Askari waliomteka Ulimboka ni wazalendo wa kweli

Wasiwasi ni kwamba, kama ni kweli serikali inahusika na jambo hili basi maisha ya huyu Dr. yapo zaidi hatarini maana watafanya kila linalowezekana kimmalizia ili siri isivuje.. Dah, naona kama sinema hivi
 
Wakati mwingine nawalaumu madaktari kwa mgomo wao lakini kwa hapa hebu nitulie japo kidogo ili nitafakari.
Hivi kama kweli kuna mkono wa serikali kwa hili la Dr Ulimboka, wanadhani wakishaua mtu mmoja watakuwa wamewalainisha madaktari wote hapa Tanzania kuachana na mgomo?
Ama kweli JK na serikali yake ni wadhifu kuliko hata uji wa mhogo.
WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI.
 
Wasiwasi ni kwamba, kama ni kweli serikali inahusika na jambo hili basi maisha ya huyu Dr. yapo zaidi hatarini maana watafanya kila linalowezekana kimmalizia ili siri isivuje.. Dah, naona kama sinema hivi

Kwa mtizamo wangu sidhani kama Serikali inaweza kufanya ujinga kama huu. Kutakuwa na genge la wahuni limehusika kwa ajili ya kuichafua serikali. Serikali wangemchukua na kumficha somewhere kwa muda flani tu then yeye baada ya kutoka huko angetangaza kuisha kwa mgomo kwenye maisha yake yaliyobaki
 
Kiongozi wa madaktari kufanya kikao na watu asiowajua?? au alikuwa anafikiria atapewa mlungula?

Mimi nina wasiwasi sana na huyu dokta Ulimboka!

Tangu zamani nilikuwa nadhani una akili lakini...............kwa siku ya leo comment zako ni mavu....zi matupu
 
Kwenye Taarifa ya Habari jana usiku walitangaza makahama kuu kitengo cha kazi wamewataka madr.wote kusitisha mgomo wao mara moja wakaenda mbali zaidi kuwa Mwenyekiti wao Dr. Ulimboka aende kwenye vyombo vya habari na kutangaza kuwa wamesitisha mgomo failure to do so sheria itachukua mkondo wake!Kama ni utekelezaji wa Agizo la Mahamaka basi lingekuwa leo sasa kabla Dr. Ulimboka hajawajibu limetokea je vinauhusinano?
 
Ujumbe amenitumia Daktari yupo pale MOI.

‘Kaka Zitto, hali ya Dr.Ulimboka yuko unconscious, multiple ribs fracture na kwenye mikono pia amevunjika pamoja na taya,yuko icu wanamstabilise kwanza kwasababu hapumui vizuri,the situation here is really bad,I agree with you this is outright outrageous’

Nimechukizwa sana na habari za kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa Dr Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari Nchini. Mambo kama haya tumezoea kuyasikia kwenye nchi za kidikteta na kuongozwa kiimla ambapo watawala badala ya kutumia njia ya kidemokrasia na kisheria kushughulikia wanaoamini ni maadui zao katika utawala, hutumia wahuni katika Taasisi za usalama kuteka raia, kuwatesa, kuwafunga na hata kuwaua.

Sitaki kuamini kwamba Tanzania imefikia huko. Nimezungumza na baadhi ya madaktari walio karibu na Dokta Ulimboka na kujulishwa kwamba majeruhi huyu wa vitendo vya hovyo kabisa kutokea hapa nchini alikamatwa jana usiku mnamo saa sita na watu wasiojulikana na kupelekwa katika msitu wa MagwePande na kujeruhiwa vibaya. Habari hizi bado hazijathibitishwa na vyanzo huru lakini ndio zilizopo hadi hivi sasa.

Serikali kama mlinzi wa usalama kwa raia inaWAJIBU kueleza tena kwa haraka ni nini kimetokea kwa kijana huyu msomi na kiongozi wa wataalamu wenzake. Serikali INAWAJIBIKA kueleza katika nyakati kama hizi ambapo kuna mgogoro kati yake na madaktari imekuwa wapi kuhakikisha usalama wa viongozi wa madaktari ili kuepusha watu wanaoitwa 'agente provocateure' kuweza kuhatarisha hali ya amani ya nchi na hata kupelekea kuweka hali ya vitisho kwa madaktari wetu.

Serikali INAWAJIBIKA kueleza kama sasa imeamua kutumia njia za kihuni kumaliza matatizo na wananchi wake.

Nimemuomba Waziri Kivuli wa Afya wa CHADEMA kufuatilia suala hili kwa kwa karibu sana ili kuhakikisha kwamba ukweli wote na ukweli mtupu unafahamika. Kamwe hatuwezi kuacha Mtanzania yeyote aonewe, anyanyaswe au akandamizwe eti kwa sababu ya kudai haki yake na za wenzake. ‘An injury to one, injuries to all’.

Naomba madaktari wamwangalie kwa karibu daktari mwenzao ili aweze kupata nafuu. Ulinzi uimarishwe ili kuhakikisha usalama wake.
 
...Nimejikuta namkumbuka hayati IMRAN KOMBE(Aliyewahi kuwa Mkurugenzi Mkuu Idara ya Usalama wa Taifa). Aliuwawa kwa kukusudia, na waliomuua leo hii wapo Uraiani, Serikali hii ya CCM inawaita ni Mashujaa...
Mungu Ibariki Tanzania
 
Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.
 
For this, serikali imefail na hata kama watasema hawahusiki ni vigumu kuliamini hilo maana leo ndio madaktari wangetoa tamko lao.
 
wakati facebook imegeuka mtandao wa ki-ma-la-ya tanzania JF imegeuka mtandao wa WAMBEYA
 
mwana_mapinduzi unamjua mhusika???? anayemjua amtaje sote tumuadhibu......ila kitu DHANA ni dhambi inayotafuna 95% ya JF. CONTIBUTORS...!
 
Serikali dharimu ya CCM inauwa watu wake ikijua ndiyo njia ya kutatua matatizo,serikali hii dhaifu mwisho wake umefika.
 
Waliomteka si askari waliomteka ni sheria,rejea taarifa ya habari ya jana usiku


kwa maana hiyo inatubidi kereview sheria zetu kama ni za ki-zalendo au la.
 
Back
Top Bottom