GHOST RYDER
JF-Expert Member
- Jun 10, 2011
- 1,025
- 475
Katika kile kinachoonekana kama kuhitimisha kwa mbwembwe Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Hussein Mwinyi, chanzo chetu cha uhakika kutoka jijini mwanza kinaarifu askari ya jeshi la Polisi na na wale wa Jeshi la wananchi Tanzania kuchapana kavukavu katika eneo la Kituo cha polisi kilichopo eneo la kiwanda cha nguo Mwatex jijini humo.
Chanzo cha mkasa huu inadaiwa kuwa ni askari wa jeshi la polisi kumkamata mwananchi aliyekuwa amevalia sare za kiraia na kofia ya kombati za jeshio kichwani.
Bila kutambua kuwa raia huyo hakuwa raia wa kawaida bali askari wa jeshi la Polisi, walimtia nguvuni. Katika zoezi la mahojiano alionekana kukaidi maswali ya polisi na kutojitambulisha yeye ni nani ndipo Polisi wakachukua uamuzi wa kumsweka lupango huku wakijisahau kumfanyia upekuzi.
Kosa hilo lilimpa mwanya kutumia simu yake ya kiganjani aliyoswekwa nayo lockup kuwasiliana na wanaJWTZ wenzake ambao bila kupoteza muda walifika katika eneo la tukio na kutifua vumbi la kipekee huku wakifanikiwa kumnasaua mtuhumiwa kutoka lupango.
Katika kujibu mapigo Polisi nao walimimina Defender mbili za FFU na kufungua mapigano makali kati ya Askari wa Polisi na JWTZ huku umati wa wananchi ukiungana na wanaJWTZ wachache kuwakabili Polisi.
Hata hivyo kadhia hiyo ilitulizwa baada ya kuwasili kwa maofisa wawili kutoka pande mbili husika na kuwatawanya vijana wao kwa amri za kiafande.
Ni bahati mbaya jana media zilifunikwa na Taarifa za Rostam kuvua gamba na hata wadau wetu kutoka huko walifunikwa na wingu hilo.
Tunaendelea kusaka picha za majeruhi na bila shaka kudadidi kama Polisi leo huko Mwanza watatoa tamko lolote kufuatia tukio hulo ambalo kwa namna ya kipekee lilihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Hussein Mwinyi hapo jana.
More updates to follow
ADIOS