Askari wetu wajitambue wafanye kazi kwa weledi hasa wanapokuwa na silaha

vannistelrooy

JF-Expert Member
Jan 31, 2017
316
644
Ni hatari kwa askari polisi mwenye silaha kuendesha bodaboda alafu nyuma yake kakaa raia ambaye hamfahamu. Yule raia anaweza akafanya lolote hata kumpora silaha. Ni muhimu polisi wenye silaha kujitambua nafasi zao na kufanya kazi kwa weredi anapokuwa na silaha.

Leo nilikuwa maeneo ya Oysterbay niliona askari polisi wawili kwenye pikipiki maarufu kama Tigo wakiwa na silaha. Baada ya muda walirudi wakiwa wamekamata pikipiki.

Huwa wakikamata bodaboda wana tabia ya kuichukua na kuamua kuiendesha alafu dereva anakaa nyuma wanaelekea sehemu ambayo wanaona wao ni salama

Polisi naomba wajitambue kwenye hili, waangalie njia sahihi ya kukamata wale bodaboda. Na pia wafanye kazi ya kusimamia usalama na sio kukusanya buku 5 5
 
Back
Top Bottom