Askari wa JWTZ agonga basi la mwendokasi na kulitelekeza gari na kukimbia

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), amegonga basi la mwendokasi na kusababisha madhara kwa abiria na basi, huku akikimbia na kutelekeza gari alilokuwa akiliendesha.

Tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Magomeni jijini Dar es salaam, baada ya dereva wa gari hilo kuingia kwenye barabara ya mwendokasi kisha kugongana na basi lililokuwa na abiria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku akiwataka madereva wote bila kujali ni taasisi gani kufuata sheria za nchi na kuacha kutumia mabavu.

Mambosasa alisema dereva huyo alifanya makosa kwa kuingia njia ya mabasi yaendayo kasi huku akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kinyume cha sheria.

"Huyu dereva ana makosa, kwanza alishindwa kuheshimu taa zinazoongoza magari na hairuhusiwi kupita katika njia hizo za mwendokasi. Baada ya kusababisha ajali hiyo, alilitelekeza gari na kukimbia", alisema Mambosasa.

"Namba za gari la jeshi (JWTZ) kwa sasa sizikumbuki kwa kuwa nimetoka ofisini nashughulika na masuala ya mafuriko".

Kuhusu madhara ya ajali hiyo, alisema watu wachache waliumia na kupelekwa hospitalini kwa ajili ya matibabu na baadaye kuruhusiwa.

Mambosasa alisisitiza kuwa madereva wa majeshi wanatakiwa kufuata sheria za nchi bila kutumia mabavu ama cheo.

"Nilishasema hakuna ambaye yuko juu ya sheria. Ni vizuri hao madereva wa Jeshi wakafuata sheria za barabarani na hairuhusiwi kutanua kwenye barabara ambayo si njia yako", alisema Kamanda Mambosasa.

Aidha, alisema kuna magari ambayo ni dharura yaliyoruhusiwa kupita kwenye njia ambayo si yake kinyume cha hapo, mengine yote yanatakiwa kufuata sheria zilizopo.

Gazeti hili lilishuhudia gari ya Jeshi ikipita katika njia ambayo si yake katika eneo la Riverside Ubungo na kumgonga mwendesha bodaboda ambaye alikuwa kwenye njia yake.

Chanzo: Nipashe
 
Ingekuwa kihalali angetelekeza Gari?
Umeambiwa aliacha gari ameondoka unajua aliwahi wapi ,na kama angechelewa nini kingetokea.unahisi wanajeshi wapowapo tu wanasubiri mishahara tu.unajuaje kama ndio mwenye dhamana ya ghala la silaha na alikua anawahi nini kisitokee ndo mana akapita njia ya mwendo kasi.mbona magari mengine hayapiti njia hyo .
 
Hatuna crisis, ukiangalia mara kwa mara magari ya jeshi huwa hayafuati sheria za barabarani magari yao yanatakiwa yakae kambini tu uraiani yanafuata nini? Siku hizi hakuna movement order?
Yakae kambini tu,halafu movement za kijeshi watumie daladala au vp mkuu
 
Gari ni ya jeshi sio binafsi.unajua alikua anawahi nini kwa maslahi ya taifa.
Unadhani abiria wa mwendo kasi walikuwa sungura wale?Kila mtu anawah anakowahi kwa maslah yake na ya taifa.
Ni kwamba madereva wa majeshi iwe polisi au JWTZ huwa wana vunja sana sheria,sasa huko alikokuwa anawah amefika?Kam kwa maslah ya taifa mbona maekimbia?
 
Umeambiwa aliacha gari ameondoka unajua aliwahi wapi ,na kama angechelewa nini kingetokea.unahisi wanajeshi wapowapo tu wanasubiri mishahara tu.unajuaje kama ndio mwenye dhamana ya ghala la silaha na alikua anawahi nini kisitokee ndo mana akapita njia ya mwendo kasi.mbona magari mengine hayapiti njia hyo .
Mshahara haubebwi kwenye basi la jeshi.
Kumbe hujawah hata kuona mishahara yao wanavyoisafirisha
 
Back
Top Bottom