Askari wa Usalama agongwa na kufariki hapo hapo Bamaga!

Ama kweli hapa ndio ujue wafanyakazi wametelekelezwa na hakuna mtu wa kuwasaidia huyo dreva aliyemgonga malipo yapo hapahapa duniani ni halali wafanyakazi wote muendelee kula rushwa itawasaidia sana yanapotokea matatizo kama haya
 
Ndugu zangu, huyu mama alitusimamisha sisi tupishe msafara, tukaipisha na yeye akakaa pembeni, ulikua msafara wa magari zaidi ya 50 na yalikua speed kubwa tuu zikiwemo na ambulance. Sasa huyu mama kosa lake pengine ni hili, Alihisi kuna watu wameunga tela msafara wa jamaa so akawasimamisha mungu saidia alisimamisha gari 2 zilizokua in a very high speed. bila ya kuangalia nyuma ya zile gari akaanza kuruhusu gari from shekilango road na hapo ndipo Discovery 4 kama sio 3 ilipofika kwenye mataa ikiwa na speed kama 120 hivi ikashindwa kusimama na kutanua ili isigongane mna magari yanayocross from shekilango. Jinsi gani ambavyo kifo kinamuita mtu mama yule alikua upande wa TBC badala ya kua upande wa sinza so jamaa alichofanya ni kukwepa madaladala hamadi traffic huyu hapa jamaa akapita. Sasa sisi tulichokua tunakiona sekunde ya kwanza ni kua jamaa kapanda ukingo ya barabara na kusepa, ila baada ya sekunde kumi niligundua kua kuna tukio zaidi ya tulichokiona nikashuka as i was walking ndio nikaona kofia ya traffic akili ikanijia sasa na wala sikutaka kwenda kuona maana wanaotazama waliniashiria kua si kitu kizuri kutazama.

Ila nimejifunza kua maisha haya jamani hatujui lini ni siku yetu, yule mama nina uhakika kabisa hakujua kama angekutwa na lililomkuta. Binafsi nimechukulia kama fundisho kwangu, sina mtazamo kama wa wachangiaji wengi wa juu yangu.

Thanx mkuu kwa taarifa.
May her soul Rest in Peace
 
Yaani so sad. nawapa pole sana familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na kifo cha marehemu. RIP dada traffic.
 
RIP & poleni sana wafiwa! Waangalie protocals za misafara hii ya rais. Tabia ya kutojali watumiaji wengine wa barabara ziangaliwe. Speed & haraka haraka zao ni za kipuuzi tu.

Ila tafadhali ondoeni hiyo picha. Inazidisha machungu
 
Serikali ya CCM inatuua kupitia vyombo vyake vya usalama, inatuua kupitia misafara, inatuua kupitia kuruhusu madawa feki ya binadamu, inatuua kupitia kutugawa kidini, inatuua kupitia kutukosesha ajira, inatuua kila mahala.

Kila mtanzania wa kipato cha kawaida kuja chini ni marehemu mtarajiwa soon!!
 
Ni hapa Bamaga,Traffic wa kike alikuwa anajaribu kusimamisha gari kumbe lilikuwa nyuma ya msafara.

Pamoja na kumgonga, msafara haukusimama
Mleta Thread please!!!.

Waambie MODs wakuwekee tahadhari kwenye kichwa cha mada.

It's so SAD na siyo UTU kuonyesha graphic photo namna hii bila tahadhari.
 
Hatarishi sana, imagine huyu ni mama wa mtu, mke wa mtu, dada wa mtu, mtoto wa mtu, and so on

Maisha yake kuishia hapa ni dhahiri kuwa system za nchi hii hazijakaa sawa.

Hivi job description ya trafiki ni kuongoza magari? Kwani taa kazi yake nini?

Kuna haja ya makusudi ya kuboresha mifumbo ya barabara ili kupunguza vifo visivyo vya lazima kama hiki

Nimeumia sana. Huzuni imenipata
 
Mara nyingi gari ya mwisho kwenye msafara huwa inakuwaga nyuma sana.

Hii hupelekea hata wale madereva wahuni kujitumbukiza halafu wanajikuta wapo kati!
 
Msafara haukusimama kutoa msaada !! ila kwenye mazishi dhaifu atajiweka kimbelembele!! Utamsikia chagonja akisema Trafiki amepigwa na kitu kizito!!
 
Hatarishi sana, imagine huyu ni mama wa mtu, mke wa mtu, dada wa mtu, mtoto wa mtu, and so on

Maisha yake kuishia hapa ni dhahiri kuwa system za nchi hii hazijakaa sawa.

Hivi job description ya trafiki ni kuongoza magari? Kwani taa kazi yake nini?

Kuna haja ya makusudi ya kuboresha mifumbo ya barabara ili kupunguza vifo visivyo vya lazima kama hiki

Mamdogo taa hazijui kama msafara unaokuja ni rais, waziri mkuu au kuna watoto wa shule wanataka kuvuka barabara.

Kuna wakati lazima mtu aingia kati aweke mambo sawa. Na hii si hapa tu
 
Ndo umesema nini hapo sasa? Aliefariki ni trafic, mwenye gari ama mpita njia?
Mara ya kwanza msafara wa rais kugonga traffic ilikuwa ni Chang'ombe mataa, enzi za mwinyi. Na hii ni mara ya pili katika historia ya nchi yetu. Msafara wa Rais unagonga trafic. How does this happen? Trafic wote si huwa wana redio za mawasiliano ili kujua msafara umefika wapi? Ni kwa vipi asimamishe gari ambalo lipo kwenye msafara?
 
Msafara haukusimama kutoa msaada !! ila kwenye mazishi dhaifu atajiweka kimbelembele!! Utamsikia chagonja akisema Trafiki amepigwa na kitu kizito!!

Na hili nalo ni kosa la JK ??? duh watu mmezidi sasa.

Wewe unaambiwa gari ya mwisho kwenye msafara imemgonga. Hata kama gari ya JK ingekuwa imegonga huyu mama unadhani ni Salama kumshusha rais wa nchi hapo shekilango? kwanza hata akishuka anafanya nini hasa? maana na yeye sio daktari. Magari yanaenda speed kubwa na hizi hatari huweza kutokea from time to time ndio maana na Ambulance ni sehemu ya msafara.
 
Kuna umuhimu wa kuendelea kuwa na picha ya marehemu ? naona kama ingeondolewa ingefaa zaidi.
 
Kwa case ya ku-clear msafara tu ni sawa

Lakini matrafiki wa nchi hii hasa Dar masaa zaidi ya 8 wanakuwa wanaongoza magari badala ya kufanya shughuli zingine

Wanakuwa exposed to risks kwa muda mrefu mno bila sababu ya msingi

Mamdogo taa hazijui kama msafara unaokuja ni rais, waziri mkuu au kuna watoto wa shule wanataka kuvuka barabara.

Kuna wakati lazima mtu aingia kati aweke mambo sawa. Na hii si hapa tu
 
Hope alishapeleka hela za unga maanawanawambia nyumban waweke maji bila kujua hela ya unga wanapata saa ngap aaa jk yulleeee anaitafta mbwen nimepshana nae naamini utakuwa msafara wake wawe na adabu sio kila gari la kusimamisha kama wanavyosimamishwa usiku counter na mabosi wao wakilewa;;yaani n aibu waone hivi ;;;;usiku wanalewa mabosi wanawaingiza vyumba vyao wasio na adabu unakuta anawashka shka live we unasubiri kumtoa mwenzio

This does not read compassionate!!
 
Mleta Thread please!!!.

Waambie MODs wakuwekee tahadhari kwenye kichwa cha mada.

It's so SAD na siyo UTU kuonyesha graphic photo namna hii bila tahadhari.

Niwape pole sana wafiwa. Kufa kupo, lakini kwa wale ambao wameshakutwa na msiba wa ghafla kama huu ngumu sana kuukubali. Mtu anatoka nyumbani salama baada ya muda unaambiwa kafa! Ni tofauti kama mtu alikuwa mgonjwa, au kogongwa na kufa baada ya siku kadhaa - pyschologically unakuwa umeshaanza kufikiria kifo.

Jambo jingine, hapa jamvini watu wameandika sana kuhusu mwendo kasi wa misafara ya viongozi wetu. Wanaendesha kwa kasi mno, na barabara zenyewe ni hizi hizi zilizojaa mashimo! Sijui ni nani aliyewaambia mwendo kasi ndio unampa kiongozi usalama? As a matter of fact, kama mtu akirusha kitu ghafla, wakati wa msafara, itakuwa vigumu kwa dereva kukwepa maana wanakimbiza sana.

Mimi nilidani njia bora ni kuwa na bullet/bomb proof car na waendeshe kwa mwendo wa kawaida. Kuna rais anayewindwa kama wa Marekani? Lakini angalia kasi ya msafara wa rais - ni kinyonga. Tutumie maarifa zaidi kuliko huu mtindo wa kizamani.

Nina hakika rais mwenyewe atafadhaika sana na huu msiba. Inahuzunisha kwa kweli. Mama wa watu katoka nyumbani salama. Poleni sana wafiwa.
 
Back
Top Bottom