Askari wa usalama barabarani wakimpiga raia

Hivi unajua mtu anayepigwa anapigwaje???

Umeshawahi kuona mtu anatandikwa wewe???

Huyo mtu amepigwa,au anavutwa vutwa shati??

Huyu hajapigwa labda hujui mtu anapigwaje???
Unajua mtoto wa kishua ukimvuta 2 anakimbia kwa ding yake analia kinouma... Kapigwa
Ndo hi video...
Sijaona kipigo zaid ya msukumano sema siku hz kila kitu kiki
 
Kwa hiyo mahakama zimewekwa za kazi gani wewe mtu?

Kwani na Wewe pale Mkeo anapokuudhi na unampiga hadi karibia na Kumjeruhi kwa muda huo Vyombo vya Kumshtakia vinakuwa vipo Likizo? Halafu yawezekana umesoma maelezo yangu ila pengine kwakuwa una matatizo ya ' Kufikiri ' hujaelewa. Sijatetea walichokifanya hao Matrafiki ila na Mimi pia nimeelezea hatua njema na nzuri za kuchukua kwa Watumiaji wa barabara ili kuepuka hayo matatizo siku za mbele.
 
mkuu bado unapiga mwanamke siku hizi?
 
Tueleze kwanza jamaa kafanyeje ndo uulize sheria zinasemaje. Traffic nao ni law enforcers endapo mkosaji alifanya au kuwafanyia kitu ambacho ni ukiukwaji Wa sheria na ni jeuri, lazima nguvu itumike.
Nguvu inatumika kumkamata sio nguvu kwa maana ya kumpiga.
 
Hao jamaa kero sana..wenyewe ndiyo wakamataji wenyewe ndiyo mahakimu wenyewe ndiyo watoa adhabu...yani mtu anakukamata anakuambia umepita kwenye redi light wakati wewe kama dereva uliona njano but kutokana na situation ukashindwa kusimama..but mwisho wa siku anakuambia umepita red light..
Ilinikuta last week mnazi mmoja nafika chini ya zile taa ikawaka njano..eti nikasimamishwa pale usawa wa starlight cinema,nikamwambia nisingeweza simama pale kwa momentum ile...akabisha kabisa anataka aniandikie!
Nika brush Viatu vyake akaniachia!
 
Hivi pale CCP wanafundishwa kupiga watu ngumi? Mtu mmeshamkamata, yupo chini ya ulinzi, kwanini mnampiga? Halafu askari anavua koti ili apigane. Upumbavu gani huu?
Ndugu umekosea alietaka kumjibu au?
 
Hivi unajua mtu anayepigwa anapigwaje???

Umeshawahi kuona mtu anatandikwa wewe???

Huyo mtu amepigwa,au anavutwa vutwa shati??

Huyu hajapigwa labda hujui mtu anapigwaje???

Kitendo cha kumgusa raia ni kosa, kitendo cha kumvuta namna ile ni kosa!
Ni udhalilishaji!
WaTZ wengi mnatia huruma aisee?!
Yani kitendo hicho Wewe hujui Kama ni kosa ?
Na ndo maana wenzenu wanatumia udhaifu wenu wa kuto jitambua Kwa kuwafanyia watakavyo!
 
Sasa kule sio kupigwa,bora ungesema wamenyanyasa.
 
Katika hili sipendi kuwa ' Mnafiki ' kwa Kupepesa macho, Kutikisa masikio na Kuyamung'unya maneno kwa kusema kwamba Watumiaji wengi wa Magari wanapenda sana ' Kuwadharau ' Askari barabarani na kuna muda mwingine utakuta Mtu kabisa anatoka ' maskani ' anakuambieni kuwa leo naenda kuwazingua ' Matrafiki ' na akitiimiza hilo anarudi na kuanza kuwacheka na kuwadhihaki.

Najua kwamba wapo ' Matrafiki ' wanaozingua ila kwa jinsi hivi sasa wanavyosimamiwa vyema na Wakubwa wao na Jeshi lao na Sisi tunaopita na kukutana nao barabarani kila uchao huku tukishuhudia mengi ni dhahiri shahiri kwamba Wamiliki wengi wa Magari huwafanya vitendo vya makusudi dhidi yao na pia kumbukeni kuwa hata Wao pia ni Binadamu na wana mioyo vile vile. Tukijiheshimu na kufuata taratibu zote za matumizi ya Magari na Usalama wa Barabarani nina uhakika hizi adha / kero zitapungua kama siyo kuisha kabisa.

Kwa mfano unakuta Mtu kabisa anaona barabara imefungwa kwa muda tu ili kupisha Msafara wa Kiongozi wa Kitaifa kupita hapo halafu unaona Mtu kabisa kwa makusudi analichomeka Gari lake ' Kiubishi ' ili tu apite kwa nia ya kuiwahi huo Msafara halafu ile akitokeza tu barabarani hapo anakutaka na Pikipiki ya Polisi ya Msafara nayo ikiwa Kasi na pengine hata kuhatarisha Usalama wake na wa yule Kiongozi anayepitishwa. Hivi kwa ' scenario ' kama hii hao ' Matrafiki ' wakikupa mkong'oto wa haja utawalaumu?

Tuwe tunatafakari kabla ya kulaumu au kuwatupia Watu lawama.
Popoma katika Ubora wako
 
Ilinikuta last week mnazi mmoja nafika chini ya zile taa ikawaka njano..eti nikasimamishwa pale usawa wa starlight cinema,nikamwambia nisingeweza simama pale kwa momentum ile...akabisha kabisa anataka aniandikie!
Nika brush Viatu vyake akaniachia!
mimi amenikazia leo..wanaogopa camera
 
Kitendo cha kumgusa raia ni kosa, kitendo cha kumvuta namna ile ni kosa!
Ni udhalilishaji!
WaTZ wengi mnatia huruma aisee?!
Yani kitendo hicho Wewe hujui Kama ni kosa ?
Na ndo maana wenzenu wanatumia udhaifu wenu wa kuto jitambua Kwa kuwafanyia watakavyo!
Hujakutana nao kwenye anga zao hata uwe nani wakiamua wanakudunda tu kama ni kesi baadae na sina mfano wa kesi yyte aliyewashitaki na akashinda akafidiwa
 
Back
Top Bottom