Askari polisi wanne mbaroni kwa tuhuma za ujambazi

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Na Mwandishi Wetu, Kigoma Yetu


ASKARI polisi wanne wa kituo cha Polisi Mkugwa kilichopo Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma wanashikiliwa kwa tuhuma za ujambazi baada ya kumpora mwanamke mmoja kiasi cha shilingi milioni mbili na kumjeruhi vibaya kwa mapanga na marungu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Bw. Venance Mwamoto alisema tukio hilo limetokea usiku wa September 18 mwaka huu katika kijiji cha Kifura, ambapo askari hao walimvamia mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Bi Jenisia Minani mwenye umri wa miaka 36 wakati alipokuwa akitoka dukani kuelekea nyumbani kwake.


Aidha askari hao ambao hawakutajwa majina yao walifanikiwa kukimbilia katika kituo cha polisi cha Kifura ambapo wananchi wenye hasira kali walikusanyika kwa lengo la kwenda kuwashambulia.


Katika tukio askari ambaye hata hivyo hakufahamika jina lake mara moja alitokeza kuutuliza umati wa wananchi hao lakini jitihada zake zilikoleza moto wa wananchi hao wakidai kutoamini jeshi la polisi na kuomba kuonana na Mkuu wa Wilaya.


Wananchi hao wenye hasira kali walikusanyika na kukivamia kituo cha polisi wakiwa na mapanga na marungu na silaha mbalimbali wakidai kuwa waliofanya kitendo hicho cha kumpora pesa mwanamke huyo na kumjeruhi ni polisi hivyo watolewe nje ili wauwe

Mkuu wa wilaya hiyo Bw Mwamoto alilazimika kuwasha gari usiku wa saa nane kuelekea kwenye tukio baada ya kupigiwa simu ili kuwatuliza wananchi hao ambapo aliahidi kulifanyia kazi swala hilo.

Bw Venance Mwamoto ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya kibondo alisema kuwa wanatarajia kuunda tume ndogo kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo.


Bi Jenisia ambaye alijeruhiwa vibaya katika tukio hilo amelazwa katika hospitali ya wilaya ya kibondo kwa matibabu zaidi.

Blogzamikoa


www.blogszamikoa.blogspot.com
 
Hivi Askari wetu kwa UTOVU wa NIDHAMU na PIA kutokuwa waangalifu bila kuzingatia NGUZO za kuwa POLISI bora ni Sababu ya KAZI zao za USIKU?

Wengi ambao wanafanya kazi USIKU ili kujipatia MALI roho zao ni kurutu haswa, Sasa ukiwapa kazi DAY-TIME ukurutu wao bado upo na hawafuati

Sheria zao za KIPOLISI... Kweli NCHI inaendelea Ingekuwa BORA kama kwenye UAJIRI wa POLISI - MWIKO Darasa la Saba

Inaanzia FORM II Falsifier

Tuna Wageni wengi toka NJE sababu ya MADINI, GAS, URANIUM nadhani polisi wetu lazima wawe na CLASS fulani Darasa la Saba No

Inaanzia FORM IV - Walioshindwa Mapolisi wa Kawaida

Form IV waliofaulu wanaanzia VYEO VYA JUU

Form VI Hapo itauplift our POLICE FORCE to be MORE EDUCATED; GOOD Salaries and better residential...
 
He did a good thing to have a wife and responsible life. This finding if anything, is going to help us get rid all of lies we are always bombard with about religion. All religions have something fishy to hide. That's why when they are roughed a wrong place they tend to use violence. If it bleeds it leads. This will help those who still labour under the slumber of belief to think twice and afresh. Thanks to the guys who were able to jimmy this myth out.
 
hawa ni kama wale wa morogoro aliyewasema marehemu dunga, mpaka wakamnyonga!
 
He did a good thing to have a wife and responsible life. This finding if anything, is going to help us get rid all of lies we are always bombard with about religion. All religions have something fishy to hide. That's why when they are roughed a wrong place they tend to use violence. If it bleeds it leads. This will help those who still labour under the slumber of belief to think twice and afresh. Thanks to the guys who were able to jimmy this myth out.

Lugha gongana!!the kwi kwi
 
Siyo lugha gongana bali nimejaribu kutuma ujumbe huo kwenye sehemu wanaposema wamegundua kuwa kumbe Yesu alioa wakaniambia sina privileges nami nikaamua kujipa hizo priv. na kuitundika hapo na kwingineko.
 
huyo mama ashukuru mungu wajomba hawakuwa na uniform otherwise sasa hivi tungekuwa tunazungumzia taratibu za mazishi
 
Hao ndio askari tuliowaamini na kuwapa madaraka ya kulinda raia na mali zao!

PM anakuambia LIWALO na LIWE!

Iko siku yao itakuwa ngumu!
 
sijui lini polisi wa mjini Arusha wataanza kukamatwa maana matapeli wengi mjini Arusha ni polisi, ujambazi wowote kwa nafasi unawezeshwa na jeshi la polisi..
 
Back
Top Bottom