Wakuu nimeona nilete hili kwenu na kwa kamanda Mpinga pia. Kwa wale ambao wameshasafiri na magari yao private watakuwa wamekumbana na hii kadhia kama ilivyonikuta mimi. iko hivi. Nimetoka moro kufika mbele ya kingolwila askari mwanamke akanisimamisha nime overspeed. Nilipenda kuona record kwenye tochi maana nilikuwa na uhakika nilikuwa naendesha chini ya km 50 kwa saa.
Cha kustaajabisha askari huyo jina na namba yake(kapuni) alijibu kwa keuri 'askari mwenye tochi yuko huko nyuma mumeshampita tayari' kwa kweli ilinistaajibisha. Tulirudi km 2 na kumkuta jamaa kavaa kiraia yuko ndani ya gari ndogo kajibanza porini ana tochi.
Tulipo lipia faini tukaambiwa risiti tukachukie ofisini yaani turudi nyuma zaidi mpaka kingolwila.Hii ni adha kubwa ukizingatia kwamba tulitakiwa kuendelea na safari yetu kama tulivyopanga. wadau je hii ni sawa? Kamanda Mpinga hivi ndivyo tunavyofanya kazi ktk serikali ya awamu ya 5?iliyodhamiria kupunguza kero kwa wananchi na kufanya kazi kwa ubunifu ?
Kwa nini askari mwenye tochi na askari wengine wenye kitabu cha faini wasikae pamoja?je imeshindikana kabisa kuwa na kitabu cha risiti ili mtu anapolipia faini tupate uhakika pesa inaenda kunakostahili?
Hii haiko sawa!