Askofu amuonya JK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Askofu amuonya JK

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

ASKOFU Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodious Kilaini, amewatahadharisha viongozi wa serikali kutochanganya uswahiba na ushirikishwaji (utendaji) katika uongozi wao, ili kukwepa vitendo vya kifisadi.

Kilaini, mmoja wa viongozi wa kidini wenye ushawishi wa kipekee, alisema ni vema viongozi wakawa na hekima na busara ambazo zitawawezesha kutofautisha kati ya ngano na pumba, uwekezaji na ufisadi, uongozi na ubabe, utumishi na wizi, ushirikishwaji (utendaji) na uswahiba.

Askofu Kilaini ambaye matamshi yake yalionyesha dhahiri kumuelekea Rais Jakaya Kikwete na wasaidizi wake wakuu wa serikali pasipo kuwataja kwa majina, alitoa kauli hiyo jana jijijni Dar es Salaam, alipokuwa akitoa mahubiri katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mburahati, Dar es Salaam.

Mbali ya hilo, Kilaini aliwataka viongozi kutokuwa waoga kwa hofu ya kupoteza madaraka yao, na kuwahimiza kuwa wakweli.

Alisema iwapo viongozi wataacha uoga na kusema kweli, wataweza kukabiliana na mafisadi ambao kwa kiasi kikubwa wamedhulumu mali za wananchi na kuwafanya waishi maisha ya dhiki, huku wao wakiishi maisha ya fahari yaliyojaa kila aina ya anasa.

"Uswahiba na ushirikishwaji kamwe haviwezi kwenda pamoja, hivyo ni vema viongozi wakaachana navyo ili waweze kukabiliana na ufisadi ambao unazidi kushamiri siku hizi," alionya Kilaini.

Alisema kanisa lake litawaombea viongozi ili wawe na busara na hekima ambazo zitawezesha kufanya maamuzi kwa misingi ya haki isiyompendelea mtu au kushawishi kwa rushwa.

"Tutafanya maombi kwa watu wote, lakini hasa kwa viongozi ili waweze kutambua tofauti ya mambo kwa lengo la kuboresha uwajibikaji wao," alisema Kilaini.

Alisema ni vema viongozi wa Tanzania kutofuata tabia ya Pilato ambaye alishindwa kusema ukweli na akaacha Yesu akasulubiwa kwa lengo la kulinda madaraka yake, huku akifahamu fika kuwa anachokifanya si sahihi.

Kilaini alisema kamwe mafisadi hawawezi kuishi maisha ya furaha, amani na upendo kwa sababu wameiba fedha ambazo zingewasaidia yatima, wagonjwa, masikini na wengineo.

Kilaini amewataka mafisadi walioiba fedha kuzirejesha na riba kama alivyofanya Zakayo, ili waweze kuishi maisha ya furaha na amani pamoja na kutubu makosa yao kwa Mungu.

"Mafisadi walioiba fedha za wananchi wanapaswa kuzirejesha na riba, na wasipofanya hivyo kamwe hawawezi kuwa na furaha, amani na upendo mioyoni mwao, kwa sababu wamefanya dhuluma dhidi ya wenzao," alisema Kilaini.

Aliongeza kuwa fedha inawabadilisha watu wengi na hasa kuwachochea katika kushiriki mambo maovu, huku akitoa mfano mmoja wa mwanafunzi wa Yesu, Yuda Eskarioti aliyeamua kumuuza Yesu kwa vipande thelathini vya fedha ili asulubiwe.

Alisema tamaa ya fedha na utajiri wa haraka haraka hivi sasa imekuwa kubwa zaidi kiasi cha kuwafanya watu wajiingize katika vitendo viovu vikiwemo kuwaua maalbino, rushwa na kuwanyima haki wengine, ili wafanikishe malengo yao.

"Vi vema walarushwa, mafisadi na wote ambao wanafanya vitendo vya kiovu wakaongoka ili madhambi wanayoyafanya yasije yakawatokea puani na kukosa msaada," alisema Kilaini.

Kilaini alichukua muda mwingi kusisitiza madhara ya ufisadi kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo wa watendaji waliopewa dhamana ya kuongoza taasisi mbalimbali za serikali.

Miongoni mwa vitendo vya kifisadi vilivyofanywa na watendaji wa serikali ni upotevu wa kiasi cha sh bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) zilizogunduliwa kulipwa kwa kampuni hewa.

