ze big
JF-Expert Member
- Apr 27, 2015
- 382
- 350
Wiki iliyopita nilikua nikitokea maeneo ya pugu naelekea Gongo la mboto kuna mahali nilikwaa shimo barabarani kubwa kidogo likanipasulia tairi nilipobadili tairi nikaja kuhamaki mkanda wa kwenye gari yaani safety belt upande wa abiria umejikaza na kwakua sikua nimepakia mtu mwingine niliendelea na safari. kabla sijafuka gongolamboto mwisho nilikutana na askari wa usalama barabarani wakanisimamisha na nikatii. Wakaanza kukagua gari yangu yote pasipo kukuta kosa lolote wakadai niwafungulie mlango nikawafungulia wakaanza kusogeza viti na kushika hapa na pale kwenye gari wakavuta mkanda na wakakuta wa upande wa abiria umejikaza wakaniambia wananiandikia kosa la mkanda kutofanya kazi ila kwasababu hakunaga kosa kama hilo risiti ya kosa langu iliandikwa kutokufunga mkanda, JE HUU SIO UONEVU.Inakera na inaudhi kuwa wengi barabarani na kila mmoja ana EFD mashine haisaidii kujenga nidhamu. Nguvu mnayotumia kukusanya mapato kushindana na TRA haisaidiii kuweka nidhamu barabarani.
Baadhi ya sehem mmekuwa chanzo cha kero kwa kusababisha foleni zisizo za lazima na sehemu zingine mmesababisha ajali kwa sababu tu mnajisikia kusimama popote na kusimamisha gari mnalotaka.
Hebu tumieni zile ethics mnazofundishwa darasani na chuoni jamani nchi haiendi hivi. Hebu mjipange jamani sidhani kukusanya pesa kwenu ni sifa bali sifa iwe nidhamu barabarani na ajali kupungua sio mnakuwa chanzo cha kero.
Mnamo tarehe 27/02/2017 majira ya saa saba mchana nilikua nikitokea maeneo ya mwenge naelekea stendi kubwa ya mabasi ubungo kupitia sam nujoma road maeneo ya mawasiliano nilikutana na trafik police ambao walinisimamisha wakaniambia wanakagua leseni zilizo expire na vibali vingine, walinikagua na kukuta kila kitu ninacho walipoona wamekosa kila kitu wakaniambia kaka tunakuandikia kosa moja ambalo ni la over speed nikawauliza wapi nilipozidisha speed wakasema haya ni maeneo ya makazi ya watu na kwa kawaida unatakiwa utembee km 50 kwa saa na wewe umetembea 52km kwa saa wakaniandikia fine elfu thelathini. JE HII NI HAKI JE TUNAELEKEA WAPI WAPENDWA, JE DHANA YA UTII WA SHERIA BILA SHURUTI ITAWEZEKANA KATIKA JAMII YETU?