoandikwa na Askofu Dk. Benson Kalikawe Bagonza na kusambazwa katika mitandao ya kijamii tangu asubuhi ya tarehe 18 Januari 2020, inaonyesha yafuatayo:

Mwandishi ametumia mbinu tatu kusanifu hoja yake. Kwanza, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa mgongano wa kitabaka (conflict frame) kati ya serikali na “Nshomile.” Ametoa ushahidi wa vyuo vilivyofungwa na serikali kinyume cha matakwa ya wamiliki.

Pili, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa hisia kali (human interest frame) za kina “Nshomile” kupoteza kofia yao ya usomi kwa sababu ya kukosa udahili kwenye vyuo vikuu vya karibu na nyumbani kwao. Uamuzi wake wa kutumia neon “kufwariki” kama ambavyo “Nshomile” hutamka neno “kufariki” ni ushahidi muhimu hapa.

Na tatu, kuna taswira inayoonyesha uwepo wa madhara hasi ya kiuchumi na kijamii (socio-economic consequences frame) kwa sababu kuikosa elimu ya chuo kikuu ni sawa na kugeuka “mnyonge” kwa sababu ya kuukosa ufunguo wa maisha bora.


View attachment 1681308
Makao Makuu, NACTE, Dar es Salaam

E. HITIMISHO, MUHTASARI NA MAPENDEKEZO
Barua ya Dr. Bagonza imeibua hoja nzuri yenye umuhimu na uharaka. Lakini, isiishie kuandikwa na kusambazwa mitandaoni. Nashauri matatu.

  • Mosi, Dr. Bagonza ajielekeze kwenye kutafiti na kujibu mapingamizi yote yanayoweza kudhoofisha mapendekezo yake. Yaani, tuhuma kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi vigezo vya kusajiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU); kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi vigezo vya kudahili wanafunzi wa vyuo vikuu; na kwamba baadhi ya vyuo hushindwa kukidhi matakwa ya misingi ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
  • Pili, Dr. Bagonza apeleke majibu ya utafiti wake kwenye mamlaka husika za kiserikali, hasa, kwa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako.
  • Na tatu, Dr. Bagonza akae na mamlaka husika za kiserikali wayajenge kwa hoja kuhusu umuhimu na uharaka wa kufufua vyuo vya Kagera, na sio kuhusu kuanzisha chuo kipya cha umma. Hakuna haja ya kuanzia kwenye zero wakati tayari kuna kianzio kikubwa kuliko zero.
Lakini, yafaa Dr. Bagonza akakumbuka kuwa, Chuo Kikuu cha KARUCO kinao upekee dhidi ya vyuo vitatu baki alivyovitaja.

Kwanza KARUCO kinapanga kufundisha mitaala ya sayansi ya kilimo. Kwa hiyo wanafunzi wake wanaweza kupata mikopo baada ya KARUCO kusajiliwa kama Chuo Kikuu.

Kujenga hoja serikalini kwamba kozi zilizo katika mitaala hiyo zinapaswa kuingizwa katika oridha ya kozi zinazofadhiliwa na HESLB ni hoja inayowezekana kutetewa hadi kukubalika. Dr. Bagonza ni bingwa wa advocacy and lobying.

Pili, sharti la kuajiri wahadhiri linajadilika kwa sababu ya uwezekano wa wanafunzi wake kupata ufadhili kutoka HESLB.

Kwa mfano, kuomba serikali iweke sera ya usajili wa muda itakayoiruhusu KARUCO kupata uhalali wa kudajili wanafunzi kupitia TCU sio hoja ngumu kujengwa.

Kwa hiyo, kuhusu KARUCO, natoa wito kwa Waziri wa Elimu, Profesa Ndalichako, kuwa na sikio sikivu. Kwa vile, Rais Magufuli pia ni mtu kutoka ukoo wa “Abazilankende” wa huko Karagwe kwa kina Bagonza, natarajia atatia neno hapo.

Kila la heri kwa Askofu Dr. Benson Kalikawe Lwalinda Bagonza, askofu wa Karagwe mwenye “mdomo.”