Kwa namna moja au nyingine, hotuba ya Askofu Kilaini inatafsiriwa wazi kuonyesha uhusiano uliokuwepo kati ya Rais Jakaya Kikwete na aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye alijiuzulu kutokana na kuhusishwa kwake na ununuzi na utoaji zabuni kwa Kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond.



Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 14 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Askofu,UMENENA.Rais wangu,tunajua kabisa kwamba maswahiba wako uliwapenda na unawapenda,hakuna ambacho hukukielewa kuhusiana na hao swahiba zako,Kinachotusikitisha ni wewe kuzidi kuwapamba,kwamba kilichowasibu ni ajali ya kisiasa.Hivi kweli RAIS WANGU KAULI HIYO UNAIONAJE WEWE BINAFSI?

na D,Juma, Mwanza,TZ, - 22.03.08 @ 10:01 | #3204

Ahsante baba askofu. Hakika umegeuka kuwa tunu. Kila kukicha tunakusubiri kusikia ipi dhambi mpya utakemea. Utajiri wa kifisadi ni dhambi ambayo imesisitizwa na kanisa lako katoliki hivyo you are in line with the pólicy of your church and the will of God. Tunakutakia maisha marefu, pasaka njema na utumishi uliotukuka wa kanisa.

na Quara, Mwanza, - 22.03.08 @ 10:39 | #3211

askofu hongera kwa hilo utajiri wa kifisadi ni dhambi hawatafika popote

na vumilia juma, da es salaam, - 22.03.08 @ 11:54 | #3223

Asante Baba Askofu KILAINI wananchi tumaini letu limebaki kwenu viongozi wa DINI,maana viongozi wetu hawaambiliki ,ukiwaambia kuna hili watasema HAKUNA USHAHIDI,magazeti yakiandika wanamwagiwa TINDIKALI au WANAWATISHIA KUWAPELEKA MAHAKAMANI,tunapata faraja tunapoona hata vingozi wetu wa DINI mnapaza SAUTI ZETU kwani walatini wanamsemo mmoja unasema hivi "VOX POPUL VOX DEI YAANI(SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU)

na deo simba, UK, - 22.03.08 @ 12:05 | #3224

itafika wakati itabidi tuchague viongozi wa nchi kutoka katika maaskofu wetu maana hao tunajua wana moyo wa huruma kwa watu,hawa viongozi wetu hawana huruma kabisa wanajilikimbizia mali utafikili hakuna siku watakufa,nahisi ingewezekana kumnunua mungu ili wasife hawa jamaa wangefanya,hawa ni baadhi tu ya mafisadi wakuu wa nchi ambao wamejilikimbizia mali ambazo tukisema tuwanyang;anye na kulipa tanesco hizo hela hakika umeme utagawiwa bure..ANDREW CHENGE,SUMAYE,MKAPA,MGONJA,ANA MKAPA,MAREGESI,ELISIFU NGOWI,huyo mgonja ndo balaa maana hata wake zake amewahamishia UK na kila mtu ananyumba yake,mimi nipo karibu na mke wake mmoja maisha wanayoishi ni kufuru

na dude, albany.NY, - 22.03.08 @ 12:43 | #3235

Baba Askofu Methodius Kilaini tunakushukuru kwa ujasiri wako wa kukemea vitendo viovu vya watawala wetu. Naamini sasa Kanisa limekwishajutia kosa mlilofanya mwaka 2005, la kusema eti Kikwete
alikuwa chaguo la Mungu. Kiongozi mmoja wa upinzani, nadhani ni Mrema, alihoji ni lini na wapi mlikuwa mmefanya kikao na Mungu akawahakikishia kuwa Kikwete alikuwa chaguo lake! Hamkumjibu.

Kikwete alikuwa anaongoza kundi hatari la wanamtandao. Na sasa imejulikana kuwa wanamtandao hao ndio waliochota mapesa Benki Kuu kufadhili uchaguzi.

Naamini sasa Kanisa limekwishajutia kosa hilo kubwa mlilofanya la kuwadanganya na kuwapotosha wananchi.

