Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,174
- 10,650
Maafisa wa Umoja wa Mataifa wametangaza kuwa, wameanzisha uchunguzi kuhusiana na unyanyasaji unaofanywa na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kwamba, umeanza kuzifanyia uchunguzi wa kina ripoti zinazohusiana na vitendo vya ubakaji na unyanyasi wa kingono vilivyofanywa na askari wa UN katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mwaka uliopita kulitolewa madai ya visa 69 vya ubakaji wa watoto pamoja na makosa mengine ya unyanyasaji wa kingono kutoka kwa askari hao.
Kundi moja la utetezi linasema kuwa limewasilisha ripoti mpya kwa Umoja wa Mataifa kwamba, mwanajeshi mmoja aliwalazimisha wasichana wanne kufanya ngono na mbwa.
Imeelezwa kuwa, Umoja wa Mataifa unakabiliwa na hali ngumu inayotishia kuondoa imani ya watu duniani kwa walinda amani wa umoja huo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaongoza kwenye orodha hiyo ambapo wanajeshi wa nchi hiyo wanaotumika kama walinda amani wa UN wanatuhumiwa kuhusika na visa 7 vya unyanyasaji wa kingono.
Afrika Kusini na Morocco zina kesi tatu kila moja.
Tuhuma hizo zinaonekana kuwakabili wanajeshi wa kofia za buluu kutoka nchi za Kiafrika kwani kati ya nchi 21 zinazonyooshewa kidole, zile za barani Afrika ni 17. Walinda amani wa kimataifa kutoka nchi za Ujerumani na Canada pia wanakabiliwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono.
source IRIB