Askari wa FFU Amuua Mkewe Kwa Kwenda Baa Bila Idhini Yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari wa FFU Amuua Mkewe Kwa Kwenda Baa Bila Idhini Yake

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Sep 1, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,608
  Trophy Points: 280
  Askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) mkoani Mwanza, F 7015 PC Emmanuel (26) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumshambulia kwa kitu chenye ncha kali hadi kupoteza maisha. Askari huyo alimuuwa mkewe aitwae Hellen aliyekuwa na umri wa miaka 24.

  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Elias Kalinga alisema jana kuwa mtuhumiwa huyo anadaiwa kumuua mkewe huyo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kumpiga nyumbani kwao katika kambi ya polisi iliyopo Mabatini.

  Kalinga, alisema mtuhumiwa huyo alimshambulia mkewe kwa kumpiga kwa kitu chenye ncha kali kichwani na mgongoni na kufia njiani wakati akikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya Bugando.

  Alisema uchunguzi umebaini kuwa kifo hicho kilisababishwa na mke wa mtuhumiwa huyo kupoteza damu nyingi sana.

  Alisema chanzo cha mauaji hayo ni mke huyo kwenda kunywa pombe na marafiki zake wawili bila idhini ya mumewe na mumewe huyo kumkuta hayupo nyumbani baada ya kurudi majira ya saa tatu za usiku.

  Alisema mtuhumiwa huyo kwanza atafikishwa katika mahakama ya kijeshi na endapo ushahidi ukikidhi atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya mauaji ya mkewe.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2964302&&Cat=1
   
Loading...