Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,376
SHERIA YA USALAMA BARABARANI:
Nimesoma kwa uzuri hii sheria ya Usalama barabarani,kama sijailewa naomba wenzangu mnisaidie kunielewesha!!
Ni wapi katika Sheria hii panapompa mamlaka askari wa usalama barabarani kumpiga faini mtu anayeendesha gari lenye Road-licence iliyoisha muda wake?
Leo asubuhi nikitoka kanisani,mmama mmoja ambaye tunasari wote ananiambia kwamba jana aliandikiwa faini na askari eti kwa kosa la kuendesha gari lenye road-licence iliyoisha muda wake wa matumizi.
Mimi nikamwambia yule mama kuwa kisheria yule askari hana mamlaka ya kumpiga ile faini,mwenye mamlaka yale kisheria ni Afisa wa TRA.
Je, nimempotosha yule mama?? Naomba wengine mnisahihishe kama nimeielewa vibaya hii Sheria ya Usalama Barabarani.
Ukiisoma kwa utulivu Sheria ya Usalama Barabarani (The Road Traffic Act),kifungu namba 40-42 na pia kifungu cha 50-51,makosa yaliyoanishwa na Sheria ya Usalama Barabarani ni haya yafuatayo:
1. Kusababisha maumivu ya mwili au kifo.
2. Kuendesha gari kwa uzembe.
3. Kuegesha gari kwa uzembe.
4. Kuendesha gari kwa mwendo kasi.
5. Kushindwa kuheshimu alama za barabarani.
6. Kuyapita magari au vyombo vingine vya moto pasipo kufuata sheria.
7. Kuendesha gari lililothibitika kuwa na makosa ya kiufundi yaliyothitishwa na Mkaguzi wa Magari (vehicle inspector).
8. Kumshawishi au kumsaidia dereva kuvunja sheria.
Sasa huyo askari aliyempiga faini huyu mamayangu muumini mwenzangu kwa kosa la kuendesha gari lenye road-licence iliyoisha muda wake ALIMPIGA HIYO FAINI KWA MAMLAKA NA SHERIA IPI?
Bado ninaamini kuwa huyo askari (traffic) alimwonea tu huyu mamayangu muumini mwenzangu. Au kama kuna mtu ameielewa vizuri hii Sheria ya Usalama Barabarani.
(The Road Traffic Act) tofauti na nilivyoielewa mimi,aje anisaidie na anisahihishe!!
Ndaga fiiijo...