Askari Polisi Wa Tanzania Police Academy Ajiua Kwa Kujipiga Risasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari Polisi Wa Tanzania Police Academy Ajiua Kwa Kujipiga Risasi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MegaPyne, Jul 3, 2010.

 1. Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi

  DAR ES SALAAM JUMAMOSI JULAI 3, 2010

  Askari polisi mmoja ambaye ni Mkufunzi wa Tanzania police Academy, Konstebo Noel Paul Jenga33), amejiua leo kwa kujipiga risasi moja kichwani akiwa kwenye chumba cha kutunzia silaha kwenye Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

  Mkuu wa Tanzania Police Academy SACP Alice Mapunda, amesema kuwa Kostebo Noel Jenga, amejiua majira ya saa moja asubuhi baada ya kupokea zamu ya ulinzi katika kituo kidogo cha Polisi cha Mfano, kilichopo Chuoni hapo.

  SACP Mapunda amesema kuwa mara baada ya kupokea zamu ya ulinzi askari huyo aliwaruhusu wenzake waliokesha kwa ulinzi katika kituo hicho kisha kuandika taarifa ya kusudio lake la kujiua kwenye kitabu maalum cha shughuli za zamu maafufu kama OB.

  Katika taarifa hiyo, iliyoandikwa saa 12.45 asubuhi, Konstebo Noel Jenga, alisema kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa hiyari yake bila ya kulazimishwa na mtu yoyote na ameomba asisumbuliwe mtu yeyote kutokana na tukio hilo.

  Amesema baada ya kuandika taarifa hiyo, Konsetebo Noel Jenga, alianza kuwapigia simu baadhi ya nduguzake kuwaaga buriani na baada ya kumaliza kufanya hivyo alizima simu na kisha kuweka mtutu wa bunduki mdomoni na kujifyatulia risasi ambayo imesababisha kifo chake.

  Marehemu Noeli alizaliwa Desemba 25, 1977 huko mjini Morogoro na baadaye kupata elimu ya msingi katika sule moja mjini Morogoro tangu mwaka 1986 hadi 1992 na kujiunga na masomo ya Sekonda kwenye Shule ya Sekondari ya Center mjini Dodoma kati Ya mwaka 1993 na 1996 kabla ya kujiunga na kidato cha tano na cha sita katika shule ya Sekondari ya Forest mjini Morogoro kati ya mwaka 1998 na 2000.

  Alijiunga na Jeshi la Polisi katika Chuo cha polisi cha Kimataifa cha CCP cha Mjini Moshi mkoani Kilimanjaro mnamo Septemba 25, 2000 na kuhitimu mafunzo ya awali ya uaskari Polisi Mei 25, 2001.

  Mara baada ya kumaliza mafunzo hayo alipangiwa mkoa wa Iringa ambapo alipelekwa katika kituo cha Polisi Ludewa kabla ya kuhamishiwa CCP Moshi mkoani kama Mkufunzi mwaka 2006 na kutokana na juhudi yake ya ukufunzi alihamishiwa katika Chuo Kikuu cha Polisi Jijini Dar es Saam ambacho sasa ni Tanzania Police Academy.

  Kamanda Mapunda amesema kuwa Polisi wameanza uchunguzi wa chanzo cha kifo cha marehemu na kwamba mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kwao Morogoro inafanywa.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Frustrations za maisha kama madeni, magonjwa yasiyotibika, ugomvi wa kifamilia n.k ndiyo shida kubwa za hawa jamaa wanaojiondoa kwa njia hizi!...Pole familia yake!
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Apumke kwa amani: Ndo matokeo ya kukata tamaa katika maisha, na pengine kutokuwa na mtu wa kumshirikisha shida zako hata kama hazitatui lakini zitakusaidia kupmua/ kutoa tension iliyojaa ndani ya moyo.
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  OOoh, Poleni sana. Hadithi kama hizi zinatia simanzi ingawa hatujui kwanini aamue kufanya kitu kama hicho
   
Loading...