Askari wa KINAPA wawadhalilisha wanawake kwa kuwapiga, kuwabaka na kuwakalisha juu ya siafu

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Serikali mkoani Kilimanjaro imeuagiza uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), kuwachukulia hatua askari wanaodaiwa kuwanyanyasa wanawake wanaoingia katika Misitu ya Nusu Maili kukata nyasi na kuokota kuni.

Mkuu wa mkoa huo, Amos Makala alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mshiri wilayani hapa.

Alisema katika ziara aliyofanya kwenye vijiji vinavyozunguka msitu huo, wanawake wamekuwa wakilalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili, ikiwamo ubakaji na kupigwa wanapokutwa na askari hao wakikata nyasi kwa ajili kulisha ng’ombe na kuokota kuni za kupikia.

“Kinapa najua wapo baadhi ya askari wenu ambao siyo waaminifu, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili na vya kinyama wanawake wanaoingia katika Msitu wa Nusu Maili. Kwa hiyo nawaagiza kuwachukulia hatua za kisheria mara moja,” alisema Makala Mkuu huyo wa mkoa alisema vitendo hivyo ni vya aibu na vya kusikitisha kwa taasisi kubwa ya umma.

“Mtu mzima hawezi kusimama kwenye hadhara ya watu wengi namna hii na kusema uongo katika mambo makubwa kama kubakwa na kutembezwa kwenye hifadhi siku nzima, kupigwa na kukalishwa kwenye siafu,” alisema Makalla.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Veronica Mlay alisema wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo siku za Jumatano na Jumamosi ambazo wameruhusiwa kukata nyasi na kuokota kuni, lakini baadhi ya askari wa Kinapa wanapowakuta huwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Kaimu mhifadhi wa hifadhi hiyo, Charles Ngendo alisema vitendo hivyo viliwahi kulalamikiwa miaka ya nyuma katika ofisi yake na kuvishughulikia.
 
“Kinapa ,, askari wenu ambao siyo waaminifu, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili na vya kinyama wanawake wanaoingia katika Msitu wa Nusu Maili. Kwa hiyo nawaagiza kuwachukulia hatua za kisheria mara moja,” al

“Mtu mzima hawezi kusimama kwenye hadhara ya watu wengi namna hii na kusema uongo katika mambo makubwa kama kubakwa na kutembezwa kwenye hifadhi siku nzima, kupigwa na kukalishwa kwenye siafu,” alisema Makalla.
Kele uu uuuwi !!!

Hili ni la UN - apparent violation of women rights, women abuse and a very serious matter. A very serious allegation, who is funding these culprints !

TAMWA mko wapi? Rush there and make deep and thorough investigation. Leave no stone un turned.

This is not high level commercial exploitation of the resource. Removal of head loads of grass and dead wood or debris for domestic use will not lead into quick degradation of the ecosystem. Use Kyoto approach, Climate change is doing much harm than your good neighbours. High rainfall in the area means fast regeneration of grass and other plants. KINAPA!! Stop classical and un human approach in your conservation methods. Be People focused! Apply software and not cohesive approach
 
Serikali mkoani Kilimanjaro imeuagiza uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (Kinapa), kuwachukulia hatua askari wanaodaiwa kuwanyanyasa wanawake wanaoingia katika Misitu ya Nusu Maili kukata nyasi na kuokota kuni.

Mkuu wa mkoa huo, Amos Makala alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mshiri wilayani hapa.

Alisema katika ziara aliyofanya kwenye vijiji vinavyozunguka msitu huo, wanawake wamekuwa wakilalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili, ikiwamo ubakaji na kupigwa wanapokutwa na askari hao wakikata nyasi kwa ajili kulisha ng’ombe na kuokota kuni za kupikia.

“Kinapa najua wapo baadhi ya askari wenu ambao siyo waaminifu, wamekuwa wakiwafanyia vitendo vya kikatili na vya kinyama wanawake wanaoingia katika Msitu wa Nusu Maili. Kwa hiyo nawaagiza kuwachukulia hatua za kisheria mara moja,” alisema Makala Mkuu huyo wa mkoa alisema vitendo hivyo ni vya aibu na vya kusikitisha kwa taasisi kubwa ya umma.

“Mtu mzima hawezi kusimama kwenye hadhara ya watu wengi namna hii na kusema uongo katika mambo makubwa kama kubakwa na kutembezwa kwenye hifadhi siku nzima, kupigwa na kukalishwa kwenye siafu,” alisema Makalla.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Veronica Mlay alisema wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo siku za Jumatano na Jumamosi ambazo wameruhusiwa kukata nyasi na kuokota kuni, lakini baadhi ya askari wa Kinapa wanapowakuta huwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Kaimu mhifadhi wa hifadhi hiyo, Charles Ngendo alisema vitendo hivyo viliwahi kulalamikiwa miaka ya nyuma katika ofisi yake na kuvishughulikia.
Mkuu chachu ombara naamini wewe ni mwana ccm mzuri na mtiifu ambaye unaweza ukatoa ushauri ukafika sehemu husika, ebu mshauri magu awatimue hao askari na kamanda wao wenye roho za kinyama namna hiyo pls
 
Sijui Tumewakosea nini makabila hadi tuchukiwe na kuonewa katika nch na ardhi yetu watu wa kaskazin?
 
Back
Top Bottom