Askari magereza wafanya vurugu kubwa mizani ya magari watoa kipigo na,kuvunja meza

mopaozi

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
3,301
520
Habari nilizozipokea hivi punde kutoka kwa mdau wangu wa mikoani kuwa askari magereza waliokuwa wakielekea Mbeya wakirudi wakitokea kwenye gwaride la muungano wamefanya vurugu kubwa kwenye mizani baada ya basi walilokuwa wamekodi la kampuni ya Muro kuwekwa korokoroni kwa kushindwa kulipa faini ya kuzidisha uzito,askari hao hawakutaka kuelewa wala kuruhusu wenye basi kulipa faini walianza kutoa kichapo kwa watu wa mizani na kuvunja meza,viti na samani hadi askari polisi walipoingilia kati kutuliza fujo hizo.Nawasilisha
 
Hao nao mizani wanapenda sana rushwa!!!!acha wachapwe kidogo wapate heshima...ma bus ya chasis kubwa maana yalikuwa malori hakuna mzigo wowote wa maana ukiangalia....wenzao wameungua jua mwezi mzima wameacha familia wamechoka pia wamedhulumiwa posho zao wana hasira...

Ila kama wamechemsha wachukiwe hatua kali za kinidhamu za jeshi la magereza!!
 
Watakuwa wamelipwa posho kwa kukaa juani sasa wanakula viroba kwenye basi wapunguze stress sasa yamewakuta. Poleni masoldier!
 
Hivi wana haki gani kutoa kichapo na kuvunja samani wao ni kina nani wazuie sheria kufanya kazi au sheria ni kwa wanyonge tuu!!
 
Hivi wana haki gani kutoa kichapo na kuvunja samani wao ni kina nani wazuie sheria kufanya kazi au sheria ni kwa raia wanyonge tuu!!
 
Wafanyakazi wamizani wameyataka!

Kwahiyo ulitaka wawaachie waendelee kuharibu barabara kwakuwa wao ni askari,je ukiwa askari unahaki ya kuvunja sheria basi wote tuwe maaskari
 
Kwahiyo ulitaka wawaachie waendelee kuharibu barabara kwakuwa wao ni askari,je ukiwa askari unahaki ya kuvunja sheria basi wote tuwe maaskari
Wale wa JW mbona huwa hawapimi vifaru wanavyo safirisha?Unajua kifaru kina tani ngapi wewe?
 
Watakuwa wamelipwa posho kwa kukaa juani sasa wanakula viroba kwenye basi wapunguze stress sasa yamewakuta. Poleni masoldier!
Mbona una jikanyaka....kuna kila dalili hawajalipwa posho hivyo wana stress ndiyo maana wakaamua kuzimalizia kwa wahusika wa mizani...serikali imefilisika kuna walimu hawajaripwa mwezi wa tatu huu....
 
Habari nilizozipokea hivi punde kutoka kwa mdau wangu wa mikoani kuwa askari magereza waliokuwa wakielekea Mbeya wakirudi wakitokea kwenye gwaride la muungano wamefanya vurugu kubwa kwenye mizani baada ya basi walilokuwa wamekodi la kampuni ya Muro kuwekwa korokoroni kwa kushindwa kulipa faini ya kuzidisha uzito,askari hao hawakutaka kuelewa wala kuruhusu wenye basi kulipa faini walianza kutoa kichapo kwa watu wa mizani na kuvunja meza,viti na samani hadi askari polisi walipoingilia kati kutuliza fujo hizo.Nawasilisha

Mdau ni mzani wa wapi? Msafara huo nimeufuatilia tayari umeashaingia Mbeya na saizi unaelekea Kiwira. Mbeya au Iringa kuna mzani?
 
Back
Top Bottom