Lwamadovela
JF-Expert Member
- Mar 5, 2019
- 325
- 235
miaka ya nyuma ilitokea pale makete mkuu wa kituo kuhusiana na wake wa maaskari. siku moja askari akiwa lindo akatonywa bosi yuko kwa mke wake. jamaa aliondoka lindoni kwenda nyumbani. alipofika akamkuta mkewe pekeyake. jamaa hakuamini!akachungulia uvunguni mwa kitanda akaona bosi amejilaza. Jamaa akalikoki. Akammaliza hukohuko. Serengeti mnafeli wapi!?Askari Polisi waandika barua kwenda kwa Waziri Lugora wakimtuhumu OCD Serengeti kutembea na wake zao, wachumba wao
Pia OCD huyo amekuwa akiomba rushwa ya ngono kwa askari wa kike
Mkuu wa kituo Cha Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara (OCD) Matthew Mgema, ameingia katika kashfa nzito ya kuomba rushwa ya ngono fesha kutoka kwa askari wa kike na wa kiume.
Mkuu huyo wa kituo cha polisi amesababisha kuvunjika kwa ndoa za askari wake anaowaongoza na wengine kuwatengenezea skendo ambazo zimesababisha wahamishwe vituo vya kazi.
Barua tuliyoipata iliyoandikwa na askari Polisi hao, ambao wamechoshwa na vitendo hivyo, inaeleza namna OCD huyo anavyofanya vitendo vya kinyanyasaji kwa askari wenzake.
Barua hiyo imeandikwa kwenda kwa RPC Mara na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Kangi Lugora ili aweze kuwasaidia Polisi hao ambao wananyang'anywa wake na wengine kunyang'anywa wachumba wao na OCD huyo.
Kulingana na barua hii na vitendo vichafu vinavyoendelea kufanyika Serengeti, Waziri Lugora hakikisha unafanya ziara ya haraka Serengeti kwa kuwa vitendo hivyo vinahatarisha usalama kwa askari wako.
Pia OCD huyo ametengeneza mtandao ndani ya askari wake ambao wanashirikiana kuchukua rushwa kutoka kwa watuhumiwa wa uwindaji haramu kwenye mbuga ya serengeti.
Pia amekuwa akitumia mtandao huo wa askari wasiokuwa waaminifu kuchukua pesa kwa wafanyabiashara na watuhumiwa wengine wanaokamatwa kwa tuhuma mbalimbali na fedha zinazopatikana wamekuwa wakigawana.
Soma chini barua hii ya askari walioiandika kwenda kwa Waziri Lugora na RPC Mara.
Na hii timu ya Ocd anayotumia kuchukua rushwa na mambo mengine.
G-6873 D/C Benson..G-5805 D/C Christophe..G-3633 D/C peter..G-4209 D/C Steve..!
BY CHARLES CHARLES