Salamu wandugu,
Kwanza ni wapongeze Askari wa barabarani kwa kazi kubwa wanayofanya usiku na mchana.
Hoja yangu ni juu ya operation mnazofanya barabarani zimekuwa na usumbufu na kero kubwa yaani, ukamataji magari hata kama huna kosa wanatafuta makosa kwa lazima
Napenda kuwashauri askari wa barabarani ni kweli mnafanya kazi nzuri ila tunawaomba mtende haki msilazimishe makosa sisi ni watanzania wenzeni hatuna mashamba ya hela tunayovuna ili kulipa hizo faini. Wengine wanaandika faini kimyamya unashangaa unakamatwa eti unadaiwa hata ulipofanya kosa hujui.
Jamani muwe na utu mnatutesa na kufanya tuwachukie kiukweli watu wanachukia sana hayo mnayofanya barabarani kama mtu hana kosa muache sio kulazimisha makosa na makosa mengine ni kumuonya mtu sio lazima upige faini mnaumiza watanzani bure na kujijengea chuki. Tambueni nyie ni sehemu ya jamii msijenge uadui na raia kwa kuwabambikia makosa
Imefikia hatua tunaogopa kuendesha gari siku za Jumamosi na Jumapili kwa sababu ya nyakua nyakua kila kona kiukweli mnapata hela kupitia hizo faini ila mnaacha majeraha mioyoni mwa watu.
Kwa hiyo nawashauri mtende haki si vinginevyo kama kosa la faini mwandikie lakini kama hamna kosa mwache dereva sio kulazimisha hata hivyo makosa mengine mnaweza shauri mtu cha kufanya sio kumuandikia faini