Askofu Bagonza atoa somo la uraia, uvumilivu wa kusikiliza hoja kinzani ndiyo siasa yenyewe

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173
Mgongano wa mawazo ndiyo afya, nchi inapitia ktk tetemeko la kisiasa baada ya kifo cha Rais aliyekuwa anahudumu

Askofu Bagonza atoa mawazo yake kuhusu masuala mbalimbali ya siasa na sayansi ya siasa.

Spika au rais wote wana huru wa kutoa mawazo yao wakiwa katika nafsi iliyo nje ya taasisi ya Bunge au taasisi ya Urais.

CCM Kuua kambi ya upinzani yaani vyama vingi kupaza sauti au kushinda viti vya udiwani na ubunge ktk chaguzi, ndiyo kumeleta upinzani ndani ya chama kimoja. Mfano spika hivi karibuni alikuwa anatoa mawazo kama vile yeye ni 'kiongozi wa upinzani Bungeni '

Askofu Bagonza ashauri jinsi ya kuongoza mchakato mzima wa kupatikana spika mpya, anatamani mchakato huo uongozwe na mtu mwenye uzoefu mkubwa kusimamia zoezi hili.

Kuna mgawanyiko mkubwa ktk hali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi hivyo rais aseme kwa ujasiri kuponyesha vidonda vya kijamii mfano watu kuumizwa kisiasa na kiuchumi.

Mihimili mitatu iliyojificha katika mhimili mmoja na kuwa mateka pia kusababisha nyufa katika taifa na inahitaji ujasiri wa ziada kurekebisha hali hii askofu Bagonza anasisitiza.

Tunaweza kupata spika mzuri sana kuliko Ndugai lake spika huyu mpya akawa hana Bunge maana bungeni kumejaa wabunge waoga wa chama dola wasioweza kuhoji, kuishauri serikali wala kupitisha miswada na sheria sahihi.

Kiongozi bora hapimwi ktk kipindi shwari kisiasa bali hupimwa jinsi anavyoweza kuhimili na kuongoza nchi katika kipindi cha mtikisiko kama tulionao sasa ... na hakuna rais ktk awamu zote zilizopita ambae amepitia bila kukumbana na matikisiko ingawa wakati wa Magufuli ndiyo yalikuwa makubwa sana ...anakumbushia Askofu Benson Bangoza.

Source: PHD MEDIA TV
 
Bagonza anafiti kabisa uwenyekiti Chadema maana sio muoga hata kwenye maandamano anaweza shiriki yeye na watoto wake tu!
 
Kama Naibu Spika anaogopa kupingana mawazo na serikali hayo maendeleo ya taifa yatatokea wapi?

Kama serikali nayo inaogopa kujibu hoja za wanaoiuliza na kuishia kuwasuta hayo maendeleo ya taifa yatatoka wapi?

Ndio maana sasa kama taifa tunalazimishwa kuona kukopa ni sifa licha ya rasilimali zote tulizonazo.
 
JPM alisema mhimili mmoja umejichimbia katika mihimili mingine miwili, lakini kupitia katika suala la Ndugai na lile la kesi ya ugaidi ya Mbowe tunabaini ukweli ya kwamba mhimili mmoja umeimeza kabisa mihimili mingine.

Mchakato wa kumpata Spika wa Bunge na wabunge unategemea hisani ya chama chake na kukubalika kwake mbele ya macho ya Mwenyekiti Taifa aliyepo madarakani. Na hata pia mchakato wa kumpata Jaji Mkuu na majaji wengine hutegemea hisani ya Rais aliyepo madarakani.

Pasipokuwepo na katiba mpya yenye kumpunguzia Rais madaraka kama ambavyo ilivyokuwa kwa hivi sasa, tutaendelea kushuhudia kuwa kauli ya Rais ni ya mwisho na ni amri kwa taifa, haipaswi kuhojiwa, kukosolewa wala kupingwa hata kama ina kasoro na ukakasi.

Tunaweza kuijenga taasisi ya urais kuwa imara na yenye tija kama tutaondokana na hii dhana potofu kuwa Rais ni "infallible" na wala hawezi kujibika ama kuwajibishwa. "Separation of powers" miongoni mwa mihimili ni kitu pekee ambacho kinaweza kuliokoa taifa letu kutokana na mambo kuzidi kuendeshwa kiholela.
 
Hapa ndio kuna ugomvi
 
Tangu wapendwa wako Ndugai, polepole, makonda, Bashiru wapigwe na kitu kizito unekuwa kama umechanganyikiwa
Dawa Iliyobakia ni yeye kuunga juhudi za kipatikana katiba mpya TU, vinginevyo aliowaimbia pambio na anaoendelea kuwaimbia pambio hawako na hawata kuwa salama. Zaidi ndani ya katiba hii chakavu🤔.
 
Bagonza anafiti kabisa uwenyekiti Chadema maana sio muoga hata kwenye maandamano anaweza shiriki yeye na watoto wake tu!
Jifunze kupokea hoja kinzani Na wala msilazimishe watoa hoja kujiuzulu,kuwahonga hela na kuwaomba waunge juhudi uchwara,kuwapoteza,kubambika kesi,kuwatwanga risasi au kuwaua kabisa.Muelewe baba Askofu
 
Kiongozi bora hapimwi ktk kipindi shwari kisiasa bali hupimwa jinsi anavyoweza kuhimili na kuongoza nchi katika kipindi cha mtikisiko kama tulionao sasa ..

12 January 2022
Ikulu Chamwino
Dodoma Tanzania

Rais Samia Hassan akutana na aliyekuwa spika wa Bunge la Muungano Mh. Job Ndugai

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai. Taarifa iliyowekwa katika ukurasa wa Twitter wa Ikulu ya Tanzania (ikulu_Tanzania) leo Januari 12, 2022 imesema kuwa Mkuu huyo wa nchi amefanya mazungumzo na Ndugai Ikulu Chamwino jijini Dodoma.

Taarifa hiyo ambayo haikueleza kwa undani yaliyozungumzwa na wawili hao imesema “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) aliyefika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma”.

Imesema taarifa hiyo ambayo iliambatanishwa na picha ya Rais Samia akiwa amesimama pamoja na Ndugai
 
Dawa Iliyobakia ni yeye kuunga juhudi za kipatikana katiba mpya TU, vinginevyo aliowaimbia pambio na anaoendelea kuwaimbia pambio hawako na hawata kuwa salama. Zaidi ndani ya katiba hii chakavu🤔.
Hatakaa apone ugonjwa wake bila katiba mpya
 
Kama Naibu Spika anaogopa kupingana mawazo na serikali hayo maendeleo ya taifa yatatokea wapi?

Kama serikali nayo inaogopa kujibu hoja za wanaoiuliza na kuishia kuwasuta hayo maendeleo ya taifa yatatoka wapi?

Ndio maana sasa kama taifa tunalazimishwa kuona kukopa ni sifa licha ya rasilimali zote tulizonazo.
Maajabu sana nchi hii na ccm yake.
 
Jifunze kupokea hoja kinzani Na wala msilazimishe watoa hoja kujiuzulu,kuwahonga hela na kuwaomba waunge juhudi uchwara,kuwapoteza,kubambika kesi,kuwatwanga risasi au kuwaua kabisa.Muelewe baba Askofu
Baba askofu anakopy yale matamshi ya kujaribu sumu kwa kuiramba!
 
Back
Top Bottom