Nimalizie tahakiki yangu kwa kutoa angalizo. Dr. Bagonza anapaswa kupunguza “mdomo” kwa kujitenga na vilema vya habari vinne (“four information disorders”) ambavyo mara nyingi vimekuwa vikiambatana na maandiko yake kadhaa. Vilema hivyo ni:

  • Kusambaza taarifa potofu kwa kujua na kwa nia ovu ya kutafuta faida ya kiuchumi, kisiasa au kijamii (disinformation);
  • Kusambaza taarifa potofu bila nia ovu na bila kujua kwa imani kwamba usambazaji huo utamnufaisha mpokeaji (misinformation); na
  • Kusambaza taarifa za watu binafsi lakini ambazo ni za kweli kwa watu wasiohusika na kwa nia ovu ya kuwachafua watu wengine wasiokubaliana naye (malinformation).

    [*]Kuwapotosha watu kwa kusambaza taarifa zenye ukweli nusu nusu kwa makusudi ili kutafuta maslahi binafsi (deception by omission).

    (Wardle and Derakshan 2018:5)
View attachment 1681317
Makao Makuu, Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, Mwenge, Dar es Salaam

F. KIAMBATANISHO CHA BARUA ILIYOANDIKWA NA ASKOFU BAGONZA

Mheshimiwa Rais JPM,
Karibu Sana Bukoba.

Bukoba ni makao makuu ya Mkoa wa Kagera. Zamani uliitwa [Mkoa wa] Ziwa Magharibi. Huu ni mkoa wenye historia ya mambo mengi. Kitaifa [Mkoa wa Kagera] ni nyumbani kwa [watu wanajitambua na kujitambulisha kama wasomi kwa kutumia neno maarufu la] "Nshomile". Hii ndiyo sababu ya makaribisho yangu [kwako Mheshimiwa Rais JPM].

Shule ya Ihungo inayopokelewa leo [na Rais Magufuli kutoka kwa mkandarasi] inapendeza. Lakini pia shule hiyo imebeba historia tukufu ya Mkoa huu [wa Kagera]. Wasomi wengi wamepita hapa. Ikiwa ni sehemu ya BUIKANO (Bukoba Seco, Ihungo, Kahororo, Nyakato na Omumwani), shule [hii] … pamoja na ile ya wasichana ya Rugambwa [vilikuwa vitovu vya] kuandaa wasomi wa Taifa hili kabla na baada ya Uhuru.

Mpendwa Rais, shule za sekondari tunazo za kutosha [mkoani Kagera] lakini hatuna chuo kikuu. [Unaweza kudhani kwamba, vyuo vikuu vya mkoa wa Kagera vilisambaratishwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea katika miaka ya hivi karibuni].

Mkoa huu una idadi kubwa ya maprofesa lakini hauna Chuo Kikuu hata kimoja [japo kuna jitihada kubwa ambazo zinafanywa ili kujenga vyuo vikuu mkoani humu]. [Kwa mfano,] akina Profesa Teddy Maliyamkono na wenzake walianzisha University of Bukoba [lakini] "ikafwariki baadaye".

KKKT ikaanzisha Josiah Kibira University College (JOKUCO) ikafungwa [na serikali] baadaye. TEC ikaanzisha Cardinal Rugambwa University (CARUMCO) ikafungwa [na serikali] na kuacha maumivu. Dayosisi ya Karagwe (KKKT) ikajenga Karagwe University College (KARUCO) [lakini] haijasajiliwa mpaka leo.

[Kuna] wazushi wanadai [kwamba KARUCO] haijasajiliwa kwa sababu Askofu [Bagonza ambaye ni mwanzilishi wa KARUCO] ana mdomo [mrefu]. Hawa ni waongo. Kwani wale Maaskofu waliofungiwa vyuo kule Bukoba nao wana mdomo [mrefu] kama Askofu [Bagonza] wa Karagwe? [Jawabu ni hapana. Kwa hiyo,] wazushi hawa watafute sababu nyingine.

[Basi, nimalizie kwa kusema kuwa,] hata kama vyuo [vya Kagera] vilivyofungwa vinaweza kufunguliwa baadaye [kama serikali itaona yafaa vifunguliwe haraka kama mimi ninavyopendekeza], bado tunahitaji chuo kikuu cha umma [mkoani Kagera kwa sasa]. Chaweza kuwa tawi (constituent college) la vyuo vikuu vya umma vilivyopo nchini [kama vile] UDSM, SUA, MZUMBE, MUHAS, nk.

