Askari wa Tanzania Building Agency, Dar wailalamikia TBA kuwafanyisha kazi bila mkataba

ngaaspeter

Member
Aug 27, 2014
15
0
ASKARI WA TANZANIA BUILIDING AGENCY MKOA WA DAR WANALALAMIKIA T.B.A KUWAFANYISHA KAZI KWA MUDA MREFU BILA MKATABA WA KAZI.,WAPO ASKARI WA MIEZI 8,9,10 NA WA MWAKA MMOJA NA NUSU BILA YA KUPEWA MKATABA WA KAZI.


Rejea hotuba ya Rais JP Magufuri kuagiza kuwa usimfanyishe mtu kazi bila mkataba wa kazi.Taasisi ya serikali Tanzania bulding agency (T.B.A) mkoa wa Dar es salaam iliyoko chini ya wizara ya ujenzi imekuwa sugu kutokutoa mkataba kwa askari wake wanaolinda nyumba za serikali.

Askari hao ambao wanalalamikia uongozi huo wa (T.B.A) wa mkoa wa Dar es salaam kwa kuhujumiwa kutowapa mkataba wa kazi kwa muda wote huo,wapo askari wengi ambao wakinung`unikia chini kwa chini kwa kuhofia kufukuzwa kibarua cha kazi.

T.B.A mkoa wa Dar es salaam imekuwa ikiwalipa mshahara askari hao jumla ya Tsh.180,000 kwa mwezi ni sawa na Tsh.6000 kwa siku.

Askari hao wanafanya kazi masaa 12 bila kupewa overtime ya masaa yanayozidi.

Askari wamekuwa hawapati malipo ya ziada siku za sikukuu wakiwa kazini
Tukirudi nyuma kwa askari wa mkoa wa Dar es salaam kunaposho ya chakula Tsh.300,000 inatolewa kwa askari wote wenye mkataba na wasiyo na mkataba.

Lakini posho hiyo inawafikia baadhi ya maskari wachache na wengi wao hawaipati posho hiyo. Je, posho ya chakula ya askari wa mkoa wa Dar es salaam inakwenda wapi? Kama ipo kwa nini hawapewi?

Mpaka sasa kuna maskari wa mkataba wanadai pesa zao za malimbikizo ya mishahara yao zaidi ya miaka miwili je watalipwa lini?

TBA imekuwa ikiwacheleweshea maskari wake mishahara kitendo ambacho kinawaumiza sana wafanyakazi wake wamekuwa wakitoa mshahara tarehe 8,9,15 ya mwezi mpaka leo hii tarehe 8/12/2016 hatujapata mshahara wa mwezi wa kumi na moja.

Uwongozi huo umekuwa ukiwadhalau na kuwapuuza maskari wake hawo kwa kushindwa kuwapa vitendea kazi kama vile tochi, filimbi, buti, makoti ya mvua na silaha n.k.

Tunaomba waziri mwenyedhamana hiyo afatilie kwa kina kilio hicho cha wafanyakazi hao ambao wanafanya kazi katika mazingira magumu na kuwasikiliza kilio chao yeye mwenyewe.
 
Back
Top Bottom