Askari KDU Arusha lawamani kwa kubambika kesi fundi bodaboda

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
752
1,810
waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba pamoja na waziri wa maliasili na utalii pr. Jumanne Maghembe wameombwa kuchukua hatua dhidi ya kashfa nzito kwa kikosi cha kuzuia ujangili KDU jijini Arusha kutokana na baadhi ya askari wake kukithiri kwa kubambika kesi za ujangili raia wasio na hatia.
e3e730cc9352b43e9a5e08d777e61d92.jpg

Tukio la tarehe 29/12/2017 kijana Aidan Anderw(32) fundi pikipiki mkazi wa mto wa mbu, Monduli amebambikwa kesi ya nyama ya Twiga, ambapo ,askari wa Tanapa hifadhi ya Manyara walimgonga kwa maksudi akiwa na pikipiki yake na baadae kumkabidhi KDU bila kuwa na ushahidi ama kielelezo cha hizo nyama za Twiga.

Mama mzazi wa kijana huyo anaomba msaada kwa serikali kutokana na uonevu wa kijana wake ambaye amepelekwa magereza akiwa na jereha la mshono wa operesheni Tumboni lililotokana na kugongwa na gari la Tanapa kwa maksudi

Ameomba serikali iwaajibishe askari hao wa Tanapa na KDU kwa hatua ya kutaka rushwa kwa nguvu dhidi ya uharamia huo.
 
Back
Top Bottom