Askari Magereza aamriwa arejeshe kamera aliyompora mwandishi

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Messages
37,093
Likes
6,669
Points
280

Pdidy

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2007
37,093 6,669 280
Askari Magereza aamriwa arejeshe kamera aliyompora mwandishi
Pauline Richard

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala imemwamuru mkuu wa askari wanaosindikiza mahabusu kutoka Gereza la Ukonga, kurejesha kamera kwa mwanandishi wa habari wa gazeti la Uhuru Keneth Bujiku, baada ya kuipora kwa lengo la kumzuia kufanya kazi.

Mpigapicha huyo aliporwa kamera yake juzi baada ya kumpiga picha raia wa Afrika Kusini, Ntombekhaya Nkonk (42), aliyefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuingiza dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Sh87.5milioni.

Hakimu Joyce Minde alitoa amri hiyo baada ya waandishi wanaoripoti habari za mahakamani hapo kumlalamikia dhidi ya tukio lililofanywa na askari huyo aliyejulikana kwa jina la Sajenti Pascal.

Hakimu Minde alisema:"Kumpiga picha mtuhumiwa siyo kosa isipokuwa kama yupo katika chumba cha mahakama, lakini kabla na baada ya hapo mpigapicha yeyote anarusiwa kupiga picha," alisema Hakimu Minde na kuhoji kuwa “mbona akina babu seya walipigwa picha wakiwa gerezani?"

Mpiga picha huyo aliporwa kamera hiyo juzi baada ya kumpiga picha mtuhumiwa huyo wakati akipanda gari la Magereza lililokuwa linaendeshwa na askari huyo kuelekea Segerea.

Baada ya waandishi kutoa malalamiko hayo, hakimu huyo alimuita kiongozi wa askari hao Magereza na kumuuliza kama ana taarifa za malalamiko hayo, naye akajibu kuwa hana. Ndipo Hakimu Minde alipotoa gari la mahakama na kuwapa wandishi hao wakiwa na baadhi ya askari magereza kuelekea katika gereza la segerea kwa ajili ya kufuata kamera hiyo ambayo thamani yake haikuweza kufahamika
 

Forum statistics

Threads 1,190,580
Members 451,229
Posts 27,675,890