Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,980
Trafiki wamekuwa kero hasa kipindi hiki cha Uchaguzi ambacho viongozi wote wa serikali wamekimbilia kwenye majukwaa ya siasa. Wamefanya mradi kwa daladala, kila ukipita umwachie 1000 au 2000 bila hivyo anakuandikia elfu 30000.
Zipo video na picha zinazoonyesha namna wanavyokusanya mapato binafsi. Makusanyo haya yanafanywa kwa wajasiriamali na walala hoi lakini uoni wenye mashangingi na magari ya hadhi wakisumbuliwa.
Bodaboda kila kona wanakamatwa, bajaji na vigari vidogo vya mzigo ndo usiseme. Je, viongozi wa wizara ya mambo ya ndani amwoni? Viongozi wa polisi hiki kinachotokea amkioni? Mnadhani uchungu walionao bodaboda, madalala drivers, makondakta na waendesha vigari vidogo utaicha CCM salama?
Jifunze kutenda haki, simamieni haki, kuweni sehemu ya kuboresha maisha ya wajasiriamali wa nchi hii,punguzeni wahalifu kwa kulinda kundi la vijana lililojitolea kujiajiri.