Askari Polisi Ajinyonga akiwa Guest House na kuacha ujumbe, "Maisha hayana maana"

Nyuki Mdogo

JF-Expert Member
Oct 31, 2021
4,138
10,538
askari Polisi wa kituo cha kati cha Dar es Salaam (jina kapuni) amekutwa amejiua kwa kujinyonga katika nyumba ya kulala wageni.

Askari huyo kabla ya kujitoa roho aliacha jumbe mbali mbali mojawapo ni kudai kuwa "maisha hayana maana"

Askari huyo alijaribu kujizuia kujiua mara kadhaa lakini ikashindikana.

Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio la askari wake kujitoa uhai.
 
Majeshi ajirini watu waliofaulu mitihani, hizo four na zero IPO siku watatumia hizo silaha kuua wengine kisha na wao kujiua.

MTU aliyepata four au zero hata akiachwa na mwanamke anaumia sana kutokana na reasoning capacity YAKE kuwa chini, atachukua SMG+risasi 30.....
 
Majeshi ajirini watu waliofaulu mitihani, hizo four na zero IPO siku watatumia hizo silaha kuua wengine kisha na wao kujiua.

MTU aliyepata four au zero hata akiachwa na mwanamke anaumia sana kutokana na reasoning capacity YAKE kuwa chini, atachukua SMG+risasi 30.....
mengineyo sawa Mkuu ila mapenzi hayahitaji IQ kubwa kuyaendesha.
 
Kimeumana....... waliona sifa kukiweka chama cha magundu madarakani, sasa wanajipukutisha tu wenyewe.

Anaandika Ndugu MalisaGJ
TATIZO LA KUJIUA KATIKA JAMII

"Kwako mke wangu
(Mama Derick). Naomba nisamehe sana kwa maamuzi haya. Maisha kwangu hayana maana tena, nisamehe sana. Nimejitahidi nimeshindwa naomba uwatunze watoto wetu” sms ya mwisho ambayo Sajenti William Giriango Chacha (40) askari wa JWTZ alituma kwa mkewe, dakika chache kabla ya kujinyonga kwa mkanda wa suruali huko Dodoma.

#MyTake:
1. Tatizo la afya ya akili ni kubwa sana kwenye jamii zetu kuliko tunavyofikiri. Kuna haja ya serikali, wadau mbalimbali (NGOs) na jamii kwa ujumla kuchukua hatua za makusudi za kukabiliana na tatizo hili.

2. Ukipata tatizo hata liwe kubwa kiasi gani jitahidi kuzingumza, usikae kimya. Kuzungumza kunapunguza risk ya kufanya maamuzi mabaya ikiwemo kujidhuru.

3. Hakuna binadamu ambaye ni bingwa wa matatizo. Uwe tajiri, maskini, mnene, mwembamba shida haichagui. Hakuna watu majasiri kama wanajeshi. Lakini pamoja na ujasiri wake, Sajenti Chacha ameshindwa kuonesha ujasiri huo kwenye matatizo, hatimaye ameruhusu matatizo yamshinde.

4. Kujiua kwa sababu ya matatizo ni kuwaachia matatizo makubwa zaidi uliowaacha. Mke na watoto wa Chacha wanaenda kukabiliana na changamoto nyingi za maisha baada ya baba yao kujiua, kuliko changamoto walizokua nazo baba yao akiwa hai.

5. Kama unaipenda familia yako, mkeo, watoto, na ndugu zako, usijiue. Kujiua ni ubinafsi. Kujiua ni njia rahisi ya kumaliza matatizo yako lakini kuacha matatizo makubwa zaidi kwa ndugu zako na marafiki. Kujiua ni kuacha alama ya maumivu isiyofutika kwa familia yako.

6. Matatizo yakikuzidi hakikisha huwi peke yako. Hakikisha unaye wa kumwambia hata kama una uhakika hawezi kukusaidia, we mwambie tu. Kushare matatizo yako ni sehemu ya healing process. Ni psychosocial therapy.!
 
Majeshi ajirini watu waliofaulu mitihani, hizo four na zero IPO siku watatumia hizo silaha kuua wengine kisha na wao kujiua.

MTU aliyepata four au zero hata akiachwa na mwanamke anaumia sana kutokana na reasoning capacity YAKE kuwa chini, atachukua SMG+risasi 30.....
Ishu sio kufaulu ama kutofaulu. Hivi vifo lazima vitushtue kama Taifa.
Watu wengi wana matatizo ya akili katika jamii zetu, na mbaya zaidi hakuna ufumbuzi wa suala hilo.
 
askari Polisi wa kituo cha kati cha Dar es Salaam (jina kapuni) amekutwa amejiua kwa kujinyonga katika nyumba ya kulala wageni...
Ukute walihusika kuwadhulumu haki ya kuishi baadhi ya Watu, unajua kuna Watu wao kulipiza kisasi ni LAZIMA Tena kimya kimya.

Polisi wengi ni katili sana with expectations za kuwa na maisha Mazuri.
 
Back
Top Bottom