Askari wa jeshi la Magereza wanatia huruma, Serikali sukeni upya hili jeshi

5997

JF-Expert Member
Jan 19, 2019
514
1,204
Aisee,

Jeshi la Magereza limekua kama vile limesahaulika sijui ni kwa sababu zipi,

Askari Magereza huku mtaani wamechokachoka hadi huruma, hali ngumu uniform zenyewe baadhi wanavaa sare zimeisha zimechakaa

Mpaka makampuni binafsi ya ulinzi wanavaa sare nzuri lakini hawa wenzetu unakuta askari kavaa sare imepauka hadi kero,

Mbona majeshi mengine mnayajali sana?
Angalia JWTZ askari wake wanamelemeta na sare zao za mabakamabaka zinavutia

POLISI askari wake wanameremeta na sare zao za kaki zinavutia,

Lakini magereza kwanza sare zao hazivutii kabisa, sare gani zinafanana udongo? halafu zikipauka sasa ndo hazitamaniki kabisa,

Juzi nilikua sehemu nikawaonsa na maafisa wa jeshi la magereza wapo kama kumi na kitu wote wana nyota, yaaani hawavutii kabisa
Si wakiume wala wakike hawavutii

Sasa serikali fanyeni hima angalau muwabadilishie hizi sare hata muwape rangi nzuri

Huu ni uonevu yaani ukiwaona unaweza kutoa machozi
 
5997,
ndugu yngu taasisi zote za usalama serikalini haziwezi kufanana ingawa zinafanya majukumu yanayolingana au kukaribiana kufanana hata kwenye familia kuna watoto pedwa na wale ambao wapo tu ndo maisha hayo..
 
Sio kweli kwamba hawapendezi, wanapendeza mno tatizo ni mgawo wa uniform unaweza kufanyika kwa miaka minne mara moja.
Na wengi wanajiongeza kwa kushonesha mitaani.
.
Pia usisahau kazi zao nyingi wanafanya juani hivyo kupauka mgongoni na suruali makalioni hilo sio la kushangaza hasa kwa wale wa magereza yenye kilimo.
Ila wa town wako vizuri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom