Askofu aisifia kampuni ya bia kwa kutoa fungu la kumi.

kuna tofauti gani kati ya bia na divai?

Tofauti ni kama ilivyoandikwa beer and wine. Wine inatokana na matunda, na beer inauokana na nafaka. Alcohol content mara nyingi wine iko juu, ndio maana a glass is enough Kama si mlevi. Beer INS ndogo that's why mtu hunywa hata 7
 
nimehudhuria shughuli nyingi za kilutheri mchungaji anapokuwepo watu hawapewi pombe tunapewa maji soda,mchungaji akishaaga na kuondoka kilaji bia,konyagi huanza kutembea sasa nashindwa kuelewa msimamo wa kanisa la lutherani juu ya pombe!
 
Tofauti ni kama ilivyoandikwa beer and wine. Wine inatokana na matunda, na beer inauokana na nafaka. Alcohol content mara nyingi wine iko juu, ndio maana a glass is enough Kama si mlevi. Beer INS ndogo that's why mtu hunywa hata 7

naona biblia iliitaja wine na sio beer!
 
Hapo ndipo mambo ya utamaduni yanapoingia! Zote ni pombe lkn utengenezaji hudiffer kutokana na raw material na availability ya hizo materials.

Issue ni pombe sio ya mnazi, amarula au Bacardi!
 
nimehudhuria shughuli nyingi za kilutheri mchungaji anapokuwepo watu hawapewi pombe tunapewa maji soda,mchungaji akishaaga na kuondoka kilaji bia,konyagi huanza kutembea sasa nashindwa kuelewa msimamo wa kanisa la lutherani juu ya pombe!
I am not one, so siwajibii. Mimi ni proudly Catholic
 
Askofu kategwa akategeka na pesa za ibilisi. Pesa ni nzuri sana maana hata Biblia inasema "Pesa ni jawabu la mambo yote" (Mhubiri 10:19). Tunahitaji pesa katika maisha yetu ya kila siku ila angalia chanzo chake kisiwe kibaya kama hizi za pombe. Na hapohapo pesa ni mbaya sana maana Biblia inasema shina la mabaya yote ni kupenda pesa (1Timotheo 6:10).
 
1 Timothy 5:23:
Stop drinking only water, and use a little wine because of your stomach and your frequent illnesses
 
mti wa mwiba kamwe tena kamwe hauwezi zaa zabibu...... na mmea wa aloe vera (shubiri) kamwe hauwezi toa asali..........! kila mti usiozaa matund MEMA UTAKATWA NA KUTUPWA KATIKA ZIWA LA MOTO
 
Umesoma maelezo chini? Mkuu wa Karamu akamwita Bwana harusi na kumwambia; "kila mtu huandaa divai nzuri kwanza hata wakishatosheka huandaa ile hafifu. Lakini wewe umeiweka divai nzuri mpaka sasa"

Sijui hiyo juice hafifu ndio huwaje?

Check hapa pia, wewe si umesoma history ya wayahudi! Soma Sira 31:25-31. Kama biblia yako imechakachuliwa (ina vitabu pungufu) pole! ...."pombe ni kama uhai kwa mtu ukinywa kwa kiasi. Maisha yafaa nini bila pombe? Imeumbwa iwafurahishe watu. Kunywa pombe wakati wake na kwa kiasi, huleta shangwe moyoni na furaha rohoni. Lkn kunywa pombe kupita kiasi, huleta kuumwa kichwa, uchungu na fedheha.

Hekima ya Yoshua Bin Sira aka Eklesiastiko

Biblia hukemea ulevi, na ndio maana kwetu huitwa. "mzizi wa dhambi" mywaji sio lazima awe mlevi. Divai wakati wa kula ni utamaduni wa wayahudi, na sio ulevi wa kupindukia, ingawa wapo wachache waliokuwa addicted.

Tupo pamoja mkuu,

Sijui kama kweli kwenye Biblia kuna kifungu kinachokataza kunywa pombe. Kwa ufahamu wangu mdogo, Biblia inakataza ulevi wa pombe haikatazi kunywa pombe. Kama unaweza kunywa usilewe na kufanya mambo ya ajabu ubaya wa pombe huko wapi?.

Tiba
 
Jamani, tusiwe kama Mababu zetu walio letewa injili na waakamini bila kufanya uchunguzi. Kizazi hiki pamoja na maarifa lazima tuonyeshe tofauti sio, tu kwenye maendeleo lakini pia kwenye neno la Mungu. Haiwezekani Mungu aseme ole wake anaye mpa mwenzake kilevi (Habakkuk 2:15, Proverbs31:4-6), halafu yeye mwenye awape kilevi kwenye harusi. Hapa lazima tutumie busara na hekima kujifunza ukweli.
Agano la kale liliandikwa kwa ki Hebrews, na kwenye kihebrews kuna maneno 3, yote ukiatafsiri kwa kiingereza ni 'Wine'
  • YAYIN: Intoxicating, fermented wine (Genesis 9:21)
  • TIROSH: Fresh grape juice (Proverbs 3:10)
  • SHAKAR: Intoxicating, intensely alcoholic, strong drink (often referred to other intoxicants than wine) (Numbers 28:7)
Na agano jipya, translated from Greek inatumia 'wine' for both farmented and unfarmented drink.
Kuna maneno 2 katika kigriki, tafsiri yake kwa kiingereza ni 'wine'

  • OINOS: Wine (generic) Matthew 9:17) - unfermented, (Ephesians 5:18)fermented.
  • GLEUKOS: Sweet wine, fresh juice (Acts 2:13)
Sasa unaposoma Biblia, ukikuta neno Wine, lazima ulewe 'wine' ipi. Otherwise, kama kweli wewe ni msomaji wa neno, Yesu angewapa watu pombe, wafarisayo na waandishi wasingelinyamazia. Lazima lingeibuka maana wao walikua wasomaji sana wa maandiko na Yesu angelitolea ufafanuzi
Tatizo lipo katika tafsiri na waliotafsiri walitafsiri kutumia wakati. Wakati Biblia inatafsiriwa, kule ulaya, neno 'wine' directly meant alcholol, ila siku hivi kuna bibles zina commentaries and dictioneries. Or else kwa wale wanao tetea ulevi (farmented wine/alcohol), someni( Proverbs 23:29-35) kuna onyo kali, kama bado unabisha soma tena Proverbs 14:12-'There is a way which seemeth right unto a man, but the end thereof are the ways of death'. 1Thessalonians 5:22 warns, 'Abstain from all appearence of evil'
 
Wote mnaopinga pombe wekeni mgomo kwenye huduma za sirikali. Hivi hamjui pombe na sigala ndo zinaendesha nchi. Ngoja siku watanzania wote hasa walevi waokoke muone kama nchi itaenda hii. Ukikataa 10% ya mapato ya pombe kanisani utakutana nayo zahanati, hata mishahara yetu sirikalini inatokana na pombe, mchangiaji wa uchumi wetu.
 
i wish waarabu na wamissionari wasingekanyaga ardhi ya nchi hii... Furahieni maisha acheni uzushi

proudly drinker!
 
Usichakachue maandiko bwana. Ile haikua pombe, ni juice inatokana na mizabibu. Kama ingekua pombe, waandishi wangesema kwamba watu walikunywa na kulewa. Hapa lugha ndo inakuchanganya, ila waulize wanaojua Greek, au soma Greek Bible. Otherwise uwe makini unavyosoma Biblia. Wayudi hawakua walevi, kwahio inakuaje Yesu awape Pombe! Tumia akiri

Biblia inasema Divai haikusema juisi. Divai inaeleweka, inakuwa na kiasi fulani ya kilevi. Acheni kujifanya hamjui. Sijui unaposema Wayahudi hawanywi pombe una maana gani? Wapi panapolimwa mizabibu? Kazi yake nini? Tutafautishe kulewa na kunywa, ni vitu viwili tofauti. Hata ukinywa soda ukizidisha unalewa na unaweza kupotesha maisha pia. Kuna mwanamke mwaka jana pia amekufa kwa kunywa maji mengi kila siku ili kupunguza mwili. Too much of Anything is Harmful!!
 
maaskofu wa K.K.T wanatia aibu, wameshaacha misingi ya Biblia wamebakia kama wana siasa. Wapi Biblia inahamassisha kutoa fungu la kumi ya muuza pombe? Breweries, aibu!!!!!!!!!!!!!
 
mti wa mwiba kamwe tena kamwe hauwezi zaa zabibu...... na mmea wa aloe vera (shubiri) kamwe hauwezi toa asali..........! kila mti usiozaa matund MEMA UTAKATWA NA KUTUPWA KATIKA ZIWA LA MOTO

so hata kikombe cha babu loliondo maana dawa yatokana na mti wenye sumu???!!!!!!!!
 
maaskofu wa K.K.T wanatia aibu, wameshaacha misingi ya Biblia wamebakia kama wana siasa. Wapi Biblia inahamassisha kutoa fungu la kumi ya muuza pombe? Breweries, aibu!!!!!!!!!!!!!

.....Nanyi mtakapoliona chukizo la uharibifu limesimama mahali patakatifu, tambueni kuwa majira ya kurudi Mwana wa Adamu yamewadi.
 
Back
Top Bottom