Kwa hiyo, katika hizi siku za toba za mateso ya Yesu Kristu, kwa niaba ya Kanisa lako Takatifu, tunakuomba uonyeshe ujasiri, ututamkie Watanzania kwamba mlipotoka kwa kiasi kikubwa mlipotushawishi kumchagua Kikwete na kundi lake. Mkifanya hivyo tutasamehe na tutaendelea kusikiliza na kuzingatia mafundisho yenu. Asante.

na Aloo Ameir, Zanzibar, - 22.03.08 @ 14:46 | #3250

Baba Askofu Kilaini hongera sana kwa mahubili yako lakini lazima tujue kwamba bila kuupiga vita ufisadi nchi yetu haitaendelea na maisha yetu yatazidi kuwa duni. Ufisadi ni moja ya sababu zilizosababisha machafuko na mauaji huko Kenya; mapendekezo ya tume mbalimbali kama za Ndungu juu ya ardhi, Anglo Leasing na Goldenberg watawala walizikalia na hawakuyafanyia kazi mapendekezo yake!! Tunaamini kuwa Rais Kikwete hatafanya makosa hayo kuhusu mapendekezo ya Tume ya Richmond otherwise atakuwa anatutengenezea balaa nchini mwetu

na bulesisiriha, Tanzania, - 22.03.08 @ 17:42 | #3265

Asante sana Baba Askofu Kilaini. Mungu akubariki sana kwa mahubiri yako yenye kuonyesha utetezi wa wanyonge na yenye kuwaonya viongozi wasipore mali ya umma na kuacha uswahiha na waporaji wa mali na rasilimali za nchi kwa manufaa binafsi. Pamoja na hayo Baba Askofu, tunaomba viongozi wa dini msiwe wepesi wa kushabikia wana siasa kabla hamjaona utendaji wao kwa kusema huyu ni "chaguo la Mungu."

na Joseph, Dar, - 22.03.08 @ 17:47 | #3267

Baba Kilaini hongera sana, sasa niwakati wa kanisa kuungama dhambi walioitenda pindi Kikwete alipoharalishwa na kanisa kuwa nichaguo la Mungu,itakuwa na maana kama Baba Askofu akikaa na baraza la Maaskofu na Muungano wa makanisa yote yaani CCT kwania moja tu ya kuuomba msamaha uma na kanisa kwamba walipotoka kwa kumtangaza mtu ambaye sio hata kidogo wala hata hana chembe ya utu kuwa nichaguo la Mwenyezi Mungu.Ukwli nikwamba hakuna Umungu hata kidogo kwa mtu huyu,Ndugu wananchi naomba tuache roho ya unafiki wakupongezana kwa kuogopana kama mambo yanayofanywa Bungeni kuwa JK mchapa kazi hodari mtu wa watu,jamani naomba tu tuone aibu ili tuseme ukweli kama ni***** basi aitwe ***** fisadi aitwe fisadi,angalikua mchapa kazi Balali, rowasa,Karamagi na wenzake wangalikua mahakamani natungalikua na balali inchini.
Nia yangu tu nikutaka watanzania tuwe wakweli tukemee maovu, pia viongozi wa dini zote tunawategemea msitupotoshe na msidanganywe na hao wenye sura za kutabasam kumbe ni mbwa mwitu.

na alex kaila, dodoma, - 22.03.08 @ 18:39 | #3271

Ninamshukuru baba Askofu Kilaini kwakulenga pale sisi watu wa chini ninahitaji, sisi kama watanzania hatuna haja uongo unaofanywa na kiongozi wetu kuwa haukujua nini kinachofanyika, JK alifaham na anajua kila nukta ya ufisadi basi JK ninakuomba utoe aidu abasi uliyonayo kwa hao wenzako wafikishwe mahamani na waludishe kila kisicho haki kwao.viongozi wa dini tunaomba mkaze buti ili huyu Fisadi namba moja atuludishie maisha yetu.

na niwaely, dodoma, - 22.03.08 @ 18:48 | #3272

Ni bora na vyema na haki kama viongozi wetu wa dini mmeng'amuka macho kuwa viongozi wetu wa serikali hawana hata chembe ya utkufu.sisi Tanzania tunakosa gani kwa Mungu tumekuwa na Amani kwa miaka mingi lakini maisha nakuwa magumu kila kukicha,hata uchumi wetu hauwezi kulinganishwa na inchi kama Rwada,Burundi,Congo,Kenya ambao wameonja ukimbizi na kusimamisha shughuli za kiuchumi ili kutafuta amani,naomba tujiulize kama maisha tulionayo sasa ni haya je tungelikabiliwa na sakata la kusaka amani situngelikufa wote? Bila aibu wanapigana wengine sisi tunaathilika kuliko walio vitani.Jamani viongozi wetu hamna hata aibu machoni pa Mungu? Kikwete huna aibu kwnda kusuruhisha walioendelea? JK kama hauna aibu tunakukumbusha kwamba mtanzania ulienae leo sio wa Mwalim nyerere.Tunafaham unacho kifanya we subili hukumu ya Mungu.

na thobias, Kasamwa Geita, - 22.03.08 @ 18:59 | #3273

Ni bora na vyema na haki kama viongozi wetu wa dini mmeng'amuka macho kuwa viongozi wetu wa serikali hawana hata chembe ya utkufu.sisi Tanzania tunakosa gani kwa Mungu tumekuwa na Amani kwa miaka mingi lakini maisha nakuwa magumu kila kukicha,hata uchumi wetu hauwezi kulinganishwa na inchi kama Rwada,Burundi,Congo,Kenya ambao wameonja ukimbizi na kusimamisha shughuli za kiuchumi ili kutafuta amani,naomba tujiulize kama maisha tulionayo sasa ni haya je tungelikabiliwa na sakata la kusaka amani situngelikufa wote? Bila aibu wanapigana wengine sisi tunaathilika kuliko walio vitani.Jamani viongozi wetu hamna hata aibu machoni pa Mungu? Kikwete huna aibu kwnda kusuruhisha walioendelea? JK kama hauna aibu tunakukumbusha kwamba mtanzania ulienae leo sio wa Mwalim nyerere.Tunafaham unacho kifanya we subili hukumu ya Mungu.

na thobias, Kasamwa Geita, - 22.03.08 @ 19:00 | #3274

kwanza napenda kuwapa heri ya pasaka watanzania wote popote pale mlipo,na pili napenda kukupa hongera askofu kilaini kwa kukemea ufisadi na naamini hayo yote uliyosema yametoka moyoni mwako,na si ule unafiki uliofanyika na kiongozi mmoja wa dini,2005 kuambiwa kwamba kikwete ni chagup la MUNGU,na mzee mrema ila yakaishia hivihivi,sasa nashukuru viongozi wa dini mmeamka ingawa bado kuna wengine wanasema ila kwa kujinga'ata maneno ila maneno yako yapo safi kabisa,viongozi wa dini mna nafasi kubwa sana ya kuweza kuongoza mapambano ya ufisadi na hata mkitaka kuiondoa serikali madarakani mana nyuma yenu tutakua wananchi,kikwete kaona wanachi wake hawana mana kwa kumkumbatia swahiba wake rostam ambae yasemekana si mtanzania,naomba muache kutumiwa km sheikh yahya ambae juzi 2 hapa kajitokeza kumsafisha lowassa ila utabiri wake ulishindwa kusema ya kua kikwete hawezi kuawachukulia hatua yoyote marafiki zake waliotajwa,sasa ukicheki utaona huu utabiri wa sheikh yahya ni wa kutumiwa na baadhi ya watu.

na mstari wa mbele, calif/usa, - 23.03.08 @ 02:32 | #3294

Kinachonisikitisha sana ni kuwa wakati wa kampeni baadhi ya viongozi wa dini walisikika wakisema eti Kiwete lilikua chaguo la Mungu. Sio mimi tu, ila watanzania wote ni mashahidi. Mimi nadhani ni vema kumuzuia ***** asiingie kuiba kuliko kumkemea akishaiba. Simlaumu Baba Askofu kwa maonyo yake, lakini ushauri wangu ni kuwa, wasisuburi wezi waingie ikulu au bungeni, bali kemeeni mapema ili wasipate mwanya wa kuingia. Maana wakishaingia, haijalishi kelele ni kubwa kiasi gani, wanaiba kwenda mbele.

na Raphael Mgaya aka Tweve, Uingereza, - 23.03.08 @ 04:22 | #3304
 
ASKOFU HAPA MIONGONI MWA MAMBO ALIYOYAONA NI USWAHIBA......!
WATCH OUT...LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA.....USWAHIBA.....!
 
ASKOFU HAPA MIONGONI MWA MAMBO ALIYOYAONA NI USWAHIBA......!
WATCH OUT...LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA.....USWAHIBA.....!

Inatia moyo kuona Maaskofu, mapadri na mashehe wanakemia maovu yanayofanywa na mafisadi, lakini wito wangu kwao wasingoje mpaka wakati wa X-mas, Easter, Maulidi au Iddi kukemea ufisadi uliokufuru bali hili liwe ni tamko lao la kila siku na kama ikiwezekana kuwatenga mafisadi wasikanyage sehemu za ibada.
 
Inatia moyo kuona Maaskofu, mapadri na mashehe wanakemia maovu yanayofanywa na mafisadi, lakini wito wangu kwao wasingoje mpaka wakati wa X-mas, Easter, Maulidi au Iddi kukemea ufisadi uliokufuru bali hili liwe ni tamko lao la kila siku na kama ikiwezekana kuwatenga mafisadi wasikanyage sehemu za ibada.

MI NADHANI HILO HUWA LINAFANYIKA, NAKUMBUKA HIVI MAJUZI ASKOFU MKUU MTEULE WA ANGLIKANA Dr.VALENTINO MOKIWAALIKEMEA KUHUSU TAKUKURU....NA KWA NINI HOSEA KABAKI...AWAFATE WENZAKE KINA KARAMAGI!
 
Which is which.Mimi nitofautiane na hao maaskofu,mbona mnajichanganya na huyu JK?Nawaambia hao maaskofu na hasa Kilaini,kwamba Mungu sio wa kigeugeu,hivyo nawataka kilamnapofanya jambo lolote mtangulizeni Mungu na sio kujichanganya nyie wenyewe.

Nyie mbona mnakua na kigeugeu cha waziwazi kwa JK,au mlifikili tutasahau kauli zenu,au mlizani atawapa ubalozi,au ilikua ni unafiki wenu tu wa kujikomba kwa JK.Nasema hivyo kwa sababu mara tu baada ya JK kuteuliwa na CCM kama mgombea wa urais mlikaa maaskofu na kutoa tamko kwa vyombo vya habari kwamba JK NI CHAGUO LA KUTOKA KWA MUNGU,leo jk hafai na mnaanza eti kumuonya,haya yametoka wapi au mnataka kutuchanganya sisi watz.

Nyie viongozi wa dini kama mngefanya maombi ya kweli ya kumpendeza Mungu basi Mungu angewaonyesha tangu mapema juu ya JK,lakini nyie mlikulupuka leo mnakuja na mengine.WHICH IS WHICH.
 
Inatia moyo kuona Maaskofu, mapadri na mashehe wanakemia maovu yanayofanywa na mafisadi, lakini wito wangu kwao wasingoje mpaka wakati wa X-mas, Easter, Maulidi au Iddi kukemea ufisadi uliokufuru bali hili liwe ni tamko lao la kila siku na kama ikiwezekana kuwatenga mafisadi wasikanyage sehemu za ibada.

Mashekhe hawaja kemea ila wameunga mkono kazi ya JK .Kanisa pekee hadi msasa limeamua kusema lakini nadhani kuna unafiki .Kama wako real wawaeleze waumini kuimwaga CCM kwenye chaguzi ili tuwe na mambo balanced Bungeni .
 
Which is which.Mimi nitofautiane na hao maaskofu,mbona mnajichanganya na huyu JK?Nawaambia hao maaskofu na hasa Kilaini,kwamba Mungu sio wa kigeugeu,hivyo nawataka kilamnapofanya jambo lolote mtangulizeni Mungu na sio kujichanganya nyie wenyewe.

Nyie mbona mnakua na kigeugeu cha waziwazi kwa JK,au mlifikili tutasahau kauli zenu,au mlizani atawapa ubalozi,au ilikua ni unafiki wenu tu wa kujikomba kwa JK.Nasema hivyo kwa sababu mara tu baada ya JK kuteuliwa na CCM kama mgombea wa urais mlikaa maaskofu na kutoa tamko kwa vyombo vya habari kwamba JK NI CHAGUO LA KUTOKA KWA MUNGU,leo jk hafai na mnaanza eti kumuonya,haya yametoka wapi au mnataka kutuchanganya sisi watz.

Nyie viongozi wa dini kama mngefanya maombi ya kweli ya kumpendeza Mungu basi Mungu angewaonyesha tangu mapema juu ya JK,lakini nyie mlikulupuka leo mnakuja na mengine.WHICH IS WHICH.
TARATIBU...TARATIBU....TARATIBU......! KAMA NI MKRISTO(samahani kama ni dini tofauti au vinginevyo)WANA WA ISRAELI WAKATI WANAHITAJI MFALME KAMA MATAIFA MENGINE "SAULI" NDIYE AKAWA CHAGUO........lakini akaja kuwa muovu ila ni chaguo.....BAADAYE DAUDI....ALIKUWA CHAGUO LA MUNGU ILA.......alihesabu wana wa israeli,alichukua mke wa mtu.......MUSA aliupiga mwamba.....!hii yote ni kuonyesh kuwa mtu anapokuwa CHAGUO sio kwamba hawezi kukosea......!
MAASKOFU SI VIGEUGEU BALI WANASEMA KILO KILICHOPO KWA WAKATI HUO
BIG UP BISHOPS.....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom