Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) John Komba (50) na wenzake watatu akiwamo binti yake mwenye miaka (17) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga wakikabiliwa na shtaka la mauaji ya kondakta wa daladala.
Washtakiwa wengine ni mgambo Warioba Nchama (28) na Bernard Semchaa (25). Kwa pamoja walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali kutokana na tukio la mauaji hayo kugusa hisia za wakazi wengi wa Tanga.
Wakili wa Serikali Denatha Kazungu, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Hilda Lyatuu alidai Januari 27, katika kambi ya jeshi iliyopo Nguvumali jijini Tanga, washtakiwa walimuua Salimu Kassim maarufu Rambo, ambaye ni kondakta.
Alidai washtakiwa walimpeleka kondakta huyo kambini ambako walimshambulia hadi akawa mahututi.
Hakimu Kazungu aliwaeleza washtakiwa kuwa hawapaswi kujibu chochote kutokana na Mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza shauri hilo kisheria kwa kuwa husikilizwa na Korti Kuu.
Kazungu aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 12 itakapotajwa na washtakiwa walipelekwa mahabusu katika Gereza la Maweni.
Mwananchi
---------------
Soma: Kipigo ndani ya kambi ya jeshi chadaiwa kusababisha kifo cha konda wa daladala