Askofu Bagonza aamua kumtetea Prof Kabudi, asema yuko sahihi katoka jalalani

saidi kindole

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
310
792
Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge.

Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa.

Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

=======

Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
 
... hoja ya msingi ni kutolewa sijui kuokotwa "jalalani". Kama mtu wa level ya profesa kaokotwa jalalani, je, sisi maskini walalahoi mbumbumbu wajinga sijui tunaishi wapi! Ndio maana hoja inajengwa kwamba za Kabudi ni zaidi ya shukrani; huenda ana ajenda zake nyingine.
 
Anaandika Baba Askofu Dr.Benson Bagonza

KABUDI YUKO SAHIHI

Kauli ya Prof. Kabudi akikiri kutokea jalalani alipoteuliwa kuwa Waziri, imelaaniwa sana kutoka pande zote. Nina mawazo tofauti, bila kulaani wala kubariki. Nina sababu kadhaa:

1. Chini ya katiba ya sasa ambayo Prof. Kabudi aliikosoa sana kabla "hajaokoka", Rais ana mamlaka ya kumteua yeyote apendavyo bila kuhojiwa wala kuingiliwa na mamlaka yoyote. Anaweza hata kumteua asiye raia na kisha akampa uraia. Kwa msingi huo, Rais ana watu zaidi ya milioni 55 ambamo ana uhuru wa kuteua yeyote. Akikuona, unajiona ni wa bahati sana. Ukiamua kuyaona yote ya nyuma kama "kinyesi", watakaokushangaa ni wale ambao hawajawahi kukutana na jicho la habari njema toka Magogoni. Prof. Kabudi ameonwa katika wengi, mnaohoji mnaonekana mna lenu. Katiba ndiyo tatizo.

2. Maprofesa wastaafu katika nchi yetu, wana hali mbaya kiuchumi (wanisamehe kama nimekosea). Wengi wao wanafanya shughuli za kupata mkate uzeeni zisizohusiana na kazi zao. Prof. Kabudi sasa hanunui mafuta, umeme, vocha, wala nauli ya bombadier. Ana wasaidizi wa kubeba koti, kupika, walinzi, dobi, kinyozi, mpaka daktari binafsi. Ufa uliopo kati yake na maprofesa wastaafu wenzake ni mkubwa sana. Kwake yeye, bora uambiwe "pumbafu" ubaki ulipo kuliko kutambulishwa mkutano wa kijiji kuwa wewe ni profesa fulani wakati una madeni duka la kijiji.

3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa. Mnaokosoa mna hoja gani kumpinga MTEULIWA anayemshukuru ALIYEMTEUA?

4. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri ni watumishi wa umma. Tulizoea kuamini kuwa mawaziri wanawajibika kwa umma na utumishi wao ni msalaba siyo ufufuko. Hivi sasa, mawaziri ni watumishi wa "serikali" kwanza, na watumishi wa umma nafasi ya pili. Wakiukosea umma wanaweza kuvumiliwa. Wakiikosea "serikali", wanaondolewa mara moja. Kwa nini Prof Kabudi aandamwe kwa kuonyesha utii na shukrani yake kwa serikali? Wangapi wameukosea umma na bado wapo lakini waliokosea wakachelewa kutii maagizo ya serikali wameondolewa? Mi naona kosa la Prof Kabudi ni kusema wazi kile kilicho moyoni kuliko wanaofanya kimya kimya.

5. Wanyambo wana msemo kuwa "Mtoto mtiifu huwa anakunya kinyesi kikubwa" (kwa maana kwamba anakula chakula cha kutosha). Utii wa Prof. Kabudi unawafanya watu wengine waanze kuzusha kuwa oh! Prof ndiye "de facto" Waziri Mkuu, ndiye anaandaliwa kuwa "serikali", ndiye "mtoto mtiifu", nk. Maana yangu hapa ni kuwa utii unalipa hata pale unapoonekana ni kujitoa akili. Je kuna shida mtu kuamua kuwa mtii?

Nami nimeamua kujitoa akili ili kumtetea.
 
Ametumia falsafa kuwakilisha hoja
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu.Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.

Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki.

So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.

Hivi anajua pension ya profesa aliyestaafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara alionao askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachopokea professor mstaafu Kila mwezi kama pension?.

Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke.

Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
 
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu .Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki .So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.Hivi anajua pension ya profesa aliyekatafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara aliondoka askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachookea professor mstaafu Kila mwezi.Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke
.Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
Binti mbona unamtetea sana mpumbavu wa jalalani???
 
Mtumishi mdogo wa salary chini ya mln moja ana uwezo wa kutengeneza venture ya zaidi ya mil.20 ndani ya miaka 15 ya utumishi wake sembuse huyo professor aliyekaa kwenye ajira zaidi ya 40 yrs na mshahara mkubwa,fursa kibao ameshindwa vipi kumiliki hivyo vitu ulivyovitaja hapo baba askofu?

Kuna haja gani ya kusoma hadi elimu ya mwisho kama haikusaidii hadi kujipendekeza kujipendekeza?
Kwa kweli njaa mbaya sana
 
Kwa vile ushajitoa akili sikushangai kwa kufanya chochote hivyo NO COMMENTS
 
Mtumishi mdogo wa salary chini ya mln moja ana uwezo wa kutengeneza venture ya zaidi ya mil.20 ndani ya miaka 15 ya utumishi wake sembuse huyo professor aliyekaa kwenye ajira zaidi ya 40 yrs na mshahara mkubwa,fursa kibao ameshindwa vipi kumiliki hivyo vitu ulivyovitaja hapo baba askofu? Kuna haja gani ya kusoma hadi elimu ya mwisho kama haikusaidii hadi kujipendekeza kujipendekeza?
Kwa kweli njaa mbaya sana
Wala profresa hahitaji hata kuwa na business kuishi pension inatosha.Huyo askofu wako mwongo halafu huwa anajitia yeye jasiri haogopi kusema ukweli.Unataka nikuhakikishie kuwa huyo askofu ni mwoga kusema ukweli na ni muongo? Haya wewe askofu Bagonza askofu usiyeogopa kusema ukweli tutajie majina ya hao maprofesa wastaafu waliochoka kimaisha.Na wameichoka Kivipi?.Tutajie majina baba askofu jasiri usiyeogopa kusema ukweli.
 
Kama profesa mstaafu anasema ametolewa jalalani ina mwaana mwalimu mstaafu wa UPE anaishi mochuari!
Hata kama katiba inaruhusu kila mtu kutoa maoni ila ya huyo reprofeseri ni kinyaa na dharau kwa sisi walimu wastaafu wa UPE!!!
 
3. Prof. Kabudi alipigania sana mawaziri wasitokane na wabunge. Rasimu haikutekelezwa lakini Rais ametekeleza kilio chake. Prof Kabudi si mbunge wa kuchaguliwa. Ameteuliwa. Jimbo lake ni aliyemteuwa

Lugha gongana
 
Lugha iliyotumika sio ya kiaskofu.Kazi mojawapo ya askofu ni kulea watoto wanaoshinda majalalani kuwalea kwenye nyumba za kulelea watoto wenye mazingira magumu.Huwezi kebehi aliyetokea jalalani.

Sana sana utampa Pole kwa kuishi maisha magumu nk anyway ni askofu wa kilutheri wao huwa hawana tabia ya kulea watoto wa mitaani wala majalalani kama wa katoliki.

So he can say anything.Kuhusu maprofesa wKistaafu kwa huwa na maisha magumu ni uongo.

Hivi anajua pension ya profesa aliyestaafu kuwa analipwa pesa nyingi tu ambazo hata mshahara alionao askofu bagonza haufikishi hata robo ya anachopokea professor mstaafu Kila mwezi kama pension?.

Kama kaona kuna professor kachoka ni tu sababu ya life style yake.Kama anashinda kwenye kunywa gongo lazima akongoroke.

Askofu anadhani maprofesa waganga njaa kama yeye anayeacha madhabahu na kukimbilia siasa.
Mkuu unashangaza. Na ki-smart chako chote hukumuelewa Askofu? Na wapi uliambiwa maAskofu wa kilutheri hawajui kulea? Au ullmaanisha kulea kama tunavyosikia yametendeka kati ya maPadre na watoto waliokabidhiwa?
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom