Askofu amwambia Lissu asipeperushe bendera ya chama chake kwani inawaumiza sana CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askofu amwambia Lissu asipeperushe bendera ya chama chake kwani inawaumiza sana CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rugemeleza, Nov 14, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Askofu huyu katumwa na nani?
  [​IMG]
  Na Mwandishi wetu - Imechapwa 10 November 2010

  [​IMG][​IMG]ASKOFU wa Kanisa Katoliki anategemewa azungumze mambo ya maadili na imani. Anatarajiwa afundishe mafundisho ya kanisa, yasiyoegemea upande wowote wa kisiasa kwa kuwa yeye ana waumini wa vyama mbalimbali katika kanisa lake analoliongoza.
  Katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani uliomalizika hivi karibuni hali imekuwa tofauti.


  Uchaguzi umepita, walioshinda wanafurahia mitaani, walioanguka wanasikitika; yote hayo ni maamuzi ya wananchi na yanapaswa kuheshimiwa.

  Katikati ya shangwe, wananchi wa Jimbo la Singida Mashariki walitumiwa ujumbe kupitia mbunge wao, Tundu Lisu. Ujumbe huo ulitoka kwa mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya, unaomtaka mbunge huyo mteule aache kufurahia ushindi kwa nguvu, na kupeperusha bendera huku akipita na vipaza sauti.
  Sababu? Eti kwa kufanya hivyo anawaumiza wale walioshindwa. Huku ni kupotosha maana ya mashindano.
  Hakuna shida. Tatizo ni kwamba waliotuma ujumbe huo ni viongozi wa serikali, yaani mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya – Singida.

  Mbaya zaidi aliyetumwa kuwasilisha ujumbe huo ni kiongozi wa Kanisa Katoliki mkoani humo, yaani askofu. Tunashindwa kuelewa.

  Ilikuwaje mkuu wa mkoa, na mkuu wa wilaya wamtume askofu huyo kumwambia mbunge wetu maneno hayo? Hakukuwepo na watu wengine wa kutumwa katika ofisi ya viongozi hao wa serikali ila atumwe kiongozi huyo wa kiroho?


  Na kwanini kiongozi huyo wa dini alijishusha sana kiasi cha kutumwa kazi kama hii isiyo na tija kwa kanisa? Na alikubali kuifanya kwa maslahi ya nani? Kwa ajili ya nini?
  Askofu ananukuliwa akimwambia Lissu kwamba "kwa kuwa umepata ulichokuwa unatafuta usiwahamasishe wananchi waache kuchangishwa." Loo!


  Mojawapo ya sera zilizomwongezea umaarufu Lissu katika kampeni zake ni kuzuia michango yote haramu, ukiwemo wa sekondari. Hoja ya Lissu ni kwamba mchango huo ni haramu kwa kuwa haukupitishwa kisheria na bunge.


  Lisu amekuwa akihoji kuwa pesa nyingi zinazotengwa na serikali hazifiki kwa wananchi kujenga shule, hivyo anataka serikali iwajibike kujenga shule hizo kwa pesa za kodi badala ya kuwatoza wananchi michango ambayo imekuwa ikiwanufaisha wachache.


  Lissu amekuwa mkali pia kwa vizuizi vinavyowekwa barabarani kukusanya ushuru wa mazao, kwani upo kinyume. Sheria ya serikali za mitaa liyofuta ushuru wa mazao ilitolewa kupitia tangazo la serikali Na 231, la tarehe 3/5/2002, wakati huo Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi akiwa waziri mwenye dhamana.


  Sasa Bunge hadi sasa halijatunga sheria nyingine tofauti na hiyo, hivyo kuonekana kuwa serikali imewaibia Watanzania michango na au ushuru haramu kwa miaka minane.

  Hayo ndio madai ya mbunge huyu machachari. Lakini askofu huyu ameenda kumshauri aache kuzungumzia ajenda hizi. Inakuwaje askofu anapokuwa anapenda wananchi wake kutozwa ushuru isivyo halali? Askofu anatumia gari yake inayolipiwa mafuta kwa sadaka za wakristo toka Singida mjini hadi Dung'unyi kwa Tundu Lissu kueleza mawazo mepesi haya.

  Njia nzima Roho Mtakatifu hakumshukia askofu huyo amshauri tofauti? Wananchi wa Singida wamekuwa wakisikitishwa na baadhi ya dhuluma zinazoonekana kufanywa na viongozi hao waliomtuma.


  Wananchi wamedhulumiwa mashamba katika mradi wa umeme unaotarajiwa kuanza, wananchi wameendelea kunung'unikia kuuzwa kwa majengo ya Chama cha Ushirika mkoani (SIRECU), wananchi wameendelea kushuhudia mikataba tata ya kifisadi katika jengo la utamaduni lililopo mjini Singida.


  Wananchi wamekuwa wakitozwa ushuru usio halali mjini Singida, hutozwa fedha kwa ajili ya usafi wakati mji wa Singida ni mchafu. Hayo yote yanahitaji mtetezi.

  Askofu anapoamua kumwonya mtetezi wa haki ili kutumikia mafisadi hawa, analenga nini? Anafaidika vipi na uongozi unaolalamikiwa na wananchi? Yeye kama askofu aliumia vipi na kwa nini aliumia na ushindi wa Lissu, hadi aone walioshindwa wanahuzunika?


  Je, anakubalina na rushwa iliyotumika kuwanunulia wananchi vitenge, kanga, magodoro fulana na kofia alizokuwa anatoa yule aliyeshindwa? Anamhurumia aliyeshindwa kwa kuwa alitoa fedha nyingi kupita kiasi kuhonga wananchi? Anatufundisha nini sisi waumini wake kwa siku zijazo?


  Je, kuwahurumia watoa rushwa walioshindwa huku akiwawaonya walioshinda kihalali waache kushangilia ushindi wao ni msimamo wa kanisa au wake binafsi?

  Maaskofu wangapi walifanya kitu kama hicho kwenye majimbo yao? Askofu huyu atatumiwa na mkuu wa mkoa kwa mambo mangapi? Na atatumiwa vile kwa muda gani? Na alipotumwa hakugundua kuwa mkuu wa mkoa anao watu wengi wa kutuma kwa mambo mepesi kama hayo ili amshauri vinginevyo kuliko kujitolea kwenda?

  Ziara yake kwenda kuonana na Lissu ililipiwa kiasi gani toka kwa mkuu wa mkoa? Kwa nini hakupewa gari na ofisi ya mkuu wa mkoa akaamua kutumia gari yake inayolipiwa na waamini wa kanisa hilo? Ni kitendo cha aibu, ambacho kama bado kipo kwenye akili za waumini, basi ni cha kuvumilia.


  Lakini mkuu wa mkoa wa Singida na askofu huyu wamedhalilisha kanisa kwa kutumia gari ya askofu kufanyia siasa ambazo hazina lengo la kumkomboa maskini wa Kitanzania.

  Si vema askofu kuwabeba viongozi wa aina hii, ni aibu katika jamii. Tunamwomba Mungu awajalie busara wasirudie mchezo mchafu kama huu. Na kwa aibu hii ingefaa askofu na mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya waombe radhi wakristo kwa Singida kwa kutumia gari la wakristo kwa shughuli zenye manufaa ya kifisadi, yasiyo na tija hata kidogo kwa maendeleo ya Kanisa.


  Hofu ya viongozi wa serikali kwa ushindi wa Lissu imekuwa kubwa tangu wakati wa kampeni, ndio maana akiwa Singida, Jakaya Kikwete alinukuliwa akisema; "Heri Dk. Slaa awe rais, kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge."

  Pamoja na hayo yote tunawaomba viongozi wa serikali na viongozi wa dini msipingane na sauti za wananchi. Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu.

  Chanzo: Mwanahalisi 10 Novemba 2010
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sijaelewa hii post nadhani nimelewa ama aliyeiweka!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwakweli post ni ndefu sana labda ungeweka abstract...
   
 4. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Du, huyu askofu ni mchungaji aneshirikiana na mbwa mwitu kuwala kondoo wa Bwana!Akafie mbele na u thithiem wake kwenye masula yanayohusu uhuru na haki za kia raia!
   
 5. R

  Rugemeleza Verified User

  #5
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Sijalewa Mchungaji na bahati nzuri huwa sinywi. Kosa langu ni kutokutoa chanzo ambacho ni gazeti la Mwanahalisi. Hivyo hiyo ni habari ambayo nimeona niwashirikshe kwani inaelekea kuna viongozi wa dini ambao wanatumika vibaya na Wanasiasa na ni lazima waumbuliwe na ndivyo gazeti la Mwanahalisi lilivyofanya.
   
 6. R

  Rugemeleza Verified User

  #6
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni habari na usiogope urefu wake soma uhabarike na ujue ni nini kinatokea katika nchi yako mwana kwetu.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Nov 14, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  hawa ccm iwaume mpaka waache ufisadi or perish!
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Nov 14, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu Mimi napata Arrogant Bastard Ale. Hawa si viongozi wa kidini ni nguchiro.

  [​IMG]
   
 9. g

  gaby Member

  #9
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kamanda lisu piga kazi ikiwezekana fanya uchunguzi hadi kanisani kwa huyo askofu huenda na yeye anawachangisha waumini wake michango haramu
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli uyo askofu ana haja ya kutubu
   
 11. Omukuru

  Omukuru JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Post ina kichwa kinachomhusu askofu na bendera ya chama, lakini mwandishi anamnukuru askofu akiongelea mchango, mara oh... gari la askofu ni sadaka ya waumini..., uchambuzi wa dhuluma walizofanyiwa wananchi wa Singida, askofu anahusika vipi. Kwa nini wasilengwe wahusika wa moja kwa moja. Au basi kama mwandishi amepata hiyo sentensi inayohusu waumini kuchangishwa, atuleteee na nyinginezo ili askofu asionekane amefunga safari nzima kwenda kuongea hilo tu. Tusiupotoshe umma kwa kuulazimisha kuangalia mambo yasiyo na msingi na kuacha nchi ikitafunwa na wenye meno.
  Kuna harufu ya chuki binafsi na kutaka kuchafuliana majina, sidhani kama hapa ni mahali pake.
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,359
  Likes Received: 22,224
  Trophy Points: 280
  duh.. kweli hii ni special kwa the perfect happy man
   
Loading...