Askari watatu wa kulinda amani kutoka Burundi wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
5,387
2,000
Askari watatu wa kulinda amani kutoka Burundi wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Askari watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao ni raia wa Burundi wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mapigano yakishadidi katika nchi hiyo ambayo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu hapo kesho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, wanajeshi watatu kutoka Burundi na wenzao wawili wamejeruhiwa kufuatia uvamizi dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa na vya serikali.

Mashambulizi dhidi ya askari hao yamejiri katika mji wa Dekoa ulio katika mkoa wa Kemo na mji wa Bakouma kusini mwa mkoa wa Mbomou.

Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alilaani vikali mashambulizi hayo na ametoa wito kwa wakuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wachunguze mashambulizi hayo."uvamizi wa kikatili."

Aidha ametahadharisha kwamba "mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuchukuliwakuwa ni jinai za kivita."

Huku uchaguzi ukikaribia, Rais Faustin Archange Touader amemtuhumu rais wa zamani Francois Bozize kuwa anapanga kufanya mapinduzi dhidi ya serikali iliyko madarakani.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakilinda doria Jamhuri ya Afrika ya Kati

Boziei, ambaye amewekewa vikwazo na Umoja wa Maaifa na amezuiwa kuwania urais, amekanusha tuhuma hizo.

Siku ya Jumanne waasi waliuteka kwa muda mfupi mji wa Bambari, ambao ni mji wa nne kwa ukubwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mji huo ulikombolewa katika oparesheni ya pamoja ya wawalinda amani wa Umoja wa Mataifa wakisaidiwa na vikosi vya serikali. Wiki iliyopita waasi walitishia kuanzisha oparesheni dhidi ya mji mkuu, Banguil lakini walishindwa kufanya hivyo kufuatia msaada wa kimataifa.

Taarifa hizo zimekuja katika wakati ambapo muungano wa waasi umetangaza kusitisha Rwanda na Russia zilituma askari zaidi katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini ili kuzuia waasi kuipindua serikali.
 
lamaa

JF-Expert Member
Nov 2, 2018
626
1,000
1: Nwe colonialism
2: Tribalism
3: Puppet leader
4: Poverty
5: Ignorance
6: Imperialist(Mabeberu)Infuluence
7: Corruption
8 DisUnity Among African

Hivi Vitu Vitaendelea kutumaliza Africa
 
covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
1,611
2,000
Askari watatu wa kulinda amani kutoka Burundi wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

[https://media]

Askari watatu wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa ambao ni raia wa Burundi wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mapigano yakishadidi katika nchi hiyo ambayo inajiandaa kwa uchaguzi mkuu hapo kesho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, wanajeshi watatu kutoka Burundi na wenzao wawili wamejeruhiwa kufuatia uvamizi dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa na vya serikali.

Mashambulizi dhidi ya askari hao yamejiri katika mji wa Dekoa ulio katika mkoa wa Kemo na mji wa Bakouma kusini mwa mkoa wa Mbomou.

Stephane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, alilaani vikali mashambulizi hayo na ametoa wito kwa wakuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wachunguze mashambulizi hayo."uvamizi wa kikatili."

Aidha ametahadharisha kwamba "mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa yanaweza kuchukuliwakuwa ni jinai za kivita."

Huku uchaguzi ukikaribia, Rais Faustin Archange Touader amemtuhumu rais wa zamani Francois Bozize kuwa anapanga kufanya mapinduzi dhidi ya serikali iliyko madarakani.

[https://media]Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa wakilinda doria Jamhuri ya Afrika ya Kati

Boziei, ambaye amewekewa vikwazo na Umoja wa Maaifa na amezuiwa kuwania urais, amekanusha tuhuma hizo.

Siku ya Jumanne waasi waliuteka kwa muda mfupi mji wa Bambari, ambao ni mji wa nne kwa ukubwa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Mji huo ulikombolewa katika oparesheni ya pamoja ya wawalinda amani wa Umoja wa Mataifa wakisaidiwa na vikosi vya serikali. Wiki iliyopita waasi walitishia kuanzisha oparesheni dhidi ya mji mkuu, Banguil lakini walishindwa kufanya hivyo kufuatia msaada wa kimataifa.

Taarifa hizo zimekuja katika wakati ambapo muungano wa waasi umetangaza kusitisha Rwanda na Russia zilituma askari zaidi katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini ili kuzuia waasi kuipindua serikali.
sehemu yyt ukisikia majeshi ya rwanda yapo tena kwawingi kaa mguu sawa..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom