Waheshimiwa mawaziri wa wizara husika [UCHUKUZI NA MAMBO YA NDANI] tunawaomba mtuokowe, Mvutano uliyopo kati ya ofisi ya kamshina wa zimamoto na mkurugenzi wa mamlaka ya viwanja vya ndege unatufanya tushindwe kufanya kazi katika hari ya ufanisi, kutokana na mambo mengi kuzolota kiutendaji. Kuna uduma ambazo tulikuwa tunazipata kutoka mamlaka ya viwanja ndege, lakini kamishina alizifuta huduma izo kwa madai kuwa atazitowa yeye lakini mpaka leo hakuna kinachoendelea juu ya uduma izo. Cha kusikitisha tangu tuhamishiwe ofisi ya kamishina hatujawai kulipwa pesa ya likizo lakini askari wenzetu wa manispaa wamekuwa wakilipwa pesa za likizo kutoka ofisi ya kamishina, hari hii inatuvunja nguvu kabisa ikizingatia sote tupo idara moja lakini sisi tunabaguliwa. Pia tangu mwezi wa tatu mwaka huu hatujawai kukatwa pesa kwa ajili ya kuchangia mifuko ifadhi za jamii [PSPF] tumekuwa tukipeleka malalamiko yetu ofisi ya kamishina bila kufanyiwa kazi. Hari hii imepelekea tushindwe kukopa pesa katika taasisi za fedha kwa kwasababu hatutambuliki, lakini askari wenzetu wa manispaa wanatambulika na mikopo wanachukuwa kwani wao wamekuwa wakichangia mifuko izo. Hari hii inaonesha jinsi gani ofisi ya kamishina ahitusamini kabisa sisi askari wa viwanja vya ndege, vitendea kazi vyenyewe vimekuwa vinatolewa kwa ubaguzi, hakuna hata siku moja tuliwai kupata hata unifom wala zana za kazi kutoka kwa kamishina lakini askari wenzetu miji wamekuwa wakipewa kutoka kwa kamishina. Hatujui sisi tupo wapi kiutendaji, WAHESHIMIWA MAWAZIRI TUNAOMBA SANA UTUNUSURU KWANI ASKARI TUNA HARI MBAYA SANA NA TUNAOMBA MTUTEMBELEE VIWANJANI TUNA KERO NYINGI SANA TENA SANA