Askofu Bagonza anatafakari sakata la Ole Sabaya

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,254
2,000
TULIYAJUA, HATUKUYAJUA, HILI NI ZAIDI YA TATIZO.

Kesi iko mahakamani, sitaki kusema yaliyomo ya kesi hiyo. Najipa haki ya kusema jambo zima kwa ujumla wake.

Siku Rais Samia alipochukua ofisi nilipendekeza Mwongozo wa Kuongoza Kipindi cha Mpito wa awamu mbili, yaani kutoka ya 5 kwenda ya 6. Nimeupitia tena, sioni cha kubadili. Naweza kupuuzwa lakini madhara ya kunipuuza hayaepukiki.

Nilisema, Wateule wote wenye HULKA ya kukanyaga sheria na katiba kwa kisingizio cha uzalendo wapumzishwe. Nikongeza, hawa wateule ni "hatari kwa Rais kuliko walivyo hatari kwa nchi".

Unapokuwa na Mteule anayemiliki "jeshi" lake, "silaha zake", "benki yake" " dini yake isiyosajiliwa popote" nk. Na Mteule huyo ana uwezo wa kumkaribia Rais wetu, Makamu wake, Waziri Mkuu wetu, Spika wetu, Jaji Mkuu wetu, maabara zetu nk - huwezi kujua atafanya nini kuwadhuru ili afiche uhalifu wake.

Tuhuma zilizotajwa, ziwe zilitokea au hazikutokea, Taifa letu lina mgogoro mkubwa mikononi mwake. Kama yalitokea na hatukujua, ni tatizo. Kama hayakutokea lakini yanazushwa kumuonea Mteule, nalo ni tatizo. Kwa nini?

1. Mfumo wetu unaolilinda Taifa letu (system) ulifeli sana. Kama haukufeli bali uliona ukaandika taarifa kwa wakubwa na hawakuchukua hatua, bado ni tatizo la mfumo, si la wakubwa. Mfumo ujifunze kutumikia taifa na siyo kutumikia Viongozi na watawala. Baba wa Taifa alifikiri kwa makini kuuita "Mfumo wa Taifa", si Mfumo wa Rais au Viongozi.

2. Sabaya asingeweza kutenda haya au kufikiriwa kutenda haya bila msaada au kimya cha mfumo. Mnyororo wa kuwezesha uhalifu huu ni mrefu na kwa uchache unajumuisha Watendaji wa mfumo, Polisi, chama tawala, Media, TCRA, PCCB, RC na timu yake, wabunge wa maeneo, makanisa, misikiti, mfumo wa afya, na serikali za mitaa. Twaweza kumshughulikia Sabaya lakini tujue mnyororo huu una virus au vidonda vya hatari.

3. Haiwezekani kuwa Sabaya ni Mteule pekee aliyefanya haya nchi nzima. Wapo wengine, tena wengi. Nami nimewashuhudia kwa macho yangu. Nina mengi. Kumshughulikia Sabaya bila kukagua ripoti za mfumo ambazo hazikusomwa au zilisomwa zikapuuzwa , itakuwa ni kutibu dalili na kuacha ugonjwa.

4. Si madhambi yote ya wateule yanafaa kwenda mahakamani. Mengine tutumie kanuni ya Baba wa Taifa kuhusu Mke wa Kaizari. Wateule wote ama waishi ng'ambo ya tuhuma au waonekane kuishi ng'ambo ya tuhuma.

5. Ili kubaini madhara ya wateule kama Sabaya, kubaini kasoro za mfumo, kuponya Taifa, kuepusha yasitokee tena na kumtendea haki Mama Tanzania, nashauri yafuatayo:

a) Tuache wazi milango ya uchunguzi kwa wateule wengine wanaotajwatajwa na kutuhumiwa kutenda uhalifu dhidi ya Katiba na sheria za nchi.

b) Hata wasiotajwa lakini wangependa kuchunguzwa ili watamkwe kuwa safi, waruhusiwe kujitokeza na kuchunguzwa.

c) Wanaotajwa, wakitoa ushirikiano kwa chombo cha uchunguzi wasamehewe lakini wajiuzuru au kuvuliwa nyadhifa zao. Hata wakikutwa hawana hatia wajiuzuru kwa kuruhusu kutuhumiwa mambo mazito.

d) Watakaokutwa na hatia (si mahakamani bali mbele ya chombo cha uchunguzi) wasiruhusiwe kuwa katika utumishi wa umma au ofisi ya kuchaguliwa kwa kipindi maalum.

e) Viongozi wa kuchaguliwa, kuteuliwa, kuajiriwa na Viongozi wa imani waliojua au kushuhudia yaliyotendwa na wateule kama Sabaya lakini wakakaa kimya waone sababu ya kuwajibika kwa ama kujiuzuru, kuomba radhi, au kustaafu.

f) Waliotiwa hasara za mali au afya wafidiwe. Sehemu ya fidia itokane na mali za waliotenda makosa hayo.

g) Tuhitimishe mchakato huo kwa kuwa na siku ya kitaifa ya MWANZO MPYA. Siku hiyo wahanga washikane mikono na watesi wao.

NB: Maoni yangu yamejaa vionjo vya Imani yangu. Imani yangu si ya Taifa. Yasipuuzwe kwa udhaifu wa kuingiza Imani. Tuna tatizo kubwa na dawa yake si kulipuuza. Ukimwacha nyoka wakati unalima shamba, utamkuta wakati wa mavuno.
 

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
16,513
2,000
.
20210605_140638.jpg
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,077
2,000
Haiwezekani kuwa Sabaya ni Mteule pekee aliyefanya haya nchi nzima. Wapo wengine, tena wengi. Nami nimewashuhudia kwa macho yangu. Nina mengi. Kumshughulikia Sabaya bila kukagua ripoti za mfumo ambazo hazikusomwa au zilisomwa zikapuuzwa , itakuwa ni kutibu dalili na kuacha ugonjwa.
Makonda, Ali Hapy, Mnyeti, Yule wa Mwanza/Mbeya na mapipa mengine ya waovu
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,136
2,000
Napendekeza tume ya kijaji iwe na mjumbe wa imani toka kanisani huyu askofu atasaidia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom