askari wa T 655 AEG wanaomba rushwa 100,000! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

askari wa T 655 AEG wanaomba rushwa 100,000!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Uswe, Mar 26, 2011.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Leo nimekumbana na mkasa ulionishtua sana, nilikua maeneo ya masaki na kwa bahati mbaya (shemeji yenu ambae sasa anajifunza driving) akataka ajikumbushie yale mambo yake ya shule, tulikua very close na kiwanjapale karibu na coco beach, nami nikaona si hatari hasa ulizingatia tulikua tuko karibu sana na kile kiwanja kama mita 100 hivi, nikasimama pembeni ili tubadilishane, ile kuwasha tu gari jamaa wakiwa katika T655 AEG kumbe walikuwa wanatutazama.

  Wakatukamata na safari ya O/bay police ikawa imeanza, mmoja akashuka kutoka gari yao toyota corola ya kijivu kilichokolea imechokachoka hivi namba T 655 AEG akaja ndani ya gari yetu, njiani akaanza kumba rushwa, akasema kosa letu faini ni 180,000/= lakini yeye tumpe laki yaishe, nikaomba sana msamaha jamaa hawaelewi, tulipofika kituoni katika kuonesha jinsi anavyojua kukomoa akaongea na askari mwenzake kwamba eti najifanya mbishi, kwa hiyo nishughulikiwe. . . .mambo mengi yakatokea, nikapiga simu nyingi sana, badae kwa shingo upande wakaniacha bila kulipa hata senti moja, point yangu hapa ni JAMANI MSIKUBALI KUWAPA RUSHWA ASKARI, WANALEMAA, UWEZO WA KUFIKIRI UNAPUNGUA, WAKIONA MTU WAO AKILI ISHAFIKA KWENYE WALETI, katika hali ya kushangaza yule afande alonikamata alikuwa anasema mi ni mbishi tu ningekua kweli nataka kumaliza si ningeenda kwenye ATM kuvuta kuliko kujifanya mkorofi, yaani hawa viumbe wanadhani tunafanya kazi ili tuwape wao rushwa? na sio aibu kabisa wao kuomba rushwa. . .I am shocked!
   
 2. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu, ila ndo hali halisi tujifunze kusema hapana kwa rushwa
   
 3. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Mimi nina aleji na hao jamaa mara nyingi wakinikamata huwa nawaletea ubishi wa kweli hata kama nina kosa basi wafuate taratibu sio wao waanze kwa kuniambia tuyamalize! Ila mkuu na wewe pia ulikuwa unavunja sheria siku nyingine uwe makini kwani muda uliopoteza kwa kitendo cha leo si wa kitoto maana hawa jamaa hawana dogo! Au ulichukulia poa kwasababu sasa hivi hata wakubwa hawafati sheria ndio maana kuna mtu karuhusiwa kutibu bila kupata usajili wa kutoa tiba kama sheria inavyotaka na wakubwa wanampigia chepuo! Kuwa makini mkuu.
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Pole kwa yaliyokukuta na hongera kwa kukataa kutoa rushwa.

  Tiba
   
 5. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kuna wengine wanazunguka mitaa ya Sinza/Kijitonyama usiku wana Mark 11 nyeupe ya zamani sikumbuki namba nao ni wa Osterbay ni wasumbufu sana.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hajambo dadangu Miss Judith?
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Nikukumbushe tu,mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni =.
   
 8. U

  Uswe JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Jitahidi upate Namba zao za gari au zile namba za kwenye uniform (Mi niliangalia mabegani kwao hawakua na kitu zaidi ya neno 'POLICE) afu tubandikie hapa, walitaka eti nilale mahabusu, yes nilikosea lakini faini yake haiwezi kuwa 180,000 na sio kosa la kutulaza mahabusu, sana sana walipaswa kushika gari hadi ntapolipa faini. . . .JAMANI BORA UPOTEZE MUDA KITUONI, RUSHWA HAPANA!
   
 9. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #9
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hajambo anakusalimiia anauliza vipi biashara yako ya kusafirisha abiria kwenda kwa babu inaendelea vema?
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Mar 27, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Kuna wale wa pikipiki wanaitwa tiGO pia ni wasumbufu ile mbaya hata sijui wana majukumu gani barabarani au ni mradi wa watu ?
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  na wewe kwanini uliombaomba sana wakati unajua hata kubargain rushwa ni kosa?

  fuata sheria uepuke vivution vya rushwa
   
 12. C

  Chamkoroma Senior Member

  #12
  Mar 27, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shossi nisawa uliyosema lkn mambo ya babu yanini kuyaingiza wakati tunaongelea rushwa? Je tuseme ndiyo kutopenda huyu mzee asiwasaidie wanaopenda kuponjwa kupitia yeye?
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  sijambo mkuu,

  next qn!
   
 14. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #14
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hao wako kikundi, wame sambaa coco beach , huwa wana vizia watu wanao fanya mapenzi au wakikukamata bila chohcote wanaku bambikai bangi, mradi utoe pesa,, Huwa wana shirikiana na raisa wanao vaa nguo za kipolice
   
 15. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #15
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135


  haha, mwaka huu watu wanatengeneza hela si mchezo. 150,000/- kila kichwa si mchezo!

  kazi ipo,

  na

  Mungu yupo
   
 16. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #16
  Mar 27, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakupa Hongera ya Kutowapa hao Wezi Rushwa kama wangekuwa ni polisi wanaolipenda Taifa wasingekuomba rushwa wangekupa Onyo kama ni kosa la kwanza ukirudia tena kufanya kosa hilohilo ndio wakuzonze faini sio rushwa. Tusjifunzeni tabia hiyo watanzania ili tuweze kujenga Taifa lenye waadilifu. No Corruption, tena mkuu nakupa Hongera kwa Uzalendo uliouonyesha
   
 17. U

  Uswe JF-Expert Member

  #17
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  m
  nilikua siBargain, nilikua naomba msamaha! yes ni muhimi kufata sheria, mi ni mmoja wa watu wanaofata sana sheria, hata siku moja sitanui, sipiti red lights, na always nahakikisha nafanya service ya gari, ila kuna siku tu mtu unajikuta umepitiwa. . .so ilikua bahati mbaya sana, ila wale jamaa kuomba 100,000! dah wamezidi sana T655 AEG toyota corola sitawasahau!
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Mar 27, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sasa akili inacheza, bse gari yao ilikua private, T655 AEG TOYOTA COROLLA! inawezekana wale walikua raia
   
Loading...