Askari zaidi 50 wa Burundi wahofiwa kuuawa katika mapigano dhidi ya waasi

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
636
1,842
Burundi.jpg

Jeshi la Burundi limepoteza askari zaidi ya 50 katika mapigano na watu wenye silaha yaliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika Msitu wa Kibira, Wilayani Mabayi, Mkoani Cibitoke, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa.

Vyanzo kadhaa kutoka serikali ya Burundi na jeshi ambavyo havikutaka majina yao yatajwe vimethibitisha taarifa hiyo, lakini vimesema kuwa shambulio hilo liliendeshwa na Rwanda.

Hata hivyo serikali ya Burundi na jeshi bado hawajathibitisha habari hii. Lakini mashahidi kutoka Wilaya ya Mabayi wamethibitisha habari hii, na kubaini kwamba askari wengi wamejeruhiwa na wengine hawajulikani waliko.

Hakuna kundi hata moja la waasi ambalo limekiri kuhusika na shambulio hilo, lakini hivi karibuni kundi la waasi la Red-Tabara lilitangaza kuwa limeanzisha vita dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka Wilaya ya Mabayi, raia wanaoishi karibu na Msitu wa Kibira wamelazimika kuyahama makaazi yao kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo hilo.

Burundi inaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu ikiwa imesalia tu miezi isiozidi kumi kabla ya uchaguzi wa urais.

Chanzo: RFI Kiswahili
 
1574144437528.png
Jeshi la Burundi limepoteza wanajeshi zaidi ya 50 katika mapigano na watu wenye silaha yaliyotokea usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili katika Msitu wa Kibira, Wilayani Mabayi, Mkoani Cibitoke, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa.

Vyanzo kadhaa kutoka serikali ya Burundi na jeshi ambavyo havikutaka majina yao yatajwe vimethibitisha taarifa hiyo, lakini vimesema kuwa shambulio hilo liliendeshwa na nchi jirani ..

Hata hivyo serikali ya Burundi na jeshi bado hawajathibitisha habari hii. Lakini mashahidi kutoka Wilaya ya Mabayi wamethibitisha habari hii, na kubaini kwamba askari wengi wamejeruhiwa na wengine hawajulikani walipo...

Hakuna kundi hata moja la waasi ambalo limekiri kuhusika na shambulio hilo, lakini hivi karibuni kundi la waasi la Red-Tabara lilitangaza kuwa limeanzisha vita dhidi ya utawala wa Pierre Nkurunziza.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka Wilaya ya Mabayi, raia wanaoishi karibu na Msitu wa Kibira wamelazimika kuyahama makaazi yao kufuatia kuzorota kwa hali ya usalama katika eneo hilo.

Burundi inaendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu ikiwa imesalia tu miezi isiozidi kumi kabla ya uchaguzi wa urais.

Chanzo: RFI SWAHILI
 
Nkurunzinza atapambana na hali yake peke yake now day Tz wanaangaria maslahi yao tu. Ila PK akichanga karata zake vibaya huko kuwasapoti Red Tabara kutam-Cost yeye na Rwanda yake.
 
Kuna madai kuwa hao waasi wanaspotiwa na PK burundi wanaweza kujibu kwa kuingia mazima vitani na PK maana burundi hawana cha kupoteza
Sawa Ila ni lazima kuwepo ushahidi usio na shaka utakaoifanya Burundi kupata baraka za jumuiya za kimataifa kama EAC na AU kuivamia Rwanda.

Swari la kujiuliza is Burundi having such guts to attack Rwanda despite the fighting against the rebels in the country?
 
PK ambaye ana uwezo wa kuivuruga DRC ndo unasema Burundi itamcost? Siamini katika hili
DRC inavurugwa na watu wengi pia kumbuka hapohapo DRC majasusi wengi wa mossad waliuwawa na majasusi wa china so DRC ni uwanja wa mapambano Hata kwa mabeberu pia

Kama burundi ataingia vitani directly na rwanda ni kuwa vit hii itapiganwa kiukabila zaidi na hichi kitu kitawapa faida zaidi burundi
 
Madai ya burundi ni kuwa hilo shambulio limeendeshwa na wanajeshi wa rwanda pia kiualisia hao waasi wa burundi hawana nguvu kivile
Sawa Ila ni lazima kuwepo ushahidi usio na shaka utakaoifanya Burundi kupata baraka za jumuiya za kimataifa kama EAC na AU kuivamia Rwanda.

Swari la kujiuliza is Burundi having such guts to attack Rwanda despite the fighting against the rebels in the country?
 
Naona Mtu mrefu mwembamba leo ame deliver kile alicho kiahidi siku 5 zilizopita.

We are going to raise the cost on the part of anybody who wants to destabilise our security. The cost is going to be very high, whether it is the means we are going to put into that to make sure we have everything it takes to ensure security and stability of our country and our development.

It is also the cost, mainly that those people who want to destabilise our country are going to incur, it is going to be a very high cost on their part. Absolutely.

I mean it and you know that I mean it,” Kagame added.
 
Rwanda kazungukwa na adui zake... Uganda na Burundi watamshinda Vita.
Uganda hana uhusiano wa kuisaidia Burundi kwenye vita,bora ungesema Tz ya Kikwete na wala si ya JPM. Congo nao wachovu wako bize na mambo yao labda walazimishe nia ya kufuta maadui. Hata hivo hizi ni kama 'WHAT IF' ambazo huwa hazina majibu
 
Ugumu unakuja hapa kuwa hizi nchi mbili zikitwangana watapigana kiukabila zaidi
 
Wanajeshi Waliouwawa ndo hao Burundi inawaaminia kua ni battle hardened na wametoka kwenye mission huko somalia/AMISOM.
 
Back
Top Bottom