Askof Malasusa acha kujifanya wewe si muuaji.

Danniair

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
360
66
Jioni hii wakati nikiangalia taarifa ya habari, ilifuatia habari iliyomwanyesha Askf. Malasusa aliyeonekana alikuwa akiulilia utawala wa sheria!!

Nikajiuliza mara moja, Je, anaweza kutuambia nini kilijiri hadi wanachuo wa Tumaini mwaka 2010/11 wakaandamana na hata kufukuzwa chuo kwa kudai haki yao ambayo hadi leo hawajaipata, kama si kwenda kwake kinyume na utawala huo wa sheria, akiwa ndiye mkuu wa chuo kikuu cha Tumaini?[ Mimi Danniar nilimaliza masomo yangu ktk chuo kikuu cha Dar (UDSM) years ago.]

Haki waliyokuwa wakidai wanachuo hao ni ile ya kupewa habari ya ni lini wataacha kuchangia Tsh. 1,000,000/= kwa kila mwaka wa masomo watakao hudhuria hapo chuoni? (i.e 3,000,000/= for 3 years).kwa kisingizio cha ujenzi wa chuo.?

Uchangiaji huu sasa umeendelea kwa miaka mingi na hakuna majengo yoyote yanayoonekana kujengwa huko Mikocheni yenye hadhi ya ukusanyaji wa kiwango cha Tsh. 1,000,000 x 300(students in one class) x 3(classes)=900,000,000 /= kila mwaka!!! sasa ni zaidi ya miaka mitano!! Hapo Tumaini Kurasini-cumps office za lecturers ni kotena juu ya kontena. Sijui std za maktaba iko vipi hapo kurasini.

Serikali inaona na imekaa kimya, nasema inaona kwani ni hivi majuzi tu ilikwenda kufunga shule kule Taborapia, iliahidi kufunga nyingine kule Morogoro. Askofu asiyetosheka anajua na anakula humo, pia yuko kimyaaa kabisa. Wazazi wanaumizwa kisa , eti kanisa linatoa mchango wa elimu. Bora Kanisa liache, kama halifuati haki. kwani mwanasheria huyu akiisha ingia ktk system, nina uhakika lazima atapokea rushwa ili kufidia maumivu ambayo wazazi wake waliyapata alipokuwa akiitafuta degree yake. Na kwa mchezo huu rushwa haitakoma kabisa. Huenda ndo maana wazazi wao wako kimya kwani wanajua pesa yao itarudi tu after 3 yrs.

Je, ni haki gani mtu aanzishe business zake na alazimishe wateja wanaokuja ili kuchangia mitaji yake? kwa vipi? Kwa sababu, mbali na Ths. 1M/= bado mwanachuo analipia Tsh. 1,500,000/= kwa elimu yake i.e kwa mwaka mzazi anawajibika kujikamua tsh. 2,500,000/=. Kisa , KANISA!!

Je, hayo si mauaji ya kutisha kwa watanzania wenzio (Askofu) ambao uchumi wao ni mdogo? Na sasa ni miaka mingi inapita kila mwaka ukikusanya pesa yao na chuo hakijengwi huko Mikocheni, ila mnakula interest kila mwaka. Bora kifo cha mwili kuliko kifo unachowafanyia watanzania wenzako na mazingira zahiri ya rushwa unaowajengea watoto hawa na jamii yetu kwa ujumla. Kiasi cha michango hakipungui na chuo hakijengwi. mradi tosha kwa kanisa lako.

Mwogope muumba wako ukatende sawa na sheria za nchi na amri ya 'Usiibe'. Mchezo huu tunauona St Marian bagamoyo pia, lakini kule wazazi huchangia mara moja kwa mwaka tu. Kwa malasusa ni miaka yote, WHY?

Kwa wale wachangiaji wa uzi huu nawashukuru sana. Ila pia nawashauri kuwa hapa JF si mahali pa walevi kupageuza kijiwe kama mlivyochangia uzi huu. Inapotokea mada inamhusu kiongozi wa juu/ kiongozi maarufu, basi fikiria kidogo ndipo uijibu hoja hiyo kwa manufaa ya taifa. Asanteni sana
 
sioni la kuchangia maana sijaelewa hata mleta mada anamaanisha nini! Wasomi wa leo hata kujieleza ni shida! sijui ni matokeo ya shule za kata?
 
Wamesharikoroga hujaona nchimbi anamshangaa mwema, ccm hamjielewi poleni sana
 
wewe mleta mada mzima kweli wewe? I mean upstairs. Mzee wa watu kazungumzia tatizo la mauji kiholela na uvunjifu wa sheria na haki za binadamu kunkofanywa na vyombo vyetu vya usalama wa raia na mali, i mean polisi halafu wewe unaleta siasa za chuo, sijui ada! Yaani hada mada ulivyopresent hakika sidhani kama kuna aliekuelewa

pengine una ujumbe unataka kufikisha but jipange vizuri namna ya kupresent ujumbe wako.

Otherwise kumuita mtu muuaji dah kisa umeshindwa kulipa ada ya shule yahitaji moyo
 
kama kuna kitu huwa naheshim ni uhuru wa mtu kusema anachokiamini kuwa ni kweli. Ila pia kuliko mtu aseme asichoweza kukieleza kikaleta mantiki basi ni bora aulize swali tu juu ya anachokiamini.
 
Jioni hii nikiangalia taarifa ya habari, lakini cha ajabu ni kuwa Askf. Malasusa alikuwa akililia utawala wa sheria!! Je, anaweza kutuambia nini kilijiri hadi wanachuo wa Tumaini mwaka 2010/11 wakaandamana na hata kufukuzwa chuo kwa kudai haki yao ambayo hadi leo hawajaipata.Haki yenyewe ndiyo ya kukusanya Tsh. 1,000,000?= kwa mwaka toka kwa kila mwanachuo kwa muda wake wa miaka yote anapokuwa chuoni hapo? i.e 3,000,000/= kwa kisingiziocha ujenzi wa chuo. Je, hayo si mauaji ya kutisha ya watanzania wenzio ambao uchumi wao ni mdogo? Na sasa ni miaka mingi inapita kila mwaka ukikusanya pesa yao na chuo hakijengwi huko Mikocheni, ila mnakula interest kila mwaka. Bora kifo cha mwili kuliko kifo unachowafanyia watanzania wenzako. Kiasi hakipungui na chuo hakijengwi.Mwogope muumba wako ukatende sawa na sheria za nchi na amri ya 'Usiibe'
kwa kifupi ni kwamba, kile chuo mimi ni mmoja wapo wa watu tuliochangia kukijenga, kipindi hicho bado nilikuwa nasali lutheran. nilihama lutheran lakini hadi leo hii bado nampongeza sana askofu mdegella wa iringa kwa kujenga chuo kile na shule zingine nyingi sana kule iringa na mikoa meingine. tulichanga kabisa, na sadaka zilitolewa ndo maana wewe ulienda kusoma pale, hukujua chuo kile kilitoka wapi, ila kwa kifupi ni kwamba hadi masikini wa vijijini walichanga kwaajili ya kile chuo tena kwa moyo bila kulazimishwa na sadaka zetu nyingi zilienda kujenga chuo kile ambacho wanaasoma walutheran, waislam, walokole,wakatoliki etc...pamoja na kwamba waliochangishwa mara ya kwanza na kukijenga chuo kile walikuwa walutheran peke yao...ndo maana tunasema wakristo tunao uwezo wa kujiendesha sisi wenyewe kwasababu tumefundishwa kutoa kwa moyo kujenga shule au hata kusaidia masikini sio kama watu wengine ambao wanaomba majengo ya tanesco ambayo yako tayari waingie kuanzisha chuo...kulialia hadi lini?kama wewe ulifeli vyuo vingine ukalazimika kwenda Tumaini, nani alikwambia ufeli? si ungeenda udsm kama una ubavu? hapo kwenda tumaini ulikuwa unasaidiwa tu kusoma chuo ambacho hukuchangia hata senti moja kukijenga ukijua kuwa pale kile chuo hakina mfadhili yeyote zaidi ya ada hizo na sadaka za walutheran ndo zinalipa malecturer wenu wanaofundisha watu wa dini zote. majengo mapya yatatoka wapi? unafikiri watabaki kulalama tuuu kuomba msaada wasaidiwe na selikali kama watu wengine? noooo, cha muhimu ni kujifunza kuwa na moyo wa kuchangia kujenga kitu kwenye jamii yetu kwasababu kitasaidia watu wetu...acha mkono wa birika, utakufa masikini.hutabarikiwa kwasababu ya kuwa mchoyo kutoa kwa watu wengine au kutoa kwaajili ya ujenzi wa jamii yako.
 
