Askari wa Hifadhi ya Rubondo wadaiwa kuzamisha wavuvi sita ziwani

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Jun 22, 2011
4,225
869
Askari wa hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo iliyopo wilayani Geita wanadaiwa kuwapiga risasi wavui wawili na kuwavunja magoti mmoja amelazwa kwenye hospiali ya wilaya ya geita na tayari alikuwa ameanza kuoza majeraha,mwenzake yuko mahabusu na hapati matibabu.

Hata hivyo inaaiwa kwamba askari hao walizamisha mtumbwi uliokuwa umewabeba wavuvi hao wapatao wanane ambapo wamezama na kufa!kun madai kwamba askari wa hifadhi hiyo wakiongozwa na mkuu wa doria wa hifadhi hiyo Fredrick chuwa wamekwa wakiwafanyia ukatili wavuvi wanaowakamata wakivua samaki ndani ya hifadhi kwa kuwapida,kuwalazimisha kutafuna kokoto na adabu nyingine.

Mkuu wa mkoa anadaiwa kufumbia macho vitendo hivyo.
 
Wabhejasana nadhani hufahamu nini kinaendelea, hao unaowaita wavuvi ndio hao hao wanaoingia hifadhini nakupiga Tembo. Mimi nimekaa kwenye hiyo hifadhi kwa muda wa miezi sita kama mtafiti ninamfahamu Chuwa uliyemtaja, sio kwa kwa jina bali kwa kazi anazofanya ni mtu aliyejitolea kupambana na ujangili akihatarisha hata maisha yake wakati mwingine mpaka kupewa ufanya kazi bora wakati flan, sio yeye tu hata wafanyakazi wengine wanafanya kazi kubwa sana kuzuia ujangili kwenye ile hifadhi bwana Kelvin mtu wa utalii Kibasa muekologia na wengineo. Kuna mwaka hao hao unaoita wavuvi walimzamisha accountant akafa bado utasema ni wavuvi wenye nia nzuri?acha kuchukua maneno ya upande mmoja tu na kugeneralize.Nasubiri ujibu.
 
Kwanza sijachukua maneno ya upande mmoja!

Bahati mbaya ni kwamba tunatumia Nick Name!

Pole sana niambie pengine unataka nini hasa nikupe?

Labda kwa kukusaidia tu ni kwamba Katika hifadhi ya Taifa ya Rubondo amewahi kuuawa Tembo mmoja tu na waliohusika ni wao wenyewe na hasa huyo Chuwa,na walichokifanya waliamua kumteketeza ka petroli!

Turudi kwenye hoja ya msingi hata kama wangekuwa wameingia hifadhini na wakakamatwa hakukuwa na sababu za msingi za kuwapiga risasi na kuwavunja miguu sheria ziko wazi sana na isitoshe ni faini tena 30000 kwa hiyo walipasawa kufuata utaratibu huo huo.

Naomba kwaa sasa niishie hapa!!
 
Back
Top Bottom