Askari JWTZ apigwa na wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Askari JWTZ apigwa na wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shaycas, Jan 29, 2010.

 1. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Askari huyo wa kambi iliyopo Arusha alipigwa na wamasai walio kuwa wanachunga ng'ombe ktk eneo la jeshi,eneo ambalo linakatazwa kufanyia shughuli zozote za kiraia.
  Siku hiyo Askari huyo akiwa na wenzake walikuwa wanafanya doria ktk maeneo hayo ili kuhakikisha halitumiwi na raia,ndipo walipo wakuta wamasai hao ambao baada ya mabishano walianza kuwachapa kwa viboko askari hao na kwa bahati mbaya askari huyo mmoja akaumizwa sana.
  Sasahivi amesafirishwa kwenda hosp ya Lugalo kwa matibabu zaidi.
   
 2. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HABARI kama hizo ndo wananchi na wanahabari wanazitaka........na ndiyo habari ambazo viongozi wanazitaka........!
  JESHI GOIGOI.......JESHI OGOPEFU....JESHI LINALOINGILIWA NDANI YA MIPAKA YAKE.....JESHI LELE MAMA.......WOODEN SOLDIER........ASKARI AMBAO WANALINDA SILAHA ISIPOTEE NA SI NCHI.....!ASKARI ANAYEAMRISHWA KUOSHA VYOMBO NYUMBANI......!
  JESHI LISILO NA MENO......!
  TUNATENGENEZA MAANGAMIVU YETU WENYEWE KWA KUJENGA JESHI LA "remote control"
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  hahahaha...
  nadhani amekiona cha moto...
  sorry anyway...
   
 4. Jenerali QoyoJB

  Jenerali QoyoJB JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Asante mwana Shaycas kwa tip ngoja tumalize sehemu iliyobaki waandishi wananchi wapate hiyo.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,347
  Trophy Points: 280
  Hapo wamasai wamefanya kuokorofi.
  Kumpiga askari jeshi ndani ya eneo la jeshi ni dharau kubwa kwa askari wetu.
  Je wajeda wakirivenji mtalalamika?
   
 6. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa hata mimi nakuunga mkono
   
 7. T

  Tom JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2010
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wamasai hao lazima waadhibiwe kwa kujichukulia sheria mkononi, ntafurahi kama tayari wapo lupango.
  Nadhani askari jeshi wetu ni goigoi ama walizidiwa sana kwa idadi ya watu, maana ilibidi wawadhibiti hao wamasai, lakini si kwa kuwajeruhi. Kuwapa wamasai kibano sawa.
   
 8. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mpaka sasa hao wamasai hawajakamatwa na kilichotokea baada ya hapo ni hiki:-
  Wamasai waliokuwa wamelima mashamba yao ndani ya eneo hilo(ktk sehemu nyingine),mazao yao yamefyekwa sijui ni kwa maelekezo ya nani lakini kuna taarifa kuwa tayari bodi ya uchunguzi inafanyika kuchunguza tukio hilo la kuharibu mazao ya Wamasai hao.
   
 9. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  na askari kumpiga raia tena uraniani hadi kufa - na hapo napo utapaitaje?
   
 10. M

  Magezi JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  upuuzi mtupu......yapo mengi ya namna hiyo
   
 11. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Baaaaah! Bodi inaunda tume kuchunguza aliyefyeka mazao ya mmasai kwa hasira, na bodi itaunda lini ya kuchunguza kupigwa askari wetu tena ndani ya ngome yake? Dharau hiyo jamani........!!

  Sasa kama askari wangeamua kumalizia hasira zao kwa kuingia kwenye maboma ya wamasai kuwashikisha adabu ingeundwa tume gani? Na je, kwa kuwa wamasai wanatembea na silaha, wanajeshi wangeamua kumtembelea Armerer na kuchukuwa fimbo zao za moto kujilipiza kisasa ingekaa vipi hiyo? Askari huyo angezawadiwa kwa uvumilivu wake na wenzake kikosini, maana wamejali utu na wametunza real definition ya jeshi la walalahoi.

  Kaulize mkuu wa polisi Mbeya anazo ripoti kwenye historia za wanajeshi wa Songwe. Aliwekwa ndani askari mmoja tena kwa sababu safi kabisa kisheria, lakini waliitwa manjagu kutoka Songwe wakaja na Landrover zimesheheni wao wamevaa kombati wakapasafisha kituoni pa mapolisi mpaka kikaeleweka na wakaondoka na mtu wao.

  Siku nyingine mapolisi wanaozuia mazao njiani kutoka Kyela walilikamata gari la jeshi limebeba sukari, wajeshi wakawashukia na kuwaamuru polisi waishushe sukari waliyoikamata, lakini wasiiguse gari ya jeshi. Walishusha kidogo tu... walipogusa gari la jeshi walipewa mkong'oto mpaka wakainua mikono juu na kusalimu amri. Hawakurudia tena mpaka kesho.

  Siku nyingine waliikamata gari imebeba samaki kutoka ziwa Nyasa, kumbe ni ya mkuu wa mkoa, gari na samaki vikapelekwa polisi kituoni, lakini wakaambiwa warudishe samaki asiye na harufu ya kuoza, wakati gari imekaa mpaka kesho yake na samaki hawakuwekwa kwenye frij. Ona hapo. Ogopa jeshi usilidharau, wako tayari kufa kwa ajili yetu ati!!!!

  Sasa mmasai tu na gorole lake na kisu kwenye ala anatukana jeshi aliye kazini tena kambini??? Mungu ibariki Tanzania.

  Leka
   
Loading...