Askari Polisi waandika barua kwenda kwa Waziri Lugola wakimtuhumu OCD Serengeti kutembea na wake zao, wachumba zao na kuomba rushwa

kwa sheria za jeshi, mkubwa wako aliekuzidi cheo, hata akikukuta uko bar na mke wako mmekaa, inabidi usimame, umpigie saluti na umpishe akae na mkeo, hakuna kuhoji, askari wa kike hakuna kukataa chochote utakachoombwa na mkubwa wako.
Fala kweli wewe mzaramo punda wa Rufiji, hiyo ni sheria za CCM
 
Askari Polisi waandika barua kwenda kwa Waziri Lugora wakimtuhumu OCD Serengeti kutembea na wake zao, wachumba wao

Pia OCD huyo amekuwa akiomba rushwa ya ngono kwa askari wa kike


Mkuu wa kituo Cha Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara (OCD) Matthew Mgema, ameingia katika kashfa nzito ya kuomba rushwa ya ngono fesha kutoka kwa askari wa kike na wa kiume.

Mkuu huyo wa kituo cha polisi amesababisha kuvunjika kwa ndoa za askari wake anaowaongoza na wengine kuwatengenezea skendo ambazo zimesababisha wahamishwe vituo vya kazi.

Barua tuliyoipata iliyoandikwa na askari Polisi hao, ambao wamechoshwa na vitendo hivyo, inaeleza namna OCD huyo anavyofanya vitendo vya kinyanyasaji kwa askari wenzake.

Barua hiyo imeandikwa kwenda kwa RPC Mara na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugora ili aweze kuwasaidia Polisi hao ambao wananyang'anywa wake na wengine kunyang'anywa wachumba wao na OCD huyo.

Kulingana na barua hii na vitendo vichafu vinavyoendelea kufanyika Serengeti, Waziri Lugora hakikisha unafanya ziara ya haraka Serengeti kwa kuwa vitendo hivyo vinahatarisha usalama kwa askari wako.

Pia OCD huyo ametengeneza mtandao ndani ya askari wake ambao wanashirikiana kuchukua rushwa kutoka kwa watuhumiwa wa uwindaji haramu kwenye mbuga ya serengeti.

Pia amekuwa akitumia mtandao huo wa askari wasiokuwa waaminifu kuchukua pesa kwa wafanyabiashara na watuhumiwa wengine wanaokamatwa kwa tuhuma mbalimbali na fedha zinazopatikana wamekuwa wakigawana.


Soma chini barua hii ya askari walioiandika kwenda kwa Waziri Lugora na RPC Mara.

Na hii timu ya Ocd anayotumia kuchukua rushwa na mambo mengine.

G-6873 D/C Benson..G-5805 D/C Christophe..G-3633 D/C peter..G-4209 D/C Steve..!

BY CHARLES CHARLES


Baharia huyo ajali kazini
 
So sad,if it is real. Nidhamu katika kazi ni mhimu,ata kama wewe ni boss lazima taratibu zifuatwe.Pia suala la ndoa lazima liheshimiwe na wanandoa wenyewe kama utasimamia msimamo wako,nahisi hilo haliwezi tokea,wangemfanyia mtego kwa PCCB mambo yangekuwa yameisha siku nyingi.
 
Hizo namba zimewekwa hadharani, natamani niwapigie hao WP nijiridhishe kama ni waaminifu kwa waume zao.
 
Moja ya sheria za kijeshi ni "kosa askari kutembea na mke wa askari mwenzake au mke wa raia yoyote au kutembea na mtoto wa askari mwenzake." akijulikana askari anafukuzwa kazi bila hata kujadili.
Ina maana endapo mtoto wa Askari akanipenda kwa hiari sitaruhusiwa uhusiano ikiwa na mimi ni Askari? naomba uweke sawa hiyo sheria tuielewe
 
Kama huyo OCD ana hizo tabia kwanini wameshindwa kumtega? Hao askari dhaifu sana, sasa wanawezaje kulinda raia na mali zao? Kwanini wanaogopa uhamisho? na kwanini wanaonea wivu wenzao wanaopelekwa Nyamongo? Askari acheni UNAFIKI!!
 
Kama Askari Hajui Haki Zake Na Hatua Za Kisheria Za Kuchukua Je Raia Wa Kawaida Itakuwaje Yakimkuta.

Ndio Maana Tuna Jeshi La Polisi La Kipumbavu Sana Nchi Hii!

Polisi Gani Hajui Haki Zake Na Sheria Anashindwa Kuwatafuta Takukuru Wakaweka Mtego Na Wakamkamata Na Ushaidi Juu?
Polisi haijafikia levo ya kuishiwa mbinu eti waombe Raia(PCCB) kuja kuingilia mambo yao ya ndani.
Polisi wana itifaki zao za 'kusokotana'.
 
Sasa hapo kosa la ocd au wake zao? Wakati mwingine huwa naona Tanzania hizi ndoa ni kama kulazimishana tu, hivi kweli Mke wako anasex na Mwanaume mwingine halafu unakwenda kumlalamikia mwingine? WTF!
Mtuhumiwa nakuona umekaa kitu cha mbele
 
kwa sheria za jeshi, mkubwa wako aliekuzidi cheo, hata akikukuta uko bar na mke wako mmekaa, inabidi usimame, umpigie saluti na umpishe akae na mkeo, hakuna kuhoji, askari wa kike hakuna kukataa chochote utakachoombwa na mkubwa wako.
Sina uhakika kama standing orders za jeshi la polisi zinasema hivyo mkuu! Ninachojua askari inabidi kutii amri halali tu. Sasa hayo unayosema sijui kama ni kati ya amri halali.
 
Ingia wikipedia au soma sheria za kijeshi zimenamtambuaje policeman halafu niletee maana ya raia.
Wewe kila siku unabishana na watu hapa kuhusu ujeshi wa polisi,wenzenu wanaangalia matendo kama haya.askari kamili hafanyi ungese kama wa hawa wananchi walioandika hiyo waraka.

Simply huu ni uraia kiwango cha phd,embu eleza ni kwanini msichunguzwe na taasisi nyingine kama mmeshindwa kujiongoza!!!
 
Nyinyi wote raia tu
In general, a civilian is "a person who is not a member of the military or of a police or firefighting force" wikipedia, kamanda huko jeshini uliingia kwa elimu ya std 7 au vipi unaniangusha!! kasome military law ujiridhishe kama ulichosema ni kweli kama sheria ya jeshi la Tz inazingua basi kasome sheria ya kimataifa ya majeshi iliyo undwa Geneva halafu ukielewa itakuwa kwa faida yako.
 
Mimi pia sijapenda huu uraia wao hao polisi wa Serengeti ndio maana nikasema 'Polisi wana itifaki zao za kusokotana'
Wewe kila siku unabishana na watu hapa kuhusu ujeshi wa polisi,wenzenu wanaangalia matendo kama haya.askari kamili hafanyi ungese kama wa hawa wananchi walioandika hiyo waraka.

Simply huu ni uraia kiwango cha phd,embu eleza ni kwanini msichunguzwe na taasisi nyingine kama mmeshindwa kujiongoza!!!
 
Back
Top Bottom