Askari shujaa aliyemuokoa mtoto aliyetumbukia chooni aitwa kwa Waziri Simbachawene

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,204
4,694
Karagwe. Askari wa jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Koplo Denis Minja ambaye alimuokoa mtoto juzi kwenye choo amesema amepokea pongezi kwa kitendo cha uokoaji.

Akizungumza na Mwananchi Digital amesema tayari amepokea barua ya pongezi hizo kutoka mamlaka zilizo juu yake.

Koplo Denis Minja pia amesema kuna wito wa Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ya kumtaka kuripoti wizarani ili kumuona yeye na ampongeze kwa ushujaa wake.

Alisema Waziri Simbachawene alieleza kuwa pamoja na kuwa wakubwa wake wa kazi wameshampongeza lakini naye anataka aende Wizara ya Mambo ya Ndani ili aweze kukutana naye.

Mbali na pongezi hizo kwa Koplo Denis Minja wenzake alioshirikiana naye katika kuokoa mtoto Anekius Evance pia wamepokea barua ya pongezi kutoka kwa Kamishina Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania, John Masunga.

Chanzo: MCL
 
Jamaa amezama chooni kwa uokozi bila PPE amezama na Magwanda,uso uko wazi,kichwani wazi,angeweza kugongwa na Nyoka shimoni
Simbachawene usiishie kumuita na Kumpongeza Koplo Denis, Muda sasa Nunulia Zimamoto vifaa.

Denis alitakiwa kuingia Shimoni kule na PPE, Mwili umekuwa covered fullly.
 
See the difference kati ya Rescue Brigade wenzetu na kwetu
casestudy-img03.jpg
 
Back
Top Bottom