Askari wa jwtz walioua wanafikishwa lini mahakamani?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wa jwtz walioua wanafikishwa lini mahakamani??

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jan 26, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,249
  Likes Received: 5,630
  Trophy Points: 280
  TUMECHOKA NASEMA TUMECHOKA NADHANI IFIKE WAKATI MTANZANIA ANAITAJI KUJILINDA MWENYEWE HATA KWA SILAHA YOYOTE
  BAADA YA KUSIKIA POLISI WAKIUA WATU UKEREWE,WANAJESHI WAKIUA WATU ARUSHA HAKUNA KINACHOENDELEA NDUGU ZANGUNI KUNA HILI LA HUYU BWANA ALIEUWA MWANANYAMALA NA ASKARI WA JWTZ MTU NA MKEWE JE WANAFIKISHWA LINI TUMEKUWA TUKISIKIA WANAPELEKWA MAAHAKAAMA YA KIJESHI MARA WAKOO HUUURU TUNAITAJI HAKI
  TUMECHOKA

  Marehemu Fundikira kuzikwa leo  na Betty Kangonga
  ALIYEWAHI kuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Kata ya Mwananyamala, Swetu Fundikira (45) ambaye aliuawa juzi kwa kipigo kutoka kwa askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), anatarajiwa kuzikwa leo baada ya kukamilika ripoti ya uchunguzi.

  Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, kaka mkubwa wa marehemu, Ismail Fundikira alisema kutokana na kifo hicho cha ghafla waliamua kulihusisha Jeshi la Polisi kwa ajili ya kubaini chanzo baada ya kudaiwa ndugu yao kupigwa na askari wa JWTZ.

  Alisema utaratibu wa kuuchunguza mwili huo umekwishakamilika ambapo madaktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndio wameongoza uchunguzi huo wakiwa na askari polisi pamoja na wanafamilia watatu.

  “Kwa kweli hapa tulipo tunasubiri uchunguzi wa daktari ili kubaini kilichomkuta ndugu yetu, na tunashukuru ndugu watatu tumehusishwa wakati wa kuchunguza mwili huo,” alisema Ismail.

  Alisema marehemu ni mtoto wa nane katika familia ya mzee Ramadhan Fundikira, nduguye marehemu Chifu Abdallah Fundikira, aliyewahi kuwa mwanasiasa mkongwe nchini. Ameacha mke na watoto wawili.

  Fundikira alifariki juzi kwa kile kilichoelezwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwa alipigwa na askari wa JWTZ kikosi cha Lugalo Dar es Salaam. Askari hao ni Sajenti Rhoda Robert na mumewe Koplo Ali Ngumbe. Wote wanashikiliwa na polisi.
   
Loading...