Askari mstaafu: Walichofanya Mdee na wenzake pale Segerea ni sawa na Gari kugonga Treni kwenye "Railway cross Road"

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Aug 14, 2012
6,663
2,000
johnthebaptist,
Kwa Watz wenye akili hii NI propaganda ya kuhalalisha ujinga na ubabe wa Utawala huu wa Kidikteta..!!

Swali ni: Je, Polepole na CCM yao walipokwenda KUMPOKEA Mashinji na baadae KUTAKA KULAZIMISHA kumpokea Mhe. Msigwa wa CHADEMA walipitia mlango gani wa Railway Crossing ya SEGEREA...???? CCM ACHENI kuwafanya Watz kuwa mandondocha please!
 

Laptop001

JF-Expert Member
Jan 18, 2020
204
250
Kustaafu Ni Pale Mtu Anapotimiza Umri Husika,huyu Hakuondolewa? Kama Aliondolewa Tuseme Afisa Aliyeondolewa,kustafu Kuna Hadhi Yake
 

MwajabuOmary

Senior Member
Jul 11, 2013
191
250
Jamani pale Segerea kuna mageti mawili kabla yakuingia lango kuu la kuingia ndani ya gereza.Maana yake nim kwamba kabla ya lolote lazima uanze kuhojiwa geti kuu la kwanza ambalo lipo karibu na barabara iendayo Kinyerezi, hapo utahojiwa askari wa zamu akijiridhisha ndipo utaruhusiwa kwenda hatua ya pili ambapo kuna geti la pili.

Pale napo utakuta kuna askari ambao watakuhoji na kukukagua na kukuhoji,wakijiridhisha ndipo watakuruhusu uende kwenye lango la mwisho litakalo kuwezesha wewe kuingia ndani ya gereza. Kumbukeni geti la kwanza na la pili linakuwezesha wewe kuingia ndani ya maeneo ya magereza na sio kuingia ndani ya gereza. Ni lango/geti la tatu ndio linakuwezesha kuingia ndani ya gereza.

Mahala walipokuwepo watu waliokwenda kumpokea Mbowe ni nje ya geti la kwanza ambalo lipo karibu na barabara iendayo Kinyerezi na watu hao walikua ndani ya magari yao.Wananchi hao hawakua na silaha yoyote, hawakua katika maeneo hatarishi kwa jeshi la magereza,kwa kuwa hawakua ndani ya maeneo hatarishi.

Nguvu iliyotumika kuwadhibiti wafuasi wa Mbowe ni kubwa mnnooooooo, kwa kuzingatia jinsia ya wanaume kuwadhibiti wanawake na wakiwa na silaha za moto.
Huyo Mwakibinga kapitiwa na ameshindwa kusema ukweli kwa ajili ya itikadi.
 

Mkereketwa_Huyu

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
8,000
2,000
Hivi mtu yuko chini ya ulinzi kisha anachana sare ya polisi ataachiwa huru kweli? Hawa wana bahati kweli, ndo ingekuwa mimi walai watu wangekuwa wanazika sasa hivi. Watu wanapenda sana kutafuta sifa kwa kulazimisha.
 

mhangahikaji

Member
Aug 13, 2013
65
125
Jay One, Nadhani hayo maelezo yako ni kwa mujibu wa askari wenyewe but ukisikilza na upande mwingine wanasema kuna wachache waliruhusiwa kuingia hadi gate fulani. Wengi wao waliambiwa wabaki nje na kwa mujibu wa maelezo yao walitii. Lakini Kama vile kulikuwa na mkakati fulani zilipigwa filimbi na kuanza kushambuliwa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,813
2,000
Nadhani hayo maelezo yako ni kwa mujibu wa askari wenyewe but ukisikilza na upande mwingine wanasema kuna wachache waliruhusiwa kuingia hadi gate fulani. Wengi wao waliambiwa wabaki nje na kwa mujibu wa maelezo yao walitii. Lakini Kama vile kulikuwa na mkakati fulani zilipigwa filimbi na kuanza kushambuliwa!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio kweli, walienda kwa makelele na shangwe za CHADEMA hadi getini Segerea Magereza, wakawa askari wanawatuliza akina Halima na wafuasi wao, wakawa hawasikii, sasa vurugu ndio zilianza hapo, kama vile ilivyokuwa wafuasi wa Chadema pale Mahakama ya Kisutu walivyofukuzana na polisi.

Mtindo huo huo walienda nao Magereza, wakajidanganya wako wengi nakudhania Magereza hawana nguvu kama polisi, walitiwa adabu ila ilikuwa ndogo, wakaanza kulia lia FFU dio wakaja kuwakamata. Ujue useme usemavyo, ukishaenda nyumba ya mtu na vurugu zimetokea kwake, ww ndio makosa yako kwako, sbb umetoka kwako hadi Magereza na kuleta fujo na uvunjifu wa amani. Hivyo adhabu yao najua itakuwa kubwa sana. Nimewadharau sana akina Halima.

Wenyewe wangeenda kimya kimya wanamchukua mwenyekiti wao tena angetoka na waende zao bila hata kelele au kujimwambafai magereza. Sbb ujue jeshini amri ndio inafanya kazi, sasa ukileta ujuaji utavunjwa ujuaji wako na unaweza poteza maisha kijinga tu.
 

Bana likasi

JF-Expert Member
Jan 7, 2020
6,937
2,000
Jay One,
Kwahiyo waliyavunja mageti yote wakaingia ndani wawatoroshe wafungwa,kila mmtu uongea lake CCTV ingekuwapo ingesema ukweli
 

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,585
2,000
Labda nianza kwa kuandika kuwa mimi si mwanaCCM na sitakuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa Tanzania mpaka mifumo ya siasa itakapobadilika nchini.

Nina kadi mfu( isiyolipiwa) ya uanachama wa CHADEMA tangu 2015. Kitendo cha kwenda kutia fujo au kelele lango la magereza kilichofanywa na baadhi ya viongozi wa Chadema hakikubaliki.

Yes, may be mlionewa lakini ndio muanze kuchukua credit kwenye kambi ya jeshi!!!
Kulikuwa na ulazima gani wa kukodi magari ili mufanye msafara kuelekea gerezani?
Kitu kimoja hamjakitambua bado; mtawala si mwepesi kama mnavyofikiria, pili mmeshindwa kutambua kuwa mtu yeyote anayelala na bunduki(askari) akili yake si sawa na raia.

Someni nyakati mtakuja kufa kizembe na hiyo hali msiipate. Kwanini sherehe ya mapokezi ya Mh.Mbowe hamjasubiri ifanyike ofisini kwenu?

Hata wale maaskari wangewaua msingepata haki mahakamani na wazungu wangeishia kuandika barua za masikitiko tu then maisha yangeendelea.

Mdee Halima namkubali sana, hata wakati wa uchaguzi wa ndani nilimwandikia SMS ya kumwomba agombee nafasi ya uenyekiti ili azibe nafasi iliyopwaya ya Mh.Mbowe.

Halima Mdee kama utausoma ujumbe huu nadhani utanikumbuka but kile ulichokifanya juzi ni utoto, Mdee umesahau Ruvu tulikufundisha kwata ya kupambana na wanaoandamana and we told you that some about that.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom