Askari wa JWTZ agonga basi la mwendokasi na kulitelekeza gari na kukimbia

Uongo MP sio traffic, majukumu ya police ctraffic yapo pale pale. MP hutumika kwa ajili ya escort. Ila kama kuna msongamano barabarani badi MP husaidia mamlaka za kiraia (Police)
Tusubiri mrejesho kama gari hilo litapelekwa kituo cha Polisi au jeshini.Na ni nani ataye kwenda kulitoa. Wao wana husika na masuala ya nidhamu jeshini pia, sio escot tu.
 
Hawa wanajidaiga wababe na wako juu ya sheria.Njia imewekwa rasmi ya mwendokasi wewe unaingiza gari lako la jeshi sijui la wokovu au.Huu sio utu kabisa maana amehatarisha maisha ya wananchi ambao kimsingi ni watu anaopaswa kuwalinda
Inategemeana lilikuwa limebeba nn na linakwenda wapi
 
Tusubiri mrejesho kama gari hilo litapelekwa kituo cha Polisi au jeshini.Na ni nani ataye kwenda kulitoa. Wao wana husika na masuala ya nidhamu jeshini pia, sio escot tu.
Naelewa zaidi ya ujuavyo wewe, sheria za nchi ziko pale pale, gari litakwenda kituo cha polisi na hao Mp watafatilia mchoro wa ajali kwa polisi, kisha ndio gari litachukuliwa huko jeshini. Kuwa na akili
 
Kama ni hivyo hata ambulance pengine wanawahi michepuko.gari ilikua ya kazini means jamaa alikua kazini acha fikra potofu kwa jeshi lako[/QUOTE

Acha ufala badi. Sherua zifuatwr na kila mtu usichukulie mazoea kiazi wewe
 
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amegonga basi la mwendokasi na kusababisha madhara kwa abiria na basi, huku akikimbia na kutelekeza gari alilokuwa akiliendesha.

Tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam, baada ya dereva wa gari hilo kuingia kwenye barabara ya mwendokasi kisha kugongana na basi lililokuwa na abiria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataka madereva wote bila kujali ni taasisi gani kufuata sheria za nchi na kuacha kutumia mabavu.

Mambosasa alisema dereva huyo alifanya makosa kwa kuingia njia ya mabasi yaendayo kasi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria.

"Huyu dereva ana makosa, kwanza alishindwa kuheshimu taa zinazoongoza magari na hairuhusiwi kupita katika njia hizo za mwendokasi. Baada ya kusababisha ajali hiyo, alilitelekeza gari na kukimbia", alisema Mambosasa.

"Namba za gari la jeshi (JWTZ) kwa sasa sizikumbuki kwa kuwa nimetoka ofisini nashughulika na masuala ya mafuriko".

Kuhusu madhara ya ajali hiyo, alisema watu wachache waliumia na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na baadaye kuruhusiwa.

Mambosasa alisisitiza kuwa madereva wa majeshi wanatakiwa kufuata sheria za nchi bila kutumia mabavu ama cheo.

"Nilishasema hakuna ambaye yuko juu ya sheria. Ni vizuri hao madereva wa Jeshi wakafuata sheria za barabarani na hairuhusiwi kutanua kwenye barabara ambayo si njia yako", alisema Kamanda Mambosasa.

Aidha, alisema kuna magari ambayo ni dharura yaliyoruhusiwa kupita kwenye njia ambayo si yake kinyume cha hapo, mengine yote yanatakiwa kufuata sheria zilizopo.

Gazeti hili lilishuhudia gari ya Jeshi ikipita katika njia ambayo si yake katika eneo la Riverside Ubungo na kumgonga mwendesha bodaboda ambaye alikuwa kwenye njia yake.

Chanzo: Nipashe
Sijaona popote Mwambosasa akiahidi atamtafuta huyo askar
 
sawa mkuu ila unaonekana wewe ni class mate wa bashite
Wewe ndiyo unaonyesha ubashite wako hapa, eti hawalali kulinda watu! Hebu tuambie hawalali kulinda watu dhidi ya nani?

Nyinyi mbona mnapenda kuwashushia heshima polisi?
Japo siwapendi kabisa CCM lakini nakiri huwa naona polisi wanapiga doria mitaani kulinda watu wa kawaida kabisa na mpaka wakati mwingine wanauwawa wenyewe.

Hao wengine naona kama vile kazi yao kubwa ni kuulinda utawala.
 
Umuhimu wao tauona mbaka vita itokee ila kwa saiv inchi ipo salama, anatulinda mungu tu. Not them.
Kwahiyo unashauri vipi, waachishwe kazi wote kwa vile umuhimu wao kwasasa haupo? Kisha ile mipaka utakwenda kuilinda wewe? Umemaliza shule lini? Na kidato cha ngapi?
 
Wewe ndiyo unaonyesha ubashite wako hapa, eti hawalali kulinda watu! Hebu tuambie hawalali kulinda watu dhidi ya nani?

Nyinyi mbona mnapenda kuwashushia heshima polisi?
Japo siwapendi kabisa CCM lakini nakiri huwa naona polisi wanapiga doria mitaani kulinda watu wa kawaida kabisa na mpaka wakati mwingine wanauwawa wenyewe.

Hao wengine naona kama vile kazi yao kubwa ni kuulinda utawala.
mkuu umepiga viroba kule mpakani nani analinda. doria za baharini nani anafanya kuna vikosi vya rada zanzibar nani anafanya, sema we poyoyo nisije kutoa siri za nchi hapa
 
Back
Top Bottom