Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Askari wa jeshi la polisi Koplo George Braiton aliyepigwa risasi na majambazi wakati akikabiliana nao katika tukio la ujambazi lililotokea barabara ya sita na saba jijini Tanga amefariki dunia.

Koplo Braiton amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Mkoa wa Tanga,Bombo, akiwa na watu wengine wawili waliopigwa risasi katika tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga ACP.Mihayo Msikhela amesema kuwa bastola ilitumika kupoteza uhai wa Koplo George Braiton wa kituo cha polisi Chumbageni na kujeruhi raia wengine wawili ambao bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga.

Polisi wamesema walifanikiwa kuwakamata majambazi hao wakiwa na bastola walioitumia kwenye tukio hilo pamoja na visu wanavyovitumi kwenye matukio ya kihalifu.

Majirani waliokuwa wakiishi na Koplo Braitoni wamesema tukio hilo limewagusa,lakini wakaiomba jamii kuwafichua wahalifu kwa lengo la kukabiliana na vitendo hivyo.

Kolpo Braitoni anatarajiwa kusafirishwa kupelekwa mkoani Mara Februari 16 kwa ajili ya mazishi.

Chanzo: Star TV

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kukumbana na matukio ya kupigwa riasasi
- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

- Kifo chenye utata cha Waziri Nicas Mahinda

- John Mwankenja auawa kwa risasi

- Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

- Dkt. Wilbert Kleruu - Utata wa kifo chake, historia na maisha yake

- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

- TANZIA - Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

- Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

- Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

- Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana
 
“Mimi kama Amiri Jeshi Mkuu wa nchi, nawahakikishia usalama wa Zanzibar na Bara, kwa yeyote atakayeleta fyokofyoko ataona,” amesema na kuongeza;

“Iwe Ukerewe, Nachingwea, Dodoma, Pemba, Zanzibar popote pale, wajue vyombo vya usalama vipo kwa ajili ya kuwashughulikia.”

Hili walilofanya majambazi Tanga ni fyokofyoko au " uzombie"?

Akizungumzia uvumi uliojitokeza wa kuwapo kikundi cha vijana wanaopiga watu katika badhi ya maeneo maarufu kama 'Mazombi', Balozi Seif alisema hana taarifa yoyote iliyomfikia akiwa kama kiongozi wa juu wa serikali kuhusu shutma hizo.

Hata hivyo, alitoa agizo kwa vyombo vya ulinzi kufanya uchunguzi dhidi ya shutuma hizo na pale itakapobainika kuwapo kwa vitendo hivyo, juhudi za kuwakamata wahusika zichukuliwe na kuwafikisha mbele ya sheria.

Link Rais Magufuli agoma kutatua mgogoro Z’bar
Link2. Home
 
Pumzika kwa Amani poti. Jambo la msingi ni kwamba hao majambazi wamekamatwa....Hongera kwa Jeshi la Polisi.
 
Back
Top Bottom