Polisi Arusha watimua Askari watatu kwa utovu wa nidhamu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,357
8,064
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.

Aidha, limewatahadharisha wengine wenye tabia kama hizo kuziacha.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alipokuwa akizungumza na Mwananchi Digital ofisini kwake.

Kamanda Masejo amesema askari hao kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya jeshi la polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi.

"Hao askari tumewaondoa katika jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na jeshi hilo,” amesema Kamanda Masejo

"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.

Mwananchi

Pia soma: Vigogo wa Polisi Arusha wadaiwa kumpora mfanyabiashara milioni 3, watupwa lokapu
 
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha,Kamishina Msaidizi,Justine Msejo alsema kuwa jeshi hilo limewafukuza kazi askari kwa fedheha askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo katika tukio ambalo hakuwa wazi.

Msejo akiongea ofisini kwake aliwatahadharisha askari polisi Mkoani Arusha wanaoenda kinyume na maadili yao kuwa yatawakuta haya yaliyowakuta wenzao.

Aliwataka kufanya kazi kwa kufuata msingi ya kazi ikienda sambamba na weledi wa kazi na wenye tabia ya kukiuka misingi ya kazi sheria ipo na hawatahurumiwa na mkono wa sheria utawakuta dhidi yao.

Alisema askari hao watatu kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya jeshi la polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi hivyo hawatoshi kuwa katika jeshi hilo.

"Hao askari tumewaondoa katika jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na jeshi hilo,” alisema Masejo

"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema

Kamanda huyo alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi majina ya polisi waliofukuzwa katika jeshi hilo kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.

Katika siku za Karibu Mkoani Arusha kulitokea matukio mawili ya Polisi kuomba rushwa moja likiwa la Kwa Mrombo Jijini Arusha la askari watatu kuomba rushwa ya shilingi milioni 3 na kurudisha shilingi milioni 2.5 na lingine likihusisha askari wanne wa Kituo cha Polisi Ngaramtoni kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 6 na baadae kurudisha ofisini kwa Kamanda Masejo.

Katika tukio la kwanza askari walihusika ni pamoja na Maofisa Wakaguzi Wasaidizi Watatu wa Polisi Arusha akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi Engutoto ,Mkaguzi Msaidizi Mahamud Jakaya kwa kosa la kupora zaidi ya shilingi mlioni 3 za Mfanyabiashara wa Mazao, Ramadhani Hamisi kutoka Mkoani Dodoma aliyedaiwa kufanya biashara ya Mirungi.

Wengine waliohusika katika tukio hilo ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi ,Ramadhani Mcheka na Mkaguzi Msaidizi aliyetambulika kwa jina moja la Machanganya ambao wote wawili ni askari viongozi kitengo cha Polisi Jamii katika wilaya ya Arusha.

Tukio la pili lilihusisha askari wanne wa Kituo cha Polisi Ngaramtoni ambapo walikiri kupokea shilingi milioni 6 mbele ya Kamanda Msejo kutoka kwa mfanyabiashara mwenye asili ya Kisomali aliyedaiwa kusafirisha dola zenye thamani ya shilingi bilioni Moja kutoka Namanga kwenda Jijini Arusha.

Matukio yote hayo Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha amekuwa mgumu kuyatolea maelezo pindi anapohitajika na kueleza kuwa yanachunguzwa na kwenda mbali zaidi kusaka askari polisi wanatoa taarifa za matukio hayo kwa waandishi wa habari.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.

Aidha, limewatahadharisha wengine wenye tabia kama hizo kuziacha.

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alipokuwa akizungumza na Mwananchi Digital ofisini kwake.

Kamanda Masejo amesema askari hao kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya jeshi la polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi.

"Hao askari tumewaondoa katika jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na jeshi hilo,” amesema Kamanda Masejo

"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.

Mwananchi
Nanukuu

"Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea..." mwisho wa kunukuu
 
Mahindi- kaka yake ni polisi central-elfu 30 ya mafuta ya pikipiki- inspectors 3- mil 3 nayo ikapokwa na kuwa jumla ya Tsh.3.3mil-akaambiwa amwambie askari mwenzao kuwa kawapa 1mil tu.
Ha ha ha Mkuu codes zimeeleweka....
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya jeshi hilo.

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.
Polisi bado akili zenu zina matatizo mengi tu, pamoja na kuwa na IGP mpya. Kama unasema upelelezi unaendelea, kwa nini uwafukuze kazi?

Na kutowataja majina kwa kuwa upelelezi unaendelea kutafuta polisi wengine, ina maana hao polisi wengine hawawajui wenzao waliofukuzwa kazi?

Na kama mna sababu ya kuwafukuza mliowafukuza, kwa nini hamjawafikisha sehemu husika kama mnavyotaka kuwafanyia hao wengine mnaowatafuta?

Yaani mnajichanganya sijui hata hilo gwaride mnawezaje kupiga!

Hivi nyie Polisi mlisoma shule zipi, hizi hizi tulizosoma sisi? Haiwezekani.
 
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limewafukuza kazi askari wake watatu kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo ikiwemo ukosefu wa nidhamu kazini, huku likiwatahadharisha wengine wenye tabia kama hizo kuziacha."

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani humo, Justine Masejo, wakati akizungumzo na chombo kimoja cha habari ofisini kwake.

Kamanda Masejo amesema askari hao kwa nyakati tofauti wamebainika kwenda kinyume na maadili ya kazi ya Jeshi la Polisi ikiwemo kushindwa kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu katika utendaji kazi.

"Hao askari tumewaondoa katika Jeshi letu na tutaendelea kufuatilia na wengine watakaoshindwa kufanya kazi kwa uadilifu, kulingana na kiapo walichokikubali wakati wanajiunga na Jeshi hilo,”

"Niwatake askari wengine wenye tabia kama hizo kama wanataka kuendelea na kazi ya kulitumikia jeshi la polisi basi wahakikishe wanafuata nidhamu na maadili ya kazi," amesema Kamanda Masejo.

Hata hivyo, Kamanda huyo amesema kwa sasa hawezi kuwaweka wazi waliofukuzwa kwani bado upelelezi unaendelea wa kuwachunguza askari wengine na wataendelea kuchukuliwa hatua za kinidhamu na wale watakaobainika kuvunja sheria za nchi basi watawafikisha katika mikono husika.

Chanzo: IPP Media
 
Back
Top Bottom