Sababu [zinazokwepeka] zaweza kuwa […] zipo lakini iko [angalau sababu] moja isiyokwepeka. Mkoa huu [wa Kagera] ni [ukanda] wa "Nshomile". Bila chuo kikuu [Nshomile] tunakuwa wanyonge [kielimu wakati majirani zetu ndani na nje ya Tanzania wanazidi kupaa].

[Kuhusu hoja hii] naweza kupingwa [na] hata wana Kagera wenyewe. [Lakini haya] ni mawazo yangu nao wana [mawazo] yao. [Mawazo] ya kwangu yakikubalika, [tukalikumbuke] Tetemeko la Ardhi [lililotokea Kagera hivi karibuni] kupitia [jina la] chuo hiki [ninachokipendekeza].

[Napendekeza kwamba, chuo hiki] kinaweza kuitwa "Tetemeko University of Bukoba" na kiwe na Idara ya Jiolojia (Geology) ili mtani wangu Prof. Muhongo akimaliza ubunge aje kufundisha pale na kutuonyesha Tetemeko jingine linakuja lini.

NYEGERA WAITU OMUKUNILWA,
[KARIBU NDUGU MHESHIMIWA]
KALIKAWE LWAKALINDA BAGONZA.

View attachment 1681378

Baadhi ya Kozi zinazofundishwa kwa sasa katika chuo cha KARUCO, Karagwe
Pole Askofu. Kanisa ni wito. Karibu uraiani.toa kanzu shika bakora
 
Najua chaguo lako hapo. Na hivyo ndivyo ulivyo,unfortunately! Kama kuna jambo lolote baya kwako academically, chanzo chake ni ujivuni pachae ukuda! Muhongo complex. Na hili ndilo sababu ya bandiko lako. Askofu waruwaru? Hivyo ulterior motive ya bandiko lako ni yote mawili disinformation na malinformation. Wataka nini au walenga nini ni usiku wa giza kwangu. Bado nasoma mabandiko yako with reservations kwa sababu sikufahamu. Kukufahamu ni muhimu kuongeza uelewa maridhawa wa mabandiko yako! Moral Rearmament wanasema: you can't live crooked and think straight nor think crooked and live straight. Nakubaliana!

Sasa, hiyo ni theomania kama sio kupiga ramli.

Unajuaje chaguo langu kabla sijakwambia?.

Kwani wewe ni Mungu anayejua kila kitu?

Naina, unadondisha maneno kama maembe yadondokavyo toka mtini. Live croooked, think straight, ujivuni pachae ukuda, etc Jesus lived a crooked life, yet thought straight to convince you become his follower!

Jielekeze katika hoja, achana na mleta hoja. Lakini nasisitiza: ni vigumu kwa Dr. Bagonza kupata audience ya serikali kama hajajitenga na haya matatu: disinformation, misinformation, malinformation about the government. Anajua vizuri makosa yake, lini yamefanyika, kwa vipi, na kwa sababu gani.

Nimeifanyia kazi barua yake kwa umakini Kwa vile naona inapigania maslahi ya umma mpana.

Anaweza kupata fursa ya ushirikiano na serikali kwa kiwango hicho, lakini sio kabla ya kujirekebisha.
 
Ms Critical Discourse Analysis, hapo hakuna kilicho bora. Nimekuelewa kuwa unadhani superiority complex ni bora! The complex you're practicing. Hata nayo haifai hata kidogo. Kwa kuwa humaanisha arrogance iliyopitiliza. Wakati inferiority complex ni unyenyekevu wa kuelekea kwenye ujinga! Hakuna complex nzuri. Kila kitu kiwe kwa kiasi. Hata upendo na uzuri wake wote nao pia uwe kwa kiasi. TOO much of ANYthing(complex) is HARMful!

Sawa. Too much of anything complex is harmful.

Lakini, mbona huchukui hatua ya kubomoa mifumo inayopinga slogan yako hii?

Sheria za Kanisa lako zinasema kuwa deliberative power is exclusively reserved for the clergy (institutionalised superiority complex).

Sheria hizo zinaongeza kusema kuwa the power of the laity is exclusively restricted to consultative power (institutionalized inferiority complex)

These are two extremes contradicting your slogan.

Any plan of transforming this institutionised sin of social inequality contrary to divine will about the equality of human dignity as specified by rational, intellectual and volitional powers equally possessed by the clergy and laity alike?
 
Sasa, hiyo ni theomania kama sio kupiga ramli.

Unajuaje chaguo langu kabla sijakwambia?.

Kwani wewe ni Mungu anayejua kila kitu?

Naina, unadondisha maneno kama maembe yadondokavyo toka mtini. Live croooked, think straight, ujivuni pachae ukuda, etc Jesus lived a crooked life, yet thought straight to convince you become his follower!

Jielekeze katika hoja, achana na mleta hoja. Lakini nasisitiza: ni vigumu kwa Dr. Bagonza kupata audience ya serikali kama hajajitenga na haya matatu: disinformation, misinformation, malinformation about the government. Anajua vizuri makosa yake, lini yamefanyika, kwa vipi, na kwa sababu gani.

Nimeifanyia kazi barua yake kwa umakini Kwa vile naona inapigania maslahi ya umma mpana.

Anaweza kupata fursa ya ushirikiano na serikali kwa kiwango hicho, lakini sio kabla ya kujirekebisha.
Kuna wakati baba askofu alibaini kuna watu waliotaka kumdhuru. Akasema wamefika Karagwe. Nadhani wale wanaojulikana sana wasiojulikama. Nahisi ni wakati ule unaabiri kuelekea Rwanda. Ilikuwa lazima upite Karagwe na kuulizia nafasi kwa ajili ya nduguyo ya kujiunga na chuo kikuu.
Chuo kikuu ambacho hakijasajiliwa kwa sababu ya mwanzilishi kuwa na mdomo. Yote unayajua. Suluhisho ni kuunga mkono juhudi. Vinginevyo asahau kama Rugemalira kuhukumiwa na mahakama. Alishahukumiwa na DPP. Yeye si mahabusu bali mfungwa.
Wasiojulikana wakajulikana. Wamerudisha visu kwenye ala. Wamechomoa kalamu. Aliyemshindia wa jambia bado yu hai. Kumtetea atamtetea tu. Si lazima kuokota makopo. Hata kumuita mtumishi wa Mungu waruwaru, tapeli sio jambo dogo. Hili ni kujitoa mhanga.
Mwanzo nilifikiri watu hawachangii hili bandiko kwa sababu ya urefu wake. Hawana muda wa kulisoma. Mafuta ya kula yamepanda bei sana. Wanaikimbiza shilingi. Imeota mbawa. Sasa ni bayana hawachangii kwa kuwa hawataki kukaribiana na mlaaniwa. Nami sasa nanawa mikono. Kazi nimemaliza. Endelea!
 
Kuna wakati baba askofu alibaini kuna watu waliotaka kumdhuru. Akasema wamefika Karagwe. Nadhani wale wanaojulikana sana wasiojulikama. Nahisi ni wakati ule unaabiri kuelekea Rwanda. Ilikuwa lazima upite Karagwe na kuulizia nafasi kwa ajili ya nduguyo ya kujiunga na chuo kikuu.
Chuo kikuu ambacho hakijasajiliwa kwa sababu ya mwanzilishi kuwa na mdomo. Yote unayajua. Suluhisho ni kuunga mkono juhudi. Vinginevyo asahau kama Rugemalira kuhukumiwa na mahakama. Alishahukumiwa na DPP. Yeye si mahabusu bali mfungwa.
Wasiojulikana wakajulikana. Wamerudisha visu kwenye ala. Wamechomoa kalamu. Aliyemshindia wa jambia bado yu hai. Kumtetea atamtetea tu. Si lazima kuokota makopo. Hata kumuita mtumishi wa Mungu waruwaru, tapeli sio jambo dogo. Hili ni kujitoa mhanga.
Mwanzo nilifikiri watu hawachangii hili bandiko kwa sababu ya urefu wake. Hawana muda wa kulisoma. Mafuta ya kula yamepanda bei sana. Wanaikimbiza shilingi. Imeota mbawa. Sasa ni bayana hawachangii kwa kuwa hawataki kukaribiana na mlaaniwa. Nami sasa nanawa mikono. Kazi nimemaliza. Endelea!

Naona unamjadili mtu unayemwita askofu na kumtaja kama mtu wa mungu bila kubainisha ushahidi wa matamko hayo na badala ya kujadili hoja ya bandiko. That is a tangential response. It warrants no further comment. Kuhusu takwimu za wasomaji, wachangiaji na watazamaji ulizoulizia, hizi hapa:

1610832897183.png


1610832949455.png
 
Back
Top Bottom