Askari Waliowalazimisha Wanawake Kunyonya Sehemu Zao Za Siri Kukiona –Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari Waliowalazimisha Wanawake Kunyonya Sehemu Zao Za Siri Kukiona –Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, Jun 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280


  [​IMG]
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda Friday, June 11, 2010 12:17 PM
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana aliomba radhi kwa niaba ya serikali kufuatia tukio lililoripotiwa kwenye vyombo vya habari kuwa kuna askari polisi waliwadhalilisha wanawake kwa kuwavua nguo na kisha kuwalazimishwa kuwanyonya sehemu zao za siri. Kufuatia tukio hilo Waziri Pinda aliwaomba radhi wananchi wote kwa ujumla na kuelezea kusikitishwa na vitendo hivyo vya askari polisi walivyowafanyia wanawake hao kwa kuwa ni kinyume na utendaji wa jeshi hilo.

  “Kwanza naomba niombe radhi iwapo tukio hili la aibu ni kweli limefanywa na askari polisi kwa sababu si jambo la kawaida katika jamii ya watanzania, polisi kuweza kufanya kitendo cha udhalimu wa namna hiyo. Nasema kama ni kweli watakiona “, alisema Pinda.

  Pinda alisema jana Bungeni kuwa atahakikisha askari waliohusika katika vitendo hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

  Pinda aliyasema hayo baada ya kufuatia kuulizwa swali la papo kwa papo na mbunge wa Tarime [Chadema] Charles Mwera kutaka kujua ni hatua gani zinachukuliwa na serikali kufuatia vitendo hivyo vilivyofanywa na askari hao.

  Pinda alijibu hayo na pia kumuahidi mbunge huyo kukutana naye mara baada ya kikao hicho cha bunge ili atoe maelezo kiundani kuhusu madai hayo na kumuagiza Waziri wa Mambo ya ndani wawe nae katika mazungumzo hayo.

  Mbunge huyo alisema kuwa kuna baadhi ya askari polisi mkoani Mara waliwakamata wanawake na kuwaamuru wawavue nguo zao na kisha kuwaamrisha kuchezea nyeti za askari hao kabla ya kuwalazimisha kuzinyonya nyeti hizo.

  Swali la mbunge huyo kwa Waziri Mkuu liliwaacha wabunge wengi vinywa wazi wasiamini kama kweli mambo haya yanafanyika Tanzania.

  NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
 2. M

  Mchili JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mh!!!!!!!!!!! Hii ni mpya.
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo hao askari waliwalazimisha wanawake wa go down? Mh..hizi tamaduni za kuiga zinatupeleka arijojo nduguzanguni.
   
 4. Maarifa

  Maarifa JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2010
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 2,880
  Likes Received: 1,049
  Trophy Points: 280
  Hao akina mama si wangewang'ata???
   
 5. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  He uwendawazimu umeshaingia TZ laahaulaaaa
   
 6. P

  Pierre III Member

  #6
  Jun 14, 2010
  Joined: Jun 1, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  These guys from Tarime know how to use swords( mapanga shaa) , how comes they did'nt castrate even one askari. can u imagine an askari forcing your mom, sister or wife kushika na kulamba microphone!
   
 7. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Naona wanaiga ya kule Congo kwa waasi mmmh
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  huu ni udhalilishaji wa hali ya juu, yaani umepita kiwango!
   
 9. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  stunning! ningekuwa IGP ningehamia huko kwa siku kadhaa.
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mkuu kule Tarime mara nyingi huwa kunakuwaga na special forces na operations maalum kutokana na mazingira ya kule...ya vita vya kikabila, uwizi wa ng'ombe na uhalifu mwingine. Wananchi wenyewe tu wamepinda kinyama. Usipime. Kwa kifupi wananchi wa kule ni wasumbufu na hizi shida ni za kujitakia kwa kiwango fulani.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Lakini kwa the legends tulizokuwa tunasikia, hii kadhia ni cha mtoto. Mbinu dhalili zaidi zilikuwa zikitumika kwenye siku za awali. Kuna ya mtu kulazimishwa kufanya mapenzi na mama mkwe au mama mzazi usiposhirikiana na geshi ra porisi et et c..Ni kwamba tu sasa tunaishi kwene kizazi cha dot com ndo maana watu wanapanic humu.!

  I aint supporting it, I'm just saying.
   
 12. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  hawa polisi unawajua sana, wakinifanyia mimi hivyo watajuta kuzaliwa.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Tarime wanatumalizia bajeti yetu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kutokana na uhalifu wao.PERIOD.
   
 14. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,288
  Likes Received: 22,050
  Trophy Points: 280
  Masha anangoja nini kujiuzulu?
  Jeshi halina maadili, awapishe wengine watakaoweza kulinyoosha
   
Loading...