Jioni hii nikiangalia taarifa ya habari, lakini cha ajabu ni kuwa Askf. Malasusa alikuwa akililia utawala wa sheria!! Je, anaweza kutuambia nini kilijiri hadi wanachuo wa Tumaini mwaka 2010/11 wakaandamana na hata kufukuzwa chuo kwa kudai haki yao ambayo hadi leo hawajaipata.

Haki yenyewe ndiyo ya kukusanya Tsh. 1,000,000?= kwa mwaka toka kwa kila mwanachuo kwa muda wake wa miaka yote anapokuwa chuoni hapo? i.e 3,000,000/= kwa kisingiziocha ujenzi wa chuo. Je, hayo si mauaji ya kutisha ya watanzania wenzio ambao uchumi wao ni mdogo? Na sasa ni miaka mingi inapita kila mwaka ukikusanya pesa yao na chuo hakijengwi huko Mikocheni, ila mnakula interest kila mwaka. Bora kifo cha mwili kuliko kifo unachowafanyia watanzania wenzako. Kiasi hakipungui na chuo hakijengwi.

Mwogope muumba wako ukatende sawa na sheria za nchi na amri ya 'Usiibe'

Vague! Hata unachoongea ukielewi?
 
Askofu Malasusa sio muuaji, na unamfananisha na nani? unaijua historia ya kuchaguliwa kwake baada ya kutokea mvutano mkubwa wa maaskofu kutaka kiti hicho? Mimi ni mLutheri namjua sana wewe mwaga data au usepe
 
Kama 'wasomi' wenyewe tunaowazalisha vyuoni ndiyo type hii tuna kazi kweli kweli! Mbona huyu haeleweki anamaanisha nini? Kujieleza kwa kiswahili tu hivyo, je ingekuwa lugha ya kikoloni ingekuwaje? Kuna kitu hapo? Inawezekana alikuwa na ujumbe aliotaka jamii iufahamu lakini the presentation was extremely poor! Pole.
 
Askofu Malasusa sio muuaji, na unamfananisha na nani? unaijua historia ya kuchaguliwa kwake baada ya kutokea mvutano mkubwa wa maaskofu kutaka kiti hicho? Mimi ni mLutheri namjua sana wewe mwaga data au usepe
Asante kwa kuliona hilo Mkuu, hata mimi si mu Anglikana lakini namheshimu sana Askofu huyu. Ni makini sana katika kujieleza na ana uelewa mpana kabisa wa mambo. Hakurupuki.
 
hey i fobbid u from insulting my bshop n no mor discussion abt dis understand
 
mtoa mada funguka tukusome fresh inawezekana una point sema hujajipanga kujieleza calm dowm, punguza jazba
 
mtoa mada jieleze vzr tukuelewe, inawezekana una hoja ya msingi ila punguza hasira na panga maneno yako vzr utaeleweka.
 
Back
Top